GHIBUU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 4,432
- 3,016
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hana mamlaka ya kuingilia na kutoa maagizo kwa mambo ya #Zanzibar yasiyo mambo ya Muungano. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na Katiba ya Zanzibar ya 1984 imeainisha waziwazi mamlaka ya Serikali mbili zilizopo." @MazruiNasso
====
====
Zanzibar. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda, Juma Hassan Reli ahakikishe anazuia utoaji wa vibali vya kuingiza sukari kutoka nje hadi sukari inayozalishwa na kiwanda cha sukari cha Zanzibar kilichopo Mahonda iishe.
Amesema haiwezekani kiwanda hicho cha pekee kinachozalisha tani 6,000 za sukari kwa mwaka kikakosa wateja wakati mahitaji ya sukari Zanzibar ni tani 36,000 kwa mwaka.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumamosi, Januari 18, 2020 wakati alipotembelea kiwanda cha kuzalisha sukari cha Zanzibar kilichopo katika eneo la Mahonda wilaya ya Kaskazini ‘A’ mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema ni vizuri wizara ikahakikisha sukari inayozalishwa na kiwanda hicho inapewa kipaumbele cha kwanza kwa kununuliwa kwa sababu wana uhakika na ubora wake kwa kuwa wameshuhudia uzalishaji wake kuanzia hatua ya awali miwa ikiwa shambani.
“Wizara ya viwanda lazima mbadilike na muweke utaratibu mzuri wa kusimamia uingizwaji wa sukari kutoka nje. Haiwezekani sukari inayozalishwa ndani ikakosa soko kutokana na uingizwaji wa sukari kutoka nje. Hatuwezi kumfurahisha mtu mmoja huku wengi wakiumia.”
Mwananchi