Majangili yakamatwa Serengeti

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
ZAIDI ya watu 170, wamekmatwa na kikosi dhidi ya ujangili kanda ya serengeti, kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya ujangili, pamoja na ya kuingia katika hifadhi ya taifa ya serengeti kinyume cha sheria.

Kamanda wa kikosi dhidi ya ujangili kanda ya serengeti, kilichoko mjini Bunda mkoani Mara, Hassan Nkusa, ameliambia gazeti hili juzi katika mahojiano maalum ofisini kwake, kuwa watu hao waliamatwa katika kipindi cha kuanzia juni 2007 hadi julai 2008.

Nkusa alisema kuwa watu hao wapatao 175, baadhi yao ni majangili waliokuwa wanaendesha uwindaji haramu katika hifadhi hiyo na kwamba walikuwa tayari wamekwishaua wanyama wa aina mbalimbali.

Alisema kuwa baadhi ya watu hao tayari wamekwisha fikishwa mahakamani na wengine walipigwa faini na kuachiwa huru, ambapo kiasi cha zaidi ya sh. milioni 1.5 zilipatikana.

Aidha, alisema kuwa katika kipindi hicho walifanikiwa kukamata nyara za serikali zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 41, 760. zikisafirishwa kwa ajili ya kwenda kuuzwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo na nchi jirani ya Kenya.

Alibainisha kuwa watu hao walikamatwa na silaha mbalimbal za jadi na za kivita, walizokuwa wakizitumia kwa ajili ya kuwindia wanyama, pamoja na nyaya za kutegea wanyama hao.

Alifafanua kuwa wanyama waliokutwa wakiwa tayari wameuawa na majangili hao ni pamoja na Nyumbu 74, Punda milia 29, Nyamela 11, Nyati 9. Pofu 5, Swala 4 na Swala Para 2.

Aliongeza kuwa pia kikosi chake kilifanikiwa kuokoa wanyama aina Nyumbu wapatao 14 Na Swala wapatao saba, waliokuwa wamenaswa na mitego ya wawindaji hao haramu, ambapo waliwafungulia na kurudishwa hifadhini.

Alisema kuwa katika kipindi hicho pia walifanikiwa kukamata jumla ya ng' ombe 13,938, zilizokuwa zinachungia ndani ya hifadhi hiyo, ambapo wamiriki wa ng' ombe hizo walipigwa faini na kuzikomboa

"Hata hivyo tunashukuru kuwa kwa sasa jamii imeanza kuelewa maana ya uhifadhi na ulinzi shirikishi, kwa kweli wanatoa ushirikiano wa kutosha...na sisi kazi yetu nikundelea kuwelimisha ili waweze kujua umuhimu wa kuhifadhi rasilimali zetu ambazo zinalipatia taifa fedha za kigeni na kuinua uchumi wetu"

Alisema kuwa kikosi chake kitazidi kupambana na majangili hao ili kutokomeza kabisa uwindaji haramu na akawataka wananchi kuzidi kutoa ushirikiano wa karibu kwa kuwapatia taarifa za siri zianazohusu wawindaji haramu.
 
Back
Top Bottom