Majaji waonywa kesi za mafisadi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,954
22,125
Habari zaidi!
Majaji waonywa kesi za mafisadi
Theopista Nsanzugwanko
Daily News; Wednesday,February 25, 2009 @19:41

Jaji Kiongozi mpya, Fakih Jundu ameapishwa na kuwataka majaji na mahakimu kuwa makini katika kutoa uamuzi wa kesi zinazohusu mashitaka ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Jundu, ambaye aliapishwa leo na Rais Jakaya Kikwete, alisema Idara ya Mahakama inakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwamo kesi mpya za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

“Kesi hizi za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ni mpya katika mahakama zetu, hivyo ni lazima mahakimu na majaji kuwa makini kutokana na kuwa jamii nzima inafuatilia kesi hizo kwa makini na kupima uamuzi wenu,” alisema.

Jaji kiongozi huyo alisema katika nafasi hiyo mpya, atakabiliwa na changamoto kuhakikisha uendeshaji wa kesi hizo unafanyika kwa umakini. Alisema changamoto nyingine inayoikabili mahakama ni uhaba wa mahakimu ambao unachangia ucheleweshaji wa kesi.

Alitoa mfano wa mkoa wa Dar es Salaam, na kusema hakimu mmoja anahudumia wastani wa kesi 400. Kwa upande wa mahakama za mwanzo, alisema zipo 1,000 wakati mahakimu ni 600. Jaji Jundu alisema atahakikisha anafanya kazi ili kuona maelekezo na maagizo ya Jaji Mkuu yanatekelezwa, na kutenda haki kutakakoifanya jamii iwe na imani na mhimili huo. Kabla ya uteuzi huo, Jundu alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Iringa. Ameshika nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Jaji Salum Massati aliyeteuliwa na Rais kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
 
Wape vitendea kazi kwanza kabla ya kuanza kutoa maonyo ! wana mafunzo ya kuendesha kesi hizo ?wana makarani wa kutosha? wana ulinzi? wana muda wa kutosha ? wana kesi ngapi za kusikiliza ?Umekaa nao kujua matatizo yao ?
 
Jaji Kiongozi anasema "kesi hizi za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka ni mpya katika mahakama zetu..." -- ni kesi zipi walizozizoea -- zile against small fish, yaani watuhumiwa wadogo wadogo tu? Hata hivyo tukubali ni changamoto kubwa kwao, ingawa kwa mfumo wetu kesi za jinai ni mali ya Jamhuri -- yaani serikali, inaweza wakati wowote wakaiondoa ikionekana serikali au wakuu wake fulani wanaumbuka. Naami ni robo tu ya kesi zote za ufisadi zilizopelekwa mahakamani hadi sasa zitaisha kikamilifu na watuhumiwa kupatikana na hatia. Hawatakuwa wale high profile. You wanna bet?
 
Huyu naye kumbe hata hafikirii nini cha kusema , ama kwa vile ndio kawa exposed kwenye media basi akaona hawezi kukaa kimya?
 
Back
Top Bottom