Majambazi wakamatwa baada ya kupora fedha Sinza Dar

Majambazi wakamatwa baada ya kupora fedha Sinza Dar

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia benki ya NMB ya iliyopo Sinza - Mori (Big Bon) na kupiga risasi za ovyo hewani, wakafanikiwa kutoka na mfuko wa hela (kiasi cha fedha hakijafahamika).

Wakati wanakimbilia kwenye gari lao Toyota Harrier lililokuwa kwenye Parking, wakakamatwa palepale!

======== Updates ========
Update: Majambazi walikuwa wanamlaghai mzee mmoja hivi ambaye alikutwa eneo tofauti na hapo Bigbon waliponaswa walihitaji hela.....ndio akawapeleka hadi bank kuwazuga ili akutane na Polisi.

Sio kuwa walitoka na mfuko wa hela, ila sasa wanashikiliwa na Polisi pia wapo katika Kituo cha Polisi Mabatini.


attachment.php

 

Attachments

  • Mori.jpg
    Mori.jpg
    46 KB · Views: 29,533
  • Leo.jpg
    Leo.jpg
    46.9 KB · Views: 30,445
Nilikuwepo eneo la tukio sema wazee wa kazi hawa wazembe
 
Safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Nawapongeza sana wahusika walifanikisha kukamatwa hao jamaa.

Huu mtandao wao siku hizi unapukutishwa kama njugu,wakachezee paka wa kwenye pumbu hadi wakome.
Watataja wenzao woooote.
Maana siku hizi kila mzembe akipata silaha tu basi anaona hiyo ndio kazi.Hapo jela maishaaaaa.
Yaani maisha ya mkato mwisho wake umekaa kimkatomkato namna hii.Segereaaaaaaaaa

Yaani hapo wanaona bora wangezaliwa Ombaomba kuliko kwenda jela.shenzzz type.
Kula chako cha halali ili upate baraka za mungu hapa duniani na maisha ya pili ya milele.
 
Daah!;Hawana mafunzo ya ku-escape hawo!,siumeona huyo aliyevalia kaunda suti!.
 
Hawa wezi nadhani mahesabu yao hayakwenda Sawa. Bora wamekamatwa.
 
Jamaa wameukabia ile mbaya.

Huyu mmoja unaweza kufikiria Mdogo wake Dangote alivyokaa kibosi kumbe JAMBANOKA.

Hapo walipo akili inaongea na kwenda mbali sana,wanatamani hata wangezaliwa Paka wa manzese kuliko kimechowakuta.
Mshahara wa Dhambi ni mauti.

Jamani maisha ya mkato haya yanajaza watoto wa mitaani na ni laana kwa mungu.Leo hii hao wote wanaacha wake zao ndio wanahangaika na watoto na familia zao na wengine hadi mama zao wazazi walikuwa wanawategemea.
Maana hapo wamepona miaka 40 jela,sasa si kifungo cha maisha?maana jinai imo ndani humohumo

Bora kuchomwa na jua ikifka jioni kula dagaa lako na wanao,mpe mungu nafasi yake,akikunyima hapa duniani ana hekma zake kwenye maisha ya milele yasiyo na tajiri wala Maskini.
 
Ushauri kwa Jeshi la Polisi.
Kuwakamata isiwe hoja ya kuishia uchunguzi kwao.

Pesa lazima zinakuwa zinajulikana zilipo na informers.Sasa waangalie kama kuna Bankers yoyote amehusika na mchongo huo.
Hawa jamaa siku hizi wamekuwa hawafanyi kazi hizi peke yao.
Ni Ushauri tu
 
Nilikuwepo eneo la tukio sema wazee wa kazi hawa wazembe
Oooh nilisahau picha,ngoja nipakie mara moja msijali.Ila picha za maiti siweki ng'ooo hii sheria ya makosa ya mtandao isije ikaanza na mimi.
Du Chachu ww kiboko yaani Ngara ulikuwepo na leo dah basi ni mtu wa mitandao unaruka haswa
Hebu niambie huyo jamaa aliyechuchumaa ambaye amevaa nguo (magwanda) ya Chama fulani alijiteteaje? bado anadai Tanzania ni Nchi mbaya kwa kumchelewesha kiberiti?

attachment.php
 
Back
Top Bottom