40 days 2022/2023 road trip adventure around Tanzania

JBourne59

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
941
8,547
40 Days 2022/2023 adventure around Tanzania main land.

1. Gari ipo, Land Rover Defender 110 / 2016 Station Wagon kama hiyo hapo chini ila rangi tofauti.

2. Wanao hitajika ni wadau watano (5), wanawake watatu (3) na wanaume wawili (2) na mimi mwenyewe jumla tuwe watu sita (6).

3. Wakijitokeza watu wengi zaidi utaratibu wa kupata (ma)gari (me)ngine utafanyika.

4. Tutatembea zaidi ya kilomita 6,000 kwa siku 32, siku 8 zitapotelea katikati kadri tutakavyo amua.

5. Makadirio ya gharama ya mafuta ni 1.8M hadi 2m.

6. Mchango kwa kila mdau itahitajika 1.5m ambayo itagharamia mafuta, chakula, malazi na utalii.

7. Mchango haukusanywi bali kila mmoja ajiwekee akiba benki au popote pale kuanzia sasa hadi mwezi October 2022 panapo majaaliwa ambapo tutafanya kikao na kupanga safari yetu, lengo liwe hadi kufikia 5 Disemba 2022 tuwe tumemaliza mzunguko wetu.

Mawazo chanya, yanakaribishwa, kuhusu Route, gharama, usahihi wa umbali, usalama, nk.

8. Mapendekezo yangu ya route iwe ni kuzunguka pembezoni mwa Tanzania kama ifuatavyo:-

Day 1
Dar - Lindi - Mtwara, almost 600km.

Day 2
Mtwara - Masasi - Mtambaswala, almost 320km.

Day 3
Mtambaswala - Masasi - Songea, almost 500km.

Day 4
Songea - Mbinga - Mbamba bay, almost 180km.

Day 5
Mbamba bay - Songea - Njombe, almost 420km.

Day 6
Njombe - Makete (via Kitulo) - Mbeya, almost 170km.

Day 7
Mbeya - Kasumulu, almost 120km.

Day 8
Kasumulu - Mbeya Tunduma, almost 230km

Day 9
Tunduma - Sumbawanga - Kasanga, almost 350km

Day 10
Kasanga - Sumbawanga - Muze - Lake Rukwa, almost 180k.

Day 11
Lake Rukwa - Muze - Namanyele - Kibaoni - Majimoto, almost 180km.

Day 12
Majimoto - Kibaoni - Stalike - Mpanda, almost 150km

Day 13
Mpanda - Uvinza - Kigoma town, almost 320km.

Day 14
Kigoma - Kasulu - Nyakanazi, almost 350km

Day 15
Nyakanazi - Lusahunga - Nyakahura - Kobero border, almost 150km.

Day 16
Kobero border - Nyamiyaga - Rusumo border, almost 70km.

Day 17
Rusuma - Nyakasanza - Mtukula, almost 250km.

Day 18
Mtukula - Bukoba town, almost 90km.

Day 19
Bukoba - Biharamuro - Geita - Mwanza, almost 450km.

Day 20
Mwanza - Bunda - Musoma - Migori, almost 300km.

Day 21, 22, 23, 24
Migori - Tarime - Serengeti, almost 200km + other 200km.

Day 25, 26
Serengeti - Ngorongoro, almost 70km + 200km.

Day 27, 28
Ngorongoro - Karatu - Arusha, almost 200km.

Day 29
Arusha - Segera - Tanga - Horohoro, almost 550km

Day 30
Horohoro - Tanga town, almost 70km + 50km.

Day 31
Tanga - Pangani - Sadani, almost 200km.

Day 32
Sadani - Bagamoyo - Dar es Salaam, almost 180k.

Karibuni kwa mawazo chanya.

___________


Updated

(a) Safari zitagawanywa kwa “5days to 8days trip” kwa kuzingatia "route" yenyewe.

(b) Idadi ya wadau watakao jitokeza itaamua gari gani na gari ngapi zitumike.

(c) Wenye gari binafsi wanakaribishwa kwenye msafara, wakipenda kuchukuwa baadhi ya wadau kwa kuchangia mafuta pia itaruhusiwa, gari ziwe zenye uwezo wa kupita njia zenye changamoto (rough roads, mud roads, sandy roads) – itazingatiwa kwenye route husika.

(d) Familia zinaruhusia kushiriki, ili mradi kila mshiriki awe ametimiza miaka 18 na kuendelea

(e) Panapo majaaliwa tarehe 15 Feb 2022 tutaanza kujiorodhesha kwa wale walioazimia kisha kupanga bajeti kwa kila route itakavyo kubaliwa.

(f) Matarajio ya safari ni July 2022 au Nov 2022 kadri wadau watakavyo amua wenyewe.

(g) Makadirio ya kilomita yamezingatia pia "idling time", mizunguko ya mchepuko, na michepuko ya kitalii, Lakini kama kuna sehemu kilomita zimekosewa sana turekebishe kwa maana ndizo zitakazo tuongoza kwenye bajeti ya mafuta.

