Majambazi waua Polisi wawili kituoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi waua Polisi wawili kituoni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by fangfangjt, Mar 17, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Majambazi waua Polisi wawili kituoni

  Shija Felician, Kahama
  MAJAMBAZI 10 waliokuwa wanashikiliwa katika kituo kidogo cha Polisi cha Kagongwa, wilayani hapa, wamewaua polisi wawili wa kituo hicho kwa risasi na kisha kutoroka.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi wakati majambazi hao walipokuwa kwenye chumba cha mahabusu kituoni hapo.

  Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi, Justus Kamugisha alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:45 usiku baada ya majambazi hao waliokuwa wakituhumiwa kwa makosa
  ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha, kumwita mmoja wa askari hao ndani ya mahabusu.

  Kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha, majambazi hao walimwita askari F5344, PC Salumu Mwanakatwe wakisema kuwa wana shida."Alipofungua mlango wa chumba cha mahabusu walimvuta ndani na kumfunika sweta kichwani kisha kumnyang'anya silaha aliyokuwa nayo aina ya SMG namba 14303612 na kuitumia kumuua," alisema.

  Kamanda Kamugisha alisema, baada ya kusikia mlio wa bunduki, askari mwingine mwenye namba F 4964, PC Ngwegwe Dira alikwenda kutoa msaada."Kabla hajafika alipigwa risasi kifuani na kufariki dunia hapohapo na majambazi hao walichukua bastola aina ya Chinese yenye namba XR 7526 aliyokuwa nayo askari huyo na kutokomea nayo," alisema.

  Baada ya mauaji hayo, majambazi hayo walitoroka na kati yao wawili ambao walikuwa wamefungwa pingu pamoja, waliikata kwa risasi na kukimbia na bastola lakini mmoja alishindwa kukimbia.

  "Jambazi huyo (aliyeshindwa kukimbia) aliyekuwa anajulikana kwa jina la Audax Bubel akakamatwa na wananchi na kupigwa shoka kichwani lililomwua hapohapo," alisema na kuongeza: "Majambazi tisa waliobaki, walitoroka na bunduki mbili." Kamanda Kamugisha alisema majambazi hao walikuwa wamekamatwa wakihusishwa na matukio mbalimbali ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha katika Mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Tabora na walikuwa wamewekwa mahabusu kwa lengo la kufanyiwa utambuzi.

  Kamugisha alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ambalo linaendeleza msako wa majambazi hayo.
   
 2. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  RIP Afande PC Ngwegwe Dira na PC Salum Mwanakatwe. Ama kweli majambazi yameshika hatamu Tanzania! Hao ni wanajeshi waliotemwa na au uzao wa JKT Kujitolea ambao hawana kazi na wanaona kina Rostam wanatanua tu, wakaamua kutumia sheria za misituni ili nao waishi. Lakini kumuua mwanausalama tena, du! Lazima washikwe hawana adabu.
   
 3. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,078
  Likes Received: 858
  Trophy Points: 280
  makamanda wetu wa polisi utafikiri wale wa kwenye picha za kihindi za miaka ya tisini. inakuwaje watuhumiwa wa mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha unawaweka kwenye kituo kidogo cha polisi. asa cheki picha waliyowafanyia askari! mbaya zaidi wlikuwa wakijulikana kuwa ni watu hatari.
   
 4. s

  salisalum JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Lo inatisha. Kukata tamaa ya maisha huko. Hawa jamaa siyo binadamu wa kawaida. Kinachoumiza zaidi ni hizi familia za askari, sijui serikali safari hii itawajali!
   
 5. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  uzembe
   
 6. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,897
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  I think kuna uzembe mkubwa sana wa askari....uzembe. to much questions ambapo hazina majibu
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  habari za kiinterejensia hazikuwaonesha kuwa hayo majambazi hayafai kuwekwa kituo cha vifaranga?
   
 8. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huu ni uzembe wa hali ya juu. Unaitwa kwenye maabusu ya majambazi unajipeleka kichwa kichwa. inaelekea askari hawa hawajaiva vya kutosha. Askari sio gwanda ila ni pamoja na ujanja wa kufikiri kwa haraka na kuchukua hatua staili. pole kwa waliofiwa na askari hao
   
 9. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  -kwanini uingie ndani ya chumba cha majambazi na silaha?
  -baada ya kuingia na silaha kwenye chumba cha majambazi, wakianza kufanya fujo utapiga risasi wote na kuwaua?
  -hivi vyumba vya mahabusu hua ni vidogo sana, ukiingia na silaha , wakakurukia huwezi kujilinda , kwanini hasinge acha silaha nje na kumuomba mwenzake amlinde wakati ana toa msaada kwa hawa wahalifu?

