Majambazi nomaaaaaaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi nomaaaaaaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Oct 9, 2009.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,422
  Likes Received: 22,335
  Trophy Points: 280
  MZIMU wa ujambazi umeendelea kutesa jijini ambapo jana kundi la majambazi wamevamia tena Kimara Stop Over na kumuua kwa kumpiga risasi mgongoni Afisa Mauzo wa Kampuni ya Lubricant, Gosbert Kanyika (32).

  Chanzo chetu cha habari kutoka eneo la tukio kimedai kuwa majambazi hayo yalivamia katika nyumba ya afisa huyo muda mfupi baada ya marehemu na familia yake kuingia ndani wakitoka hospitali kutibiwa.

  Imedaiwa kuwa mara baada ya Gosbert na familia yake kutibiwa walikodi taksi na kurejea nyumbani na walipoingia ndipo majambazi hao waliokuwa na bunduki walipovamia na kuwalazimisha kutoa fedha.

  Katika purukshani hizo majambazi hao walimvaa Gosbert na kumlazimisha awape fedha na ndipo walipoanza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia silaha zenye ncha kali walizokuwa nazo.

  Wakati uhalifu huo ukiendelea, majambazi wengine walianza kupekua nyumba hiyo wakitafuta fedha na mali ambapo inadaiwa kuwa waliambulia sh 8,000.

  Majambazi hao kuona hivyo walianza kumshambulia mke wa mwenye nyumba hiyo kwa kumpiga na silaha zenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake.

  Kisha majambazi hao walimchukua Gosbert na kwenda naye nje kisha kumpiga risasi mgongoni na kufariki papo hapo na kisha majambazi hao kutoweka.

  Majeruhi aliyefahamika kwa jina la Catherine, ambaye ni mke wa marehemu Gosbert, amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili akiendelea kupata matibabu na maiti imehifadhiwa hospitalini hapo.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema taarifa kamili zitatolewa baadaye leo.


  SOUCE
  MAJIRA
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Huh....Hizo hela walikuwa wameweka kwake! Pole sana Familia ya Marehemu. Huu ujambazi hasa katika Eneo la Kimara nadhani unatakiwa kuwekewa jicho la tatu, maana mmetuambia juzijuzi kwamba ni hukohuko tena wamevamia Kanisa la KKKT na kupora mali kibao.Mungu ilaze pema peponi roho ya Marhum!
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Tragic end of the guy's life.This is a reminder that more has to be done to combat crime in TZ
   
 4. M

  Mchili JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mh poleni sana famila ya Gosbert. Inasikitisha sana, bila hata huruma!!!!!!
   
 5. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Duh! Kweli tuombe polisi ifanye kazi...
   
 6. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hapo kwa kweli Polisi wanatakiwa kuonyesha makucha halisi. Hakuna aliyeko salama sasa. Polisi wamelala? Pole sana jamani, mwe!

  Leka
   
 7. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Majambazi ni wanyama wa hali ya juu. Hivi kwenye karne ya leo wanategemea kumkuta mtu na burungutu la fedha nyumbani wakati benki zipo? May GOD forbid.
   
 8. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145

  Eneo hili kati ya Kimara Mbezi lina vituo viwili y polisi. Kimoja kipo imara kingine Mbezi wa Yusufu. Utashangaa maaskari wa vituo hivi wanafanya nini.

  Je inawezekana mauaji ya huyu jamaa ni ya kulipiza kisasi kwani kwa dunia ya sasa hivi jambazi anavamia nyumbani kwa mtu na kutegemea kukuta pesa ndani kweli? Nina wasiwasi!!!!!!

  Ukweli ni kwamba Kova Dar Es Salaam inaelekea kumshinda kabisa. Hawa maaskari wapanda pikipiki badala ya kufuatilia majambazi wako busy na kukamata magari yanayotanua barabarani na makosa mengine yanayopashwa kufuatiliwa na traffic police.

  Poleni wafiwa.

  Tiba
   
 9. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Rest in peace Gothbert.
  Ujambazi sijui ndio kipimo cha maendeleo?MAREKANI IMEKUWA INASHIKILIA REKODI YA DUNIA YA UHALIFU WA KUTUMIA SILAHA(nisahihishwe kama sipo sawa).
  Kunapokuwa na tofauti ya kipato ktk jamii ndio mambo yake yanaanza hivyo.Itafikia kipindi KIKUNDI CHA WAHALIFU(majambazi) kuomba kazi ya ULINZI KWENYE TAASISI NA MASHIRIKA,WAKINYIMWA WANAKUJA "KUCHUKUA"
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Huwezi kupambana na uhalifu kwa kutumia bunduki au kuajili polisi wengi. Dawa ya kumaliza uhalifu ni kutengeneza mazingira mazuri ya ajira za vijana. Hili ni tatizo kwa nchi yetu wanasiasa hawalioni hili.

  Wao wanafikiria kujilimbikizia mali tu, kwa kuwa wanajua kuwa watapatiwa ulinzi wa kutosha maisha yao yote, haki ambayo anastahili kila mtanzania kwa kuwapatia mazingira mazuri ya kuishi vijana ili wasijiingize kwenye uhalifu.
   
 11. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Amini usiamini hakuna mnyama asiyefugika,maadam umegundua kuwa hawa ni wanyama basi ujue kuna mtu anawafuga na anawatafutia malisho yaliyo mema,ndio maana wanafanikiwa kwa asilimia kubwa!!
   
Loading...