Godbless J Lema
Arusha MP
- Sep 28, 2013
- 92
- 2,205
Nimepata taarifa jana ya mlipuko wa Bomu uliotokea Arusha katika Bar ya Arusha Night Park , taarifa niliyoipokea inasema baadhi ya Watu wameumizwa vibaya sana lakini hata hivyo bahati nzuri mpaka sasa sijapokea taarifa ya Binadamu aliyepoteza maisha .
Maisha yanaendelea kuwa magumu katika fikra za Watu kwani milipuko kama hii ilianzia Kanisani halafu ikafuata katika Mkutano wa hadhara wa Chadema na sasa ni kwenye Bar za Pombe , sijui ni nini kinaendelea Arusha , lakini ni vyema muda wa kutafakari ukaongezewa nafasi . Kama Mbunge sina neno zaidi mpaka nitakapokuwa nimefika Arusha leo nakuona na kutafakari .
Poleni sana Familia zote zilizofikwa na majanga haya nawaombea kwa Mungu huku nikitambua mashaka makubwa ya Watu wote wa Arusha . Majaribu haya ni makubwa lakini kwa Dua na Sala mtashinda .