Majambazi wavamia baa Kimara na kupora pesa

Majambazi wavamia baa Kimara na kupora pesa

Yaani we acha tu, leo saa kumi nilitoka na gari kwa kumuambia wife nakwenda kujaza mafuta kesho nisihangaike, ukweli nilikua na kiu ya guiness tatu au nne. Kufika petrol station mdogo wangu aliye dandia safari yangu aliniomba hela kidogo, nikamwambia sina, ilibidi niache kwenda bar nirudi nyumbani. Ubahili umeniokoa. Safari yangu ilikua ni Latemba bar au Mkulima pale Kona.

Mkulima ipo Sehemu gani? Ni pale Kez Pub?
 
Huku Kimara Mbezi kuna bar za kuepuka sana. Hizi ni kama, Kilimani Temboni, Nsala Inn kwa Yusufu, Kwa Mtitu, Kwa Mushi, Resort na Alasta Vista kwa Msuguri. Geografia ya hivi bar ni kwamba wakija na silaha moja tu hatoki mtu, kibaya zaidi ni kwamba matajiri wote au wenye hela za wizi hupendelea sana Kilimani Temboni na Resort kwenye ktmt.

Mapopo bado mko bar

Vipi na kule New Mbezi Rest kuna shida? Au kule hakuna matukio
 
Ngoja wafumliwe wale walevi wanaokunywa na kutaka shari!
 
Khaa!! Ndiyo mkome. Jifunzeni kunywea majumbani bana. Stim ni ileile tu na tena unakuwa salama sana
Nyumbani ??? wife yupo au hayupo ? halafu ukipepesa macho utakua unaangalia nini ? TV ? Bar kuna mengi, kuanzia kongoro, mabinti wakipita pita na kuonyesha mapaja, kamziki kwa mbali ? wewe unafikiri kwa nini m barmaid wanavaa kihasarahasara ? Nyumbani utawaona. Mheshimiwa futa kauli yako isije ikaingizwa kwenye hansard.
 
Jana ilikuwa tabu ndugu.Nilikuwa mbele kidogo ya Kez Pub kuna grossary zimepangana.Nikasikia milio ya risasi kumbe ilikuwa Latemba, kukatulia.

Wakawasha bodaboda haooo Korogwe kwa Kawacha hapo ndio risasi kibao.Ila walikuwa wanapiga hewani hawajaua mtu.

Pia nasikia endapo wapo kundi na mmoja wao akiua.Basi hela zote wanampatia aliyeua maana damu itawatafuna.

Ila wasipoua nasikia inakuwa dili zuri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom