Majambazi wavamia na kupora pesa CRDB na DCB Bank Chanika

fab280391

Senior Member
Jul 29, 2015
122
31
Leo eneo La Chanika, Dar es salaam mida ya saa 9 jioni majambazi wapatao zaidi ya 8 wavamia na kuziteka Bank mbili zilizo eneo moja kwa muda wa dakika 45. CRDB ambayo hata haijaanza kufanya kazi rasmi na DCB Bank..

Majambazi walikuwa na Pikipiki 4 aina ya boxer, gari tinted na Silaha za kivita wamefanikiwa kuchukua pesa nyingi, kuua walinzi 2 wa Suma JKT na kujeruhi wafanyakazi wengine..

Polisi wamefika dakika 15 baada ya majambazi kuondoka ijapokuwa kituo kidogo cha Polisi kipo karibu ni kama umbali wa dakika 10 kwa miguu kutoka Bank.

=================

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Ulrich Matei, ameithibitishia JamiiForums kutokea kwa tukio hilo na kwamba majambazi hao wanasadikiwa kuwa walikuwa kati ya 6 hadi 8.

Amesema wahalifu hao walianza kuingia kwenye Benki ya DCB na kupora fedha zilizokuwa kaunta na muda mchache baada ya hapo walivamia Benki ya CRDB na kupora fedha ambazo hadi sasa haijajulikana thamani yake.

Aidha, amesema majambazi hao waliwaua askari wawili wa Suma JKT, waliotambuliwa kwa majina ya Ramadhani Halidi na Shane Rajabu.

"Tumeanza upelelezi ikiwemo kuelekea katika maeneo ya Mkuranga ambapo ndiko tunakoamini kwamba hawa wahalifu wameelekea, tutakapowakamata tutawapa taarifa kamili" alikaririwa na JamiiForums.

attachment.php

 

Attachments

  • IG.JPG
    IG.JPG
    17.8 KB · Views: 12,568
Yamevamia CRDB microfinance na DCB huko chanika na kuua askari wawili Wa SUMA JKT, kisha yakapora kiasi kikubwa cha fedha (idadi bado haijajulikana) na pia yamepora bunduki aina ya shotgun moja na kutokomea kusiko julikana . Kazi imeanza..
 

Attachments

  • IMG-20151208-WA0027.jpg
    IMG-20151208-WA0027.jpg
    76.6 KB · Views: 4,195
Mmmh ila ninavyojua vituo vidogo havina silaha mtoa taarifa kwenye bank hizo hapakuwa na askari wa ffu kama zilivyo bank zingine
 
Mpaka kesho jioni Kova atakuwa tiyari kishaleta shortgun nyingine na mapanga ka 6 hivi kuwa wananchi msiogope tumeshakamata hiyo silaha.
Yawezekanaje majambazi yatingishe sehemu kwa dk 45 halafu waondoke ndio polisi mnaingia 15 dk baadaye? Nasikia harufu flan hapo. Sii bure
Wazirudishe tu fedha zetu na kuwalipa hao wafiwa. Staki kuamini
 
Duuu...hapa kazi tu inatumika vibaya. Hizo benki kwakeli
pale mahala zilipo hakuna kituo cha polisi karibu.

Ila mimi narusha zigo la lawama kwa benki hizi kuweka maisha
ya walinzi na pesa katika mazingira hatarishi ,wewe unaweka
SUMA JKT aliye na kirungu tu unategemea atahimili vishindo
vya wazee wa kazi wakija wako nondo.??

Kwanini benki zote zisilindwe na FFU au hata wanajeshi...? kwani
mishahara ya kuwalipa watu hao ni shiling ngapi ..? Mbona mameneja
na wafanyakazi wa taasisi za kifedha wanalipwa vizuri ila waliopewa
dhamana ya ulinzi wamewekwa rehani...? Kwani kwa mwaka kwenye
yale mabilioni mnayotusomeaga kuwa mmepata faida baada ya kufunga hesabu
zenu hayawezi kulipa ulinzi madhubuti...?

R.I.P mwera wa SUMA JKT.
 
Afadhali wameiba sasa ili Raisi aangalie eneo hilo atumbue majipu Polisi wanaokula na majambazi.
 
Afadhali wameiba sasa ili Raisi aangalie eneo hilo atumbue majipu Polisi wanaokula na majambazi.

Tusilaumu polisi kwa kila jambo baya, kwani hayo makampuni
yanashindwa kuajili au kuingia mikataba na vyombo vya ulinzi
na usalama kama Polisi au wanajeshi sio hao "militia " wa SUMA JKT.
 
Afadhali wameiba sasa ili Raisi aangalie eneo hilo atumbue majipu Polisi wanaokula na majambazi.

Niambie Umeghafilika kwa hili..... otherwise we unaona ni vyema watu kupoteza maisha yao ili jipu litumbuke kweliiii ???
 
Yamevamia CRDB microfinance na DCB huko chanika na kuua askari wawili Wa SUMA JKT, kisha yakapora kiasi kikubwa cha fedha (idadi bado haijajulikana) na pia yamepora bunduki aina ya shotgun moja na kutokomea kusiko julikana . Kazi imeanza..

R.I.P mwera , ila hizi picha za wafu sio nzuri
mnawaumiza mioyo wapendwa wao.
 
Sasa kulikuwa na haja gani kuwaua hao jamaa kama wana virungu! Wawe wastaarabu hawa watu, hela tutawapa!
 
silaumu vituo vidogo vya police saana unakuta jambazi kaja na silaha ambazo hamna hapo kituoni utakimbilia huko ukatolewe utumbo huku unajua kabisaaa. chakufanya serikali iongeze silaha vituo vidogo vya police
 
Tusilaumu polisi kwa kila jambo baya, kwani hayo makampuni
yanashindwa kuajili au kuingia mikataba na vyombo vya ulinzi
na usalama kama Polisi au wanajeshi sio hao "militia " wa SUMA JKT.

Hilo sio suluhisho mkubwa. Hata wangekuwepo JWTZ wawili majambazi wakija idadi kubwa (kama hiyo ya jambazi wanane8) watazidiwa nguvu tu. Suluhisho ni jeshi la polisi imara litakalo tokomeza huu mtandao wa ujambazi kuanzia mitaani mpaka vichochoroni. Bahati nzuri baadhi ya mitandao iliokomaa wanaijua vizuri na kuna taarifa baadhi ya maaskari wanakula nao.
 
Tuwe wastarabu katika kurusha picha,,mabenk yetu wakati mwingine waangalie location inakuwaje watu wanakaa 45 mnts?
 
Hawa majambazi nadhani ni wale wale waliovamia Mbagala rangi tatu wiki iliyopita,dereva wetu wa dala dala nusura amgonge mmojawapo akamkwepa kwa kumuogopa mwingine pembeni alikuwa amesimama na chekeche yaani smg.
 
Back
Top Bottom