Osaka
JF-Expert Member
- Jun 21, 2011
- 1,762
- 551
Salaam wana Jamvi!
Jana jioni majira ya saa 11, Ma Padri watatu wa kanisa katoliki walipata wakati mgumu baada kukuta kizuizi barabarani wakati wakirudi toka Sehemu ijulikanayo kama kata ya Kitunda (wilaya ya Sikonge) njia kuu kuelekea Mbeya ukitokea Tabora. Ma Padri hao walikwenda kitunda kwa ajili ya maandalizi ya ujio wa Askofu wa Jimbo kuu la Tabora (Paul Ruzoka). Baada ya kufika Utimule walikuta miti miwili mikubwa ikiwa imekatwa na kuangukia barabarani; muda ule ule majambazi takribani manane yalitokea yakiwa na SMG mbili na kuteka hao watumishi wa Mungu na kuchukua sadaka kiasi zaidi ya Tshs. Million moja na ushehe. Aidha magari mengine madogo mawili yalitekwa pamoja na lori moja na kuporwa mali kadhaa.
Source: askari polisi wa Sikonge.
Nilikuwa nikitokea Rukwa kulekea Mwanza Via Tbr. Nimekutana na polisi hao pale Ipole, njia panda ya kwenda Mbeya na Rukwa ukitokea Tabora. Inasemekana eneo hilo la Utimule liko karibu sana na sehemu yalipotokea maafa ya ' mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe'. Inasikitisha!