Majanga ya King'amuzi hichi cha Startimes!

Rapherl

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Posts
3,504
Reaction score
2,256
WanaJF,

Nipo sehemu fulani mbali na Nyumbani kwangu kama wiki sasa,hapa nilipo muda mwingi natumia kupumzika hapa home nachat na kuangalia sana tv kupitia kingamuzi cha Startimes(ndo kilichopo).

Sasa nilichogundua baada ya siku kama tatu za kukaa hapa ni kwamba hichi king'amuzi kinachagua ni kitu gani cha kuonyesha na kipi hakionyeshi,

Kwa mf:StarTv ikianza habari kitakata kata weee wakiweka matangazo aaah fresh unaona vizuri kabisa wakirudi kwenye habari kinaanza tena kukata na kuna nyimbo ambazo mpaka nimeshakariri kwamba huu wimbo ukipigwa unakata kata hata ufanye nini haisaidii ila kwenye Channel nyingine wimbo huo huo utauona vizuri kabisa...ikianza BBC swahili itakata kata mpaka inaisha ikiisha tu inaonyesha vizuriiiii hata bila ya kurekebisha antenna...

Na hili la habari ni karibia Channel zote wakiwa wanatangaza studio inaonyesha kwa afadhali kidogo ila wakiungana na waandishi wao huko nje ni Majanga tena!

Ni hivyo hivyo pia kwa channel nyingine zote!

Nimemuuliza mwenye nacho kaniambia yeye kashazoe ndio hivyo hivyo kila siku hata kurekebisha kashachoka

Sasa mimi imebidi tu nikanunue CD nianze kuangalia kwasababu hakuna raha tena ya kuangalia hii tv

Sijui wadau kama na nyie mna-experience hili swala kama huyu ndugu yangu.
 
Subiria tu ununue cha mkombozi wetu! Mana aja! AZAM TV! Kipo vizury! Full rahaaaa! uploadfromtaptalk1375825407098.jpg
 
Umelipia hilo Tangazo lako?
 
mara nyingi ikiwa inakata kata au inanata haipati mawimbi vizuri. ulizia mnara wao wa kurushia matangazo upo direction gani uulekezee huko au mwite fundi dishi au wa startimes wakurekebishie
 
WanaJF,

Nipo sehemu fulani mbali na Nyumbani kwangu kama wiki sasa,hapa nilipo muda mwingi natumia kupumzika hapa home nachat na kuangalia sana tv kupitia kingamuzi cha Startimes(ndo kilichopo).

Sasa nilichogundua baada ya siku kama tatu za kukaa hapa ni kwamba hichi king'amuzi kinachagua ni kitu gani cha kuonyesha na kipi hakionyeshi,

Kwa mf:StarTv ikianza habari kitakata kata weee wakiweka matangazo aaah fresh unaona vizuri kabisa wakirudi kwenye habari kinaanza tena kukata na kuna nyimbo ambazo mpaka nimeshakariri kwamba huu wimbo ukipigwa unakata kata hata ufanye nini haisaidii ila kwenye Channel nyingine wimbo huo huo utauona vizuri kabisa...ikianza BBC swahili itakata kata mpaka inaisha ikiisha tu inaonyesha vizuriiiii hata bila ya kurekebisha antenna...

Na hili la habari ni karibia Channel zote wakiwa wanatangaza studio inaonyesha kwa afadhali kidogo ila wakiungana na waandishi wao huko nje ni Majanga tena!

Ni hivyo hivyo pia kwa channel nyingine zote!

Nimemuuliza mwenye nacho kaniambia yeye kashazoe ndio hivyo hivyo kila siku hata kurekebisha kashachoka

Sasa mimi imebidi tu nikanunue CD nianze kuangalia kwasababu hakuna raha tena ya kuangalia hii tv

Sijui wadau kama na nyie mna-experience hili swala kama huyu ndugu yangu.
 
haaahaaaa hata hiki cha kwangu ni kasheshe huwa kinachagua hadi muda wakuangali.kuna muda huwa hakioneshi kabisa!!!
 
Back
Top Bottom