Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,402
- 12,792
Hamba je,lilikua na mtu mmoja anaitwa Mporipori,mwinyi peku na wakeze
hahaa nimecheka sana mkuu,unakumbuka Mapung'o alishachezea hadi manchester united?
Kila zama na kitabu chake...kwa ambao tumezaliwa vijijini tulipata bahati ya kujua robo ama nusu kabisa ya yaliyokua yanajiri mjini kutokana na watunzi na masanii mahiri wa zama za nyuma kidogo..Nimekuwa mpenzi wa muda mrefu sana wa majarida tajwa hapo juu na hakika pamoja na kutokuwa na kipato wakati huo ila nilijidunduliza na kuhakikisha kila mwezi najinunulia nakala tatu kwa maana ya Sani,Bongo na Tabasamu...
Kwa kua inspired na kazi za watunzi waliobobea kama kina John Kaduma (R.I.P) E.P. Ndoda,Abrahman Dohu,4T Ndila,Dikwe Ndoto,Katembo na wengine kwa wingi wao leo najivunia matunda ya msukumo nilioupata...Mungu azipe pumziko la heri roho za wasanii na watunzi wa hadithi,riwaya na tamthiliya ambao walitupa nuru wakati digital ikiwa mapumziko ughaibuni...
Hadithi ilitungwa na Said Mbwana Makatta Bhawji. Ilikuwa inaitwa maji Mazito (Jina la Jambazi Kapuko wa Kapuko).
Da umenikumbusha mbali. Nakumbuka FAHARI lilikuwa gazeti la kawaida na jina lake lilikuwa la mwandiko mwekundu.
Nakumbuka Busara. Marehemu Mzee Hammie Rajab amepta kuandika humo. Hata character "Power Mbulumundu" aliyekuja kuchorwa na John Kaduma nadhani katika Tabasamu kwa jina la Power Mbulumbundu alitokea katika jarida la Fahari. Vituko vya Mbulumbundu/Mbulumundu vilifanana na Baba Ubaya aliyeanzia katika Jarida la KIU.
Well, niseme nini hapa!!!!!?? Honestly nimelog in ili nirespond kwa sentensi hii. Kwanza asante kwa kunikumbusha Jina la Mcheshi. Nilikuwa nawaza hawa wanawake wenye mahipsi, mapaja yanayong'aa, macho yaliyolegea, nywele za Afro na mashavu yanayomeremeta nilikuwa nawaona katika jarida gani. Heshima sana kwako "mzee" Sky Eclat.
Naomba nikuzawadie Vicky, Omari Kisila na Mzee Mkongwe.... Maji Mazito. Respect!!
View attachment 95485
FRED JIM MDOE (2013) Published on 7 Apr 2013 Jim Mdoe ni mwanahabari maarufu nchini TZ na mchapishaji wa kujitegemea mwenye uzoefu wa siku nyingi.Kwa bahati mbaya, sehemu ya mwisho ya mahojiano haya imepotea. Kanda ya awali ninayo na nipatapo nafasi nitaweka mahojiano mazima kwenye Mtandao ili watu wafaidike na mawazo yake. Source: John Mtembezi Inniss wa youtube.Umesahau 'FAHARI' kiboko cha majarida. Mtunzi alikuwa Freddy Jimm Mdoe.
nimefurahi kusikia ulikua ni mmoja kati ya waandishi katika majarida yale,labda nikuulize kitu kimoja;KWANINI MAJARIDA YALE YAMEPOTEA ILIHALI YALIKUA YANAPENDWA SNA
majarida ya sani,bongo nk yalianza kupoteza umaarufu baada ya kuanza kutoka vijarida vidogo vidogo ambavyo vikaja kupata umaarufu mkubwa sana.Sababu sani na bongo yalikuwa yakitoka mara 2 au moja kwa mwaka.Hivi vijarida vilikuwa vikitoka kila baada ya miezi miwili au mitatu.Watu wakapoteza mvuto na majarida hayo kwa kusubiri kwa muda mrefu.Kufa kwa gazeti la HEKO ni ugomvi uliotokea baina ya BEN na mwanasiasa maarufu nchini ambaye anaitwa waziri mkuu mstaafu siku hizi.Mtifuano huo ulipelekea BEN kukaa rumande kwa miezi 3,kwa tuhuma ya wizi wa computer.Alisumbuliwa sana kwa kesi ya uongo ambayo ikaanza kudhoofisha gazeti la HEKO ambalo lilikuwa linaelekea kuwa gazeti la kila siku badala ya wiki.Ni stori ya kusikitisha kwa ufupi ni hayo mkuu
lakini majarida ya sani na bongo yalkua yanatoka mara moja kila mwezi
hapo kwa wanawake wa
kuchorwa aisee kwenye majarida walikua wanazidisha,msichana utafikiri
hayupo dunian yan anakuwa wakipekeee ile mbaya