  -hapa mimi naamini ni mafunzo mabovu kwa asjari wetu, ndio maana hata kwenye maandamano hua wanatumia akili kidogo na nguvu nyingi. polisi ni sehemu ya jamii, lazima wapewe mafunzo na vifaa vya kufanyia kazi zao lasivyo wataumizwa tu.
   
 10. J

  JENSENE Member

  #10
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunawapa pole familia za askari hawa waliouawa.
  Tanzania mauaji haya hayatakwisha bali kuongezeka kutokana na viongozi wazembe kama Kamugisha. Kama kweli umetambua wazi kuwa watu hawa ni hatari katika jamii kwanini uwahifadhi katika kituo kisichokuwa na usalama wa kutosha? Huu ni UZEMBE WA KUTISHA.
  Askari wetu pia kueni makini someni alama za nyakati msikurupuke tu kabla ya kufikiri kwa kina.


  "Aliyeuwa kwa upanga naye pia atauawa kwa upanga"
   
 11. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hapo kituoni kulikuwa na askari wangapi? Na ni askari yupi aliyetoa hii stori. Inaelekea Mkuu wa Kituo kawatoa kafara hao wenzake. Inawezekanaje kituoni kuwa na askari wawili tu? Maana stori yote ni kama ya kutunga ingawa kweli askari wawili wameuwawa. Hebu huyo mkuu wao atueleze kinaga ubaga kulikuwa na askari wangapi mpaka hayo majambazi yakawazidi nguvu. Maana stori imeanzia katikati.
   
 12. charger

  charger JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,324
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  R.I.P askari wetu lakini hii pia iwe changamoto kwa jeshi letu namna gani wana handle hao wahalifu.
   
 13. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160

  Nilipoisoma hii habari haikuingia akilini kirahisi. Haiwezekani wateka nyara, wauwaji uwaweke kwenye kituo kidogo cha polisi na polisi wawili tu. Jamani, hivi tukisema ilikuwa njama ya kuwatorosha hao majambazi tutakuwa tunakosea? Mungu nisamehe kwa hili, lakini watu kama hawa ni hatari kuwekwa sehemu ambayo haina ulinzi madhubuti, wao kutoa roho ya mtu ni sawa na kumfinya Mbu.
  RIP in peace maafande wetu.
   
 14. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Sasa hao wameua maaskari sasa wako mitaani sijui kama patatosha!
   
 15. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  na majambazi ya namna hii , kwa hali waliojiweka sasa ni vigumu sana kukubali kukamatwa wakiwa hai, watapambana mpaka kufa
   
 16. N

  Ntandalilo Member

  #16
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Its Scarry....................!!!
   
 17. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Poleni Mliopoteza ndugu,

  ila tukio lina maswali mengi! ni fundisho kwa makamanda wa polisi kufanya kazi kwa umakini, busara na uadilifu na sio kwa mazoea.
   
 18. NAHUJA

  NAHUJA JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,054
  Likes Received: 15,648
  Trophy Points: 280
  Maskini askari hao wapumzike kwa amani raha ya milele uwape ee bwana na mwanga wa milele uwaangazie wapumzike kwa amani. Amina
   
 19. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,636
  Likes Received: 1,418
  Trophy Points: 280
  duuuh kama muvi vile,
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  Mar 17, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  R.I.P. Maaskali wetu ,na Poleni wafiwa,Hii habari inakufanya mtu ufikirie kwa undani zaidi ni kwa kiwango gani askari wetu wako salama wanapokuwa kazini,na inatia mashaka habari yenyewe inaonyesha jinsi linavyoendesha operation zake za ulinzi kwa askari wake haziko sahihi kabisa,wanaweka askari katika mazingira hatarishi sana kama jeshi haliwekezi katika miundo mbinu na vifaa kama redio calls na magari inawezekana kabisa hicho kituo hakina gari,kwa mana hiyo wakashindwa kuwasafirisha majambazi kuwapeleka kituo chenye ulinzi zaidi.
  Kama IGP Mwema amemdharirisha OCD wa Maswa aliyekatwa mtama mbele ya askari wadogo, ni vipi tutashindwa kuamini kwamba hayo Majambazi yameruhusiwa kufanya waliofanya kwa amri ya OCD au RPC maswali ni mengi zaidi ya majibu
   
Loading...