Majaliwa amekagua matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan

Matengezo tu ambao sio ujenzi mpya ni 1.5 Bln, Ghorofa zile hostel Mpyaaaaaaaaa 10Bln? Haya Tutafanyaje sasa.
Yaani Ukarabati wa Makazi unalingana na Ujenzi wa Majengo Matatu Mapya ya zile Hostel pale Mawasiliano.
Hii nchi bana upigaji ni cancer aisee, kuisha ni ngumu sana
 
Hiyo Mil 680 ni ya kutenganisha watumishi na wasaidizi wa makamu wa Rais kwa vp?

Inatumika kama gharama ya usafiri wa kuwahamisha au?
 
Yaani Ukarabati wa Makazi unalingana na Ujenzi wa Majengo Matatu Mapya ya zile Hostel pale Mawasiliano.
Hii nchi bana upigaji ni cancer aisee, kuisha ni ngumu sana
Kila mtu ana namna yake ila wanatufanya kama mazwazwa vile kwamba hatuwez kuona wala kuhoj
 
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan atakapohamia Dodoma.

Akague na eksipasheni jointi zilizo achwa kama ni zigzag au mnyooko zinazofika hadi kwenye marumaru..

Nimecheka sana, angalie mamboleo asikuhitaji
 
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan atakapohamia Dodoma.

Waziri mkuu amefanya ukaguzi huo leo Jumatano, Desemba 6, 2017 mchana katika eneo la Kilimani mjini Dodoma ambako yalikuwa makazi ya mkuu wa mkoa.

Akitoa taarifa ya ujenzi, Waziri wa Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Wenye Ulemavu na Vijana, Jenista Mhagama amesema kikosi kazi cha kuratibu kazi ya Serikali kuhamia Dodoma kilibaini mahali alipokuwa akiishi awali si sahihi kwa ajili ya makazi ya kudumu ya Makamu wa Rais.

“Pale palikuwa panafaa kwa ajili ya ziara za kikazi alipokuwa akija Dodoma, kwa hiyo tumeamua tufanye ukarabati hapa ili aweze kuishi kwa viwango vinavyostahili,” amesema katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema kazi ya matengenezo itagharimu Sh1.5 bilioni wakati kazi ya kutenganisha ofisi za watumishi na wasaidizi wa Makamu wa Rais itagharimu Sh680 milioni.

Waziri mkuu pia amekagua matengenezo ya ofisi inayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais ambayo itakuwa eneo la Ndejengwa.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma, Steven Simba anayesimamia ujenzi huo amesema wanataraji kazi itakamilika kabla ya Desemba 30, 2017.
kwanini wasijenge kaghorofa kamoja tu kama UDSM ili tuweze kuokoa gharama kuliko kufanya yote hayo.? Naamini serikali yangu sikivu itachukua mawazo yetu.
 
Sidhani kama gharama kubwa ipo kwenye matofali zaidi itakuwa kwenye maeneo ya usalama, mawasiliano na comfort.
Mayonene....NKima/Ngosha acha kutetea uozo...

kama majengo ya hostels za udsm ni 10bil....iweje hiyo nyumba tena ukarabati utumie 1.5 bil....

hiyo security unayoiongelea ni ipi hasa...mbona nyumba zote za viongozi ulinzi unaanzia kwa jirani mita 500 toka nyumbani kwa kiongozi...tena wanafanya polisi na usalama wa taifa wanaolipwa mishahara ya serikali.

HAPA KWENYE UKARABATI KUNA KITU SIO BUREEE....UWIANO WA TBA KUFANYA HOSTELS KWA 10BIL NA TBA HAOHAO KUFANYA NUMBA UKARABATI KWA 1.5BIL...IKO JAMBO HAPO...nakumbuka ukarabati wa nyumba ya Jacob Zuma wa south africa...

Iko namna khanjibhai...
 
..Ndiyo maana wengine tunapinga uamuzi wa kukurupuka kuhamia Dodoma.

..mabilioni ya fedha wanayotumia kujenga makazi na maofisi kwa ajili ya watumishi wa serekali Dodoma yangeweza kuwekezwa ktk sekta za uzalishaji kama viwanda na kilimo.

.
Sema wewe kaka...tukisema sie tutaitwa wachochezi...

gharama za kuhamia dodoma hata nyerere aliziogopa maana zinawanyima watanzania haki ya kufurahia matunda ya kuwa huru...

huwezi na haiwezekani kwa kiongozi makini kupuuzia uwekezaji katika watu wake na kuwekeza katika vitu ili uache legacy...

haikubaliki na wala haimithiliki kuhamia dodoma kwa expenses za madawa hospital kukosekana, wanafunzi kukosa elimu kisa mikopo hakuna, wafanyakazi kunyimwa stahiki zao..wakulima kukosa masoko ya mazao yao...na mengineyo kede wa kede.
 
kati ya vitu vilivyompandisha hadhi magufuli na kuwazidi maraisi waliomtangulia ni kuipeleka serikali kati kati ya nchi yaani Dodoma.
Na kati ya projects zinazomkwamisha mkulu kumwamo na kumchelewesha kukubalika na kuheshimika ni pamoja na hiyo...lakini kwa mpangilio naomba nianze na hizi....kama zipo zingine wadau wataongezea

1÷Project MAKAO MAKUU DODOMA

2÷Project FUFUA ATC BOMBADIERZ

3÷Project TREN YA UMEME

4÷Project FLYOVERS ZA DSM NA DARAJA LA COCO BEACH SALENDER

5÷ ........

Hizi projects atamaliza miaka 10 na kuomba aongezewe kabla hajaona matunda ya uwekezaji huo kwa wananchi wa kawaida na wapiga kura wake kwa ujumla.

Ashauriwe kusikiliza maoni ya wataalam wa uchumi...

personal desires and ambitions to leave LEGACY (Nation's Hero)when you are gone will not help the nation at large except him and people close to him.

I do hope the oposite of legacy is curse or what....a public enemy
 
Nyumba ya makamu wa raisi (marekebisho) ni 1.5bn ? Au sijaelewa. .TBA si ndio walijenga block za udsm kwa 500m per jengo?? Shubhaaaamit
Ila wanasema hawana hela za kuongeza mishahara ya madiwani, wafanyakazi serikalini n.k. n.k.!
kwa hela hizo, vijiji 30 wangepata zile 50m/- walizoahidiwa!
Twarudi pale pale, utumiaji wa hela za umma bado una ukakasi, ya mhimu hatutaki, ila kama haya wala hatuoni tatizo, zinamwagwa tu! Kama vile .....Inauma sana aise :(:mad:
Halafu hawataki kupingwa wala kuulizwa kwanini hela zote hizo zimetumika kukarabati, siyo kujenga mkuu, KUKARABATI MAKAZI?!
 
Nyumba ya makamu wa raisi (marekebisho) ni 1.5bn ? Au sijaelewa.

..
TBA si ndio walijenga block za udsm kwa 500m per jengo??

Shubhaaaamit

Kiuzito ujenzi/Marekebisho unategemea aina ya design, construction material haswa suala la security na status linapokuwa la msisitizo (Makazi ya Makamu wa Rais) lakini kuhusu mabweni kuwa 500mn sina la kusema
 
Back
Top Bottom