nakubaliana nawe HK kabisa,hawa kina Dau et al wanajilimbikizia pesa yetu,hata kama leo michango yetu inapelekwa wakati shilingi ina nafuu kwa dola,itafika siku sh haina maana lakini wao watatupa hela ileile,inauma sana
Naomba niwe tofauti kidogo kwenye pension. Ni vizuri tuelewe tofauti kati ya pension na social welfare kwa maana ya un-employment benefits. Pension ni malipo ya uzeeni, wakati ambapo kwa hali ya kibinadamu mtu unakuwa hauna tena nguvu ya kuweza kuchacharika na kazi kama wakati ya ujana. Kila nchi ina umri wa 'uzee' lakini kwa vyovyote vile mzee hawezi kuwa mtu mwenye miaka 30, 35, au hata 45! Hata hivyo unaweza kuwa kwenye kundi la uzee (kwa maana ya malipo ya uzee) kama unapatwa na matatizo kazini ambayo yatasababisha wewe kutuweza kuendelea kufanya kazi e.g ajali etc.
Kwa upande wa Un-emploment benefitsm haya ni malipo kwa watu ambao wako kwenye umri wa kufanya kazi, wana uwezo wa kufanya kazi lakini kwa sababu mbalimbali hawako kwenye ajira i.e kupunguzwa, uhaba wa ajira etc. Kwa kawaida wenye kutoa hizi un-employment benefits ni 'state' kwa maana ya dola/serikali na sio shirika moja moja.
Dau na NSSF yake, PPF, PSPF, LAPF na mashirika mengine ya pension ni mashirika ya PENSION na sio un-employment benefits. Pension FUNDS zinaendeshwa kwa kanuni na masharti ya ki-pension. Zinachukua kiasi cha hela kwa wanachama na kuwekeza ili wapate faida na kuwalipa pindi pale umri wa uzee unapofikia au wanashindwa kufanya kazi kutokana na umri/magonjwa. Kama itatokea kwamba mwanachama (mfanyakazi) anakuwa nje ya ajira (mfano kapunguzwa) wakati umri wake bado ni chini ya category ya uzee hilo lilitakiwa liwe shauri la 'state'. Na hapa ndio linakuja tatizo la nchi zetu ambazo hazina kitu kinazhoitwa un-employement benefits.
Hapo kwenye red; malipo ya pension hutolewa kwa formula baada ya 'actuary' kufanya evaluation. Huwezi kuchukuwa michango ya watu (future ya watu tena wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi itakuwa imepungua) na kufanyia shughuli ambazo hauna uhakika nazo 100% kwamba zitakuwa na faida.
Pamoja na yote hayo ninao wasiwasi kiasi na 'boldness' ya NSSF kwenye suala zima la uwekezaji. Sababu kubwa hata Kingwangala anajata NSSF ni kutokana na ukweli kwamba hawa mabwana (NSSF) wamekuwa mstari wa mbele kumwaga hela kwenye miradi mingi. Nasema boldness wameji-expose sana kwenye miradi mingi, huku baadhi ikiwa na risks au ina shinikizo kubwa la kisiasa.
Nirudie Pension ni future ya watu hivyo unapowekeza hela kwa harufu ya kisiasa iko hatari ya kupata hasara maana hukufanya business decision' Na unapopata hasara maana yake mfuko (pension funds) mfuko unapungukiwa na uwezo wake kutoa au kuongeza kiwango cha pension kwa mwanachama. Hiki ndicho kinanipa shida. NSSF na wengine wanaweza kujitetea likini tumekuwa tunasoma matumizi mabaya ya resources, mikopo ambayo haijarudi. Nani analipa? Kwa vyoyote ni mwanachama.