Majengo ya CCM Moshi kuchukuliwa na CHADEMA

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
Baada ya kushinda vijiji vingi katika jimbo la moshi vijijini changamoto mpya imezuka. Majengo mengi ambayo ofisi za vijiji zipo ni ofisi pia za CCM.

Katika vijiji vya Okaseni na Kimanganuni ofisi za vijiji zilijengwa wakati wa chama kimoja, na kwa kuwa CCM ndo walikuwa viongozi wa serikali za mtaa hii haiukuwa changamoo.

Sasa hatujui itakuwaje kwa kuwa CHADEMA nao wamepandisha bendera zao kwenye haya majengo, hivyo CCM sasa hawana tena ofisi katika vijiji hivi ambayo wameichagua CHADEMA 100%.

Busara inatakiwa haraka, CHADEMA watumie haya majengo kama ofisi za seriakli na wasipandishe bendera ili miaka ijayo yatumike na vyama vyote, dr. Slaa ingilia kati tafadhali.
 
Haa, haa, mkuu tunaomba kwanza utupatie matokeo ya jumla ya jimbo la moshi kabla hatujajadili hili la ofisi.
 
Kama CCM walikuwa wanapandisha bendera katika Ofisi hizo zilizojengwa na Serikali kwa nini Chadema wasipandishe bendera yao katika hiyo ofisi kwa kuwa ndo viongozi wa serikali katika hivyo vijiji. Hii ni mwanzo, siku CCM inatoka madarakani viwanja vyote na majengo yaliyojengwa na serikali na kupewa CCM yatachukuliwa.
 
Mali ya nchi na si ya chama kama walokuwamo hawakua kwa kuwafanyia ccm ni kwa kuwafanyia wa tz bas hata hao wa cdm wanastahil kuwamo, niviongoz wa wananchi na si viongozi wa chadema
 
Baada ya kushinda vijiji vingi katika jimbo la moshi vijijini changamoto mpya imezuka. Majengo mengi ambayo ofisi za vijiji zipo ni ofisi pia za ccm,

katika vijiji vya okaseni na kimanganuni ofisi za vijiji zilijengwa wakati wa chama kimoja, na kwa kuwa ccm ndo walikuwa viongozi wa serikali za mtaa hii haiukuwa changamoo,

sasa hatujui itakuwaje kwa kuwa chadema nao wamepandisha bendera zao kwenye haya majengo, hibyo ccm sasa hawana tena ofisi katika vijiji hivi ambayo wameichagua chadema 100%

busara inatakiwa haraka, chadema watumie haya majengo kama ofisi za seriakli na wasipandishe bendera ili miaka ijayo yatumike na vyama vyote, dr, slaa ingilia kati tafadhali
mkuu tuwekee matokeo ya hilo jimbo kwanza!
 
Ofisi zilizotajwa ziko kata ya Uru kusini yenye vijiji saba kati ya hivyo cdm imeshinda saba na ccm kimoja.awali cdm ilikuwa na kijiji kimoja tu cha Kariwa mwenyekiti nikiwa Mimi na nimetetea tena nafasi yangu kwa kishindo.matokeo kwa ujumla katika jimbo cdm tumeshinda 60% dhidi ya 5% za awali.
 
Safiiiiiiiiii. Acha wakome hao wavaa nguo za kijani zinazomaanisha kula mboga za majani hadi ufe!
 
Katika kata ya uru kusini mawela yenye vijiji 7, ccm wameambulia mjumbe mmoja tu wa kitongoji aitwaye yuli mushi, huyu alikuwa cdm akaenda ccm dakika za mwisho, hivi wengi walimchagua wakifikiri ni chadema,
 
ofisi zilizotajwa ziko kata ya uru kusini yenye vijiji saba kati ya hivyo cdm imeshinda saba na ccm kimoja.awali cdm ilikuwa na kijiji kimoja tu cha kariwa mwenyekiti nikiwa mimi na nimetetea tena nafasi yangu kwa kishindo.matokeo kwa ujumla katika jimbo cdm tumeshinda 60% dhidi ya 5% za awali.

mkuu hiyo ndo hali halisi
 
Baada ya kushinda vijiji vingi katika jimbo la moshi vijijini changamoto mpya imezuka. Majengo mengi ambayo ofisi za vijiji zipo ni ofisi pia za ccm,

katika vijiji vya okaseni na kimanganuni ofisi za vijiji zilijengwa wakati wa chama kimoja, na kwa kuwa ccm ndo walikuwa viongozi wa serikali za mtaa hii haiukuwa changamoo,

sasa hatujui itakuwaje kwa kuwa chadema nao wamepandisha bendera zao kwenye haya majengo, hibyo ccm sasa hawana tena ofisi katika vijiji hivi ambayo wameichagua chadema 100%

busara inatakiwa haraka, chadema watumie haya majengo kama ofisi za seriakli na wasipandishe bendera ili miaka ijayo yatumike na vyama vyote, dr, slaa ingilia kati tafadhali

Mkuu Mwikimbi ni kweli busara inahitajika vinginevyo chadema watajikuta inarudia makosa yale yale ya ccm! Kimsingi ofisi hizi zinapaswa kuhudumia wananchi wote wa eneo husika bila kujali itikadi zao za vyama! Baada ya hawa viongozi kuchaguliwa wanapaswa kuwahudumia pia wananchi wote wa eneo husika bila kujali itikadi zao za vyama! Hizi ofisi za serikali za vijiji nk zinapaswa kuwa na bendera ya Taifa tu! Vyama vyote, hata kinachokuwa kinatawala eneo husika vinapaswa kuwa na ofisi zao zinazoendeshwa kwa gharama zao wenyewe na sio kwa kodi za wananchi wasio wanachama wao!
 
Back
Top Bottom