(h) Katika mapendekezo ya "route' inawezekana kukawa na route muhimu imesahaulika, basi TUPENDEKEZE, Mapendekezo ya awali ya mgawanyo wa "route" ni kama ifuatavyo:-

1st route.
Dar – Lindi – Mtwara (day 1 = 600km)

Mtwara – Masasi – Mtambaswala – Masasi (day 2 = 450km)

Masasi – Songea (day 3 = 400km)
Songea – Mbinga – Mbamba bay (day 4 = 180km)

Mbamba bay – Songea – Makambako (day 5 = 500km)

Makambako – Iringa – Morogoro – Dar (day 6 = 650km)

{Makadirio jumla ni kilomita 2,800}

2nd route.
Dar – Makambako –Tunduma (day 1 = 950km)

Tunduma – Ileje – Kasumulu (day 2 = 250km)

Kasumulu – Tukuyu – Makete (day 2 & day 3 = 170km + 50km)

Makete – Njombe - Iringa – Dar (day 4 = 830km)

{Makadirio jumla ni kilomita 2,250}

3rd route.
Dar – Mikumi (day 1 = 300km + 100km)

Mikumi – Mbeya (day 2 = 550km)

Mbeya – Tunduma – Sumbawanga (day 3 = 350km)

Sumbawanga – Kasanga – Namanyele – Kibaoni – Majimoto (day 4 = 350km)

Majimoto – Lake Rukwa – Muze – Sumbawanga (day 5 = 160km)

Sumbawanga – Mbeya – Morogoro (day 6 = 960km)

Morogoro – Dar (day 7 = 200km)

{Makadirio jumla ni kilomita 3,000}

4th route.
Dar – Dodoma – Manyoni – Itigi – Tabora (day 1 = 850km)

Tabora – Sikonge – Ipole – Makongolosi – Chunya (day 2 = 550km)

Chunya – Mbeya – Mlowo (day 3 = 140km)

Mlowo – Mtowisa –Muze (day 4 = 280km)

Muze – Ntendo – Chala – Mashete – Kisi – Mpanda (day 5 = 300km)

Mpanda – Inyonga – Ipole – Tabora (day 6 = 300km)

Tabora – Nzega – Singida – Dodoma (day 7 = 580km)

Dodoma – Dar (day 8 = 450km

{Makadirio jumla ni kilomita 3,200}

5th route.
Dar – Dodoma – Iringa (day 1 = 750km)

Iringa – Mbeya – Chunya (day 2 = 420km)

Chunya – Rungwa – Itigi (day 3 = 450km)

Itigi – Tabora – Ipole – Inyonga – Mpanda (day 4 = 450km)

Mpanda – Uvinza – Kigoma town (day 5 = 320km)

Kigoma – Tabora – Itigi – Manyoni (day 6 = 700km)

Manyoni – Dodoma – Dar (day 7 = 600km)

{Makadirio jumla ni kilomita 3,700}

6th route.
Dar – Singida (day 1 = 700km)

Singida – Kahama (day 2 = 300km)

Kahama – Nyakanazi – Kibondo – Kasulu – Kigoma (day 3 = 550km)

Kigoma – Kobero border – Rusumo border (day 4 = 520km)

Rusumo – Singida (day 5 = 600km)

Singida – Babati – Kondoa – Dodoma (day 6 = 240km)

Dodoma – Dar (day 7 = 450km)

{Makadirio jumla ni kilomita 3,400}

7th route.
Dar – Sadani (day 1 = 180km + 50km)

Sadani – Pangani – Tanga (day 2 = 200km )

Tanga – Horohoro – Tanga –Korogwe (day 3 = 250km)

Korogwe – Arusha – Karatu (day 4 = 490km)

Karatu – Ngorongoro – Karatu - Arusha (day 5, day 6 = 340km)

Arusha – Segera – Msata – Bagamoyo – Dar (day 7 = 650km)

{Makadirio jumla ni kilomita 2,200}

8th route.
Dar – Kahama (day 1 = 900km)

Kahama – Bukoba – Mtukula (day 2 = 480km)

Mtukula - Bukoba – Biharamula – Geita – Mwanza (day 3 = 510km )

Mwanza – Musoma – Sirari (day 4 = 300km )

Sirari - Tarime – Serengeti (day 5, day 6 = 120km + 100km)

Serengeti – Karatu – Arusha (day 7 = 400km)

Arusha – Chalinze – Dar (day 8 = 650km)
{Makadirio jumla ni kilomita 3,500}

#Tuhakiki umbali (kilomita)
#Tuanishe route muhimu zilizo sahaulika
#Tupeane maangalizo ama mambo ya kuzingatia kwa ajili ya usalama
#Mengineyo

Karibuni.

___________
JBourne59
 
Budget ndefu sana mzee. Ila sio mbaya kwa alie tayari kukaa nje ya comfort zone kwa mwezi mzima.

