Maiti ya mtoto yakutwa juu ya kaburi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maiti ya mtoto yakutwa juu ya kaburi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msharika, Mar 20, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MAITI ya mtoto mdogo wa kike anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili hadi mitatu, imekutwa juu ya kaburi katika eneo la Buguruni Madenge, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema maiti huyo ambaye hajatambuliwa, aliokotwa juzi saa 5 asubuhi.

  Alisema mwili wa mtoto huyo uliokotwa ukiwa hauna jeraha lolote, ingawa alikuwa anatokwa na povu mdomoni na kwamba mpaka sasa haijajulikana maiti huyo alifikaje juu ya kaburi hilo na kwa madhumuni gani.

  Aidha, Kamanda Shilogile alisema sababu na chanzo cha kifo cha mtoto huyo hakijafahamika na maiti amehifadhiwa Hospitali ya Amana kwa uchunguzi zaidi huku Polisi ikiendelea na msako dhidi ya watuhumiwa.

  Akizungumza kwa simu jana kufafanua tukio hilo, Kamanda Shilogile alisema hawajamkamata mtu yeyote kuhusiana na tukio hilo ambalo lina utata. “Mtoto alikuwa amefunikwa kwa nguo.

  Hakuwa na jeraha lolote. Lakini unaweza kujiuliza maswali mengi kuhusu tukio zima. Je, alitupwa hapo? Alikuwa anaumwa, au ilikuwaje,” alisema Kamanda Shilogile na kuongeza kwamba hata mazingira ya kulihusisha na ushirikina, pia inawezekana.

  Wakati huohuo, mtoto mwingine wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka tisa hadi 12, amekutwa amekufa huku maiti akiwa anaelea juu ya mto Mzinga uliopo Wilaya ya Temeke.

  Maiti huyo aliokotwa juzi saa nane mchana na inasadikiwa kwamba chanzo cha kifo chake ni kunywa maji mengi wakati akiogelea na wenzake katika maeneo hayo.

  Kwa mujibu wa Polisi, pembeni mwa mto huo zilikutwa nguo za marehemu, kandambili, sabuni na kwamba maiti amehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke na upelelezi zaidi unaendelea.

  Source: habari leo
   
 2. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Jamani haya mambo mbona yanatisha tena???/
   
Loading...