yaweza kuwa, binti tajiri kaamua kuolewa na kijana hohe hahe, akamuwezesha huyo mumewe, baada ya biashara kumchanganyia, mume amekuwa jeuri, kiburi na nyumba ndogo lukuki, hasikii la muadhini wala la mnadi swala...kamtelekeza mkewe!
yaweza kuwa, mume kabeba boksi ughaibuni usiku na mchana, kakopa huku na kule almuradi amlete mkewe toka Bongo wayafwaudu wote maisha ughaibuni. Baada ya mke kufika ughaibuni, kalaghaiwa na wajanja, hamtaki tena mume... anadai mshamba na madharau mengine lukuki!
yaweza kuwa,... Mifano mingi...
Hii inaonyesha jinsi binadamu asivyotabirika, awe mume au mke au siyo??? Asante kwa mifano.