Ila hapo kwenye gari una maanisha gari gani exactly?

Defender 110 haipo ya mwaka 2021. Defender 110 ilitengezwa mwisho 1990.

90A5D8E9-B767-44B3-805A-AF237DF24760.jpeg


Ya sasa 2020/21 inaitwa tu Defender usiweke 110 mbele. Model ni L663 kama sijakosea.
2A02F0C0-51E5-4DFE-89F4-8551815821D7.jpeg


Kama ni ilo gari la hapo chini, aisee mtainjoi sana.

Ushahuri:

Kwa hizo siku kwanini msiingie hadi nchi za jirani mfano Nairobi au Kusini?
 
Siku 40 mbona nyingi sana?? Labda kwa mtu asiyekuwa na majukumu ndani ya hizo siku zote 40.
Ni kweli ndio maana mawazo chanya yanakaribishwa kuboresha.

Route ni kwa ajili ya mwaka 2022/2023

Hata kuzikata pia inawezekana ili kuendana na mayakwa ya wadau kwa maana tunaweza kugawa route kwa vipande vipande,

Haya, karibu tuboreshe sasa.
 
Budget ndefu sana mzee. Ila sio mbaya kwa alie tayari kukaa nje ya comfort zone kwa mwezi mzima.

Ila hapo kwenye gari una maanisha gari gani exactly?

Defender 110 haipo ya mwaka 2021. Defender 110 ilitengezwa mwisho 1990.

View attachment 2051469

Ya sasa 2020/21 inaitwa tu Defender usiweke 110 mbele. Model ni L663 kama sijakosea.
View attachment 2051465

Kama ni ilo gari la hapo chini, aisee mtainjoi sana.

Ushahuri:

Kwa hizo siku kwanini msiingie hadi nchi za jirani mfano Nairobi au Kusini?
Gari siyo yangu ila ya jamaa yangu ambaye hana shida nami, nimemuumiza amesema ni Defender ya 2016, startech sixty eight.

Siyo lazima iwe siku 40 mfululizo

Na kuhusu bajeti siyo kihivyo kama ukianza kuchanga kuanzia Jan

Kila mtu atatumia hela zake, bajeti iliyotajwa na makadirio tu hiyo labda kwenye kuchangia mafuta ambapo napo tutachanga kila tunapojaza full tank labda au kadri wadau watakavyo amua
 
Budget ndefu sana mzee. Ila sio mbaya kwa alie tayari kukaa nje ya comfort zone kwa mwezi mzima.

Ila hapo kwenye gari una maanisha gari gani exactly?

Defender 110 haipo ya mwaka 2021. Defender 110 ilitengezwa mwisho 1990.

View attachment 2051469

Ya sasa 2020/21 inaitwa tu Defender usiweke 110 mbele. Model ni L663 kama sijakosea.
View attachment 2051465

Kama ni ilo gari la hapo chini, aisee mtainjoi sana.

Ushahuri:

Kwa hizo siku kwanini msiingie hadi nchi za jirani mfano Nairobi au Kusini?
Lengo la kuizunguka Tz ili wadau wapate kuijua Tz yao, angalau kwa kuanzia, kisha trip nyingine tuvuke mipaka
 
Mkuu wazo zuri sana, naliunga mkono kwa 100%
Maboresho:
1. Kama budget inaruhusu namanga ikunje kwenda nairobi-mombasa-Tanga
Japo hapo maana halisi ya kuizunguka Tanzania itapotea kidogo kwa mkoa wa kilimanjaro
2. Kama ni mapumziko/likizo siku 40 zijumuishe utalii wa ndani hasa kwa mikoa ya njombe, mara, Arusha na kilimanjaro.

Project imekuja wakati mbaya, natengeneza road trip ya SADC (solo adventure) kwa mwezi December, 2022 to January, 2023
Japo kwangu naiona ni trip makini sana isiyo ya kuikosa

Hongera sana kwa wazo
 
Mkuu wazo zuri sana, naliunga mkono kwa 100%
Maboresho:
1. Kama budget inaruhusu namanga ikunje kwenda nairobi-mombasa-Tanga
Japo hapo maana halisi ya kuizunguka Tanzania itapotea kidogo kwa mkoa wa kilimanjaro
2. Kama ni mapumziko/likizo siku 40 zijumuishe utalii wa ndani hasa kwa mikoa ya njombe, mara, Arusha na kilimanjaro.

Project imekuja wakati mbaya, natengeneza road trip ya SADC (solo adventure) kwa mwezi December, 2022 to January, 2023
Japo kwangu naiona ni trip makini sana isiyo ya kuikosa

Hongera sana kwa wazo
Kadri itakavyo pokelewa tutapanga muda sisi wenyewe lini tuanze trip, na tuimege vipi hata ikibidi iwe ya SEVEN DAYS sawa tu, lakini tuta cover eneo dogo la nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom