Majambazi wavamia Benki ya Stanbic tawi la Mayfair, Msasani

Majambazi wavamia Benki ya Stanbic tawi la Mayfair, Msasani

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,032
Reaction score
64,143
2013_7$thumbimg124_Jul_2013_164001233.jpg

Benki ya Stanbic tawi la Mayfair, Msasani, Dar, leo imevamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi na kupora kiasi kikubwa cha pesa.

Wamekuja na Noah nyeusi wakapark kama wateja. Walikua wawili, mmoja akapanga msitari mwingine akaenda kujaza fomu za kuchukulia hela. Yule alopanga msitari akafunga mlango na yule Askari akakunjwa akanyang'anywa alarm. Yule alokuwa anajaza fomu kawambia wateja nyote lala chini, alikua anamjua mwenye ufunguo, wakasema Anna leta huo ufunguo. Akataka kugoma walipomnyoshea mtutu akatoa. wakaingia Kwenye chumba cha hela wakakomba hela zote wakapakia kwenye Noah.

Wakawaaga na kusema iteni hao Polisi wenu. Hamna aliyeumizwa zaidi ya Askari kukunjwakunjwa alipotaka kubonyeza alarm.

Today at stanbic mayfair plaza:

...Gang of armed robberies, arrest security guard, took the remote buton and proceed to strong room key custodian who was coming from wash room they open the strong room and ATM took all money Customers, USD 175,000/-, Euro 260,000, £190,Tzs 186mil. ATM 30mil....

Staff and our guard locked in strong room and they left keys at bank counter. Initial investgtn shows there was an inside job, why teller's didn't press alarm at first when security guard kept under arrest of robberies? They ran away by car...

all staff being sent to Police for statements.
======================
Updates kutoka Mwananchi la leo

Dar es Salaam. Watu 13 wakiwamo wafanyakazi tisa wa Benki ya Stanbic jijini hapa wanashikiliwa na polisi baada ya majambazi kuiba fedha zaidi ya Sh1 bilioni jana jioni.

Watu hao wanashikiliwa katika Kituo cha Oysterbay kwa uchunguzi zaidi wa uporaji huo uliofanywa na majambazi yenye silaha yaliyoingia katika Tawi la benki hiyo la Mayfair Plaza lililopo Barabara ya Mwai Kibaki na kutokomea na kitita hicho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, aliliambia gazeti hili jana kuwa watu wengine wanne wanaoshiliwa ni askari aliyekuwa lindo na wengine watatu ambao hakuwa tayari kuwataja.

Wambura ndiye aliyeongoza kikosi cha askari kanzu na wenye sare kufanya uchunguzi wa awali katika jengo la benki hiyo ili kujiridhisha na kilichotokea katika tukio hilo. Alisema kiasi kamili cha fedha zilizoibwa kitatolewa baadaye baada ya polisi kukamilisha uchunguzi wao.

"Siwezi kusema leo moja kwa moja kiasi kamili cha fedha zilizoibwa kwa sababu kila mmoja tuliyemhoji anatoa kiwango tofauti," alisema Wambura.

Hata hivyo, chanzo chetu cha habari ambacho hakikutaka kitajwe gazetini, kilidai kuwa hadi jana alasiri, maofisa wa benki hiyo waliokuwa wanashiriki uchunguzi, walibainisha kuwa kiasi cha zaidi ya Sh1.0943 bilioni kilikuwa kimeibwa.

Chanzo hicho kilibainisha kuwa kiwango hicho cha fedha kinajumuisha sarafu mbalimbali zikiwamo fedha za Tanzania, Euro, Pauni na Dola za Marekani.

Habari zilizopatikana baadaye kutokana katika chanzo chetu, zilidai kuwa fedha zilizoibwa ni Euro 260,000 (Sh598 million), Dola za Marekani 175,000 (Sh280milioni), Sh216 milioni za Tanzania, na pauni 190 za Uingereza (Sh380,000).
 
Baadhi ya watumishi wa beki watakuwa wanahusika tu hii ni mipango kwanza mpaka jambazi ajue pesa ziko chumba gani siyo rahisi lazima amepata maelekezo toka kwa watumishi wasio waminifu.
 
Gari zenye tinted ni marufuku kupaki benk. Tamko hilo linakuja soon by kova
 
Today at stanbic mayfair plaza:

...Gang of armed robberies, arrest security guard, took the remote buton and proceed to strong room key custodian who was coming from wash room they open the strong room and ATM took all money Customers, USD 175,000/-, Euro 260,000, £190,Tzs 186mil. ATM 30mil....

Staff and our guard locked in strong room and they left keys at bank counter. Initial investgtn shows there was an inside job, why teller's didn't press alarm at first when security guard kept under arrest of robberies? They ran away by car...

all staff being sent to Police for statements.
 
Today at stanbic mayfair plaza
...Gang of armed robberies,arrest security guard ,took the remote buton and proceed to strong room key custodian who was coming from wash room they open the strong room and ATM took all money Customers,USD 175,000/-, Euro 260,000,£190,Tzs 186mil. ATM 30mil....staff and our guard locked in strong room and they left keys at bank counter.initial investgtn shows there was an inside job,why teller's didn't press alarm at first when security guard kept under arrest of robberies. They ran away by car...all staff
being sent to Police for statements.

polisi nao pia ni wezi na majambaz,juma 3 imeripotiwa polisi waliwekwa selo kwa kuuza kidhibiti kituo cha kimara,ilikua mitungi
 
Mbona kama tukio limekuwa staged,kama lile la Barclays hv,time will tell!
 
"USD 175,000/-, Euro 260,000,£190,Tzs 186mil. ATM 30mil"

Mmmmmhhh Ngumu kumeza kwa hapo kuwa na kihasi kikubwa cha fedha.
 
Back
Top Bottom