Maisha

Sasa huo mfungo umewasaidia nini
 
Hao wadada mtu mwenye roho chafu kama hiyo ndio wana kaa na kudumu miaka kwa miaka ila ishi nae wewe ki ubinadamu na utu vituko kila leo.
Nilikuwa sijasoma hii comment kabla sijaandika yangu.

huwa nahisi pengine sehemu za watu wenye roho ngumu, