Majambazi wavamia baa Kimara na kupora pesa

Majambazi wavamia baa Kimara na kupora pesa

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,849
Reaction score
29,569
Wakuu muda mfupi uliopita nimepata taarifa kutoka kwa mtu wangu wa karibu aliyepo maeneo ya Kimara kwamba majambazi wamevamia bar Kimara, inasemekana wameanzia Kona, Korogwe na Kawacha bar zote zikiwa ni bar na kumimina risasi.

Sijapata taarifa za watu kupoteza maisha ila inasemekana kote walipopita wamepora fedha.

Taarifa zaidi zinakuja!

Jana ilikuwa tabu ndugu.Nilikuwa mbele kidogo ya Kez Pub kuna grossary zimepangana.Nikasikia milio ya risasi kumbe ilikuwa Latemba, kukatulia.

Wakawasha bodaboda haooo Korogwe kwa Kawacha hapo ndio risasi kibao.Ila walikuwa wanapiga hewani hawajaua mtu.

Pia nasikia endapo wapo kundi na mmoja wao akiua.Basi hela zote wanampatia aliyeua maana damu itawatafuna.

Ila wasipoua nasikia inakuwa dili zuri.
 
mnaokwenda katika mabar angalieni sana asee
 
Yaani we acha tu, leo saa kumi nilitoka na gari kwa kumuambia wife nakwenda kujaza mafuta kesho nisihangaike, ukweli nilikua na kiu ya guiness tatu au nne. Kufika petrol station mdogo wangu aliye dandia safari yangu aliniomba hela kidogo, nikamwambia sina, ilibidi niache kwenda bar nirudi nyumbani. Ubahili umeniokoa. Safari yangu ilikua ni Latemba bar au Mkulima pale Kona.
 
Makubwa kama wanavamia vituo vya police watashindwa kuvamia baa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
walioko latemba bar,mkulima bar na Kez pub mtujuze jameni
 
Huku Kimara Mbezi kuna bar za kuepuka sana.

Hizi ni kama, Kilimani Temboni, Nsala Inn kwa Yusufu, Kwa Mtitu, Kwa Mushi, Resort na Alasta Vista kwa Msuguri. Geografia ya hivi bar ni kwamba wakija na silaha moja tu hatoki mtu, kibaya zaidi ni kwamba matajiri wote au wenye hela za wizi hupendelea sana Kilimani Temboni na Resort kwenye Kitimoto.

Mapopo bado mko bar
 
Hard cores wote wanakaa kimara kwahiyo sishangai kusikia njugu zimemiminwa huko....
 
Khaa!! Ndiyo mkome. Jifunzeni kunywea majumbani bana. Stim ni ileile tu na tena unakuwa salama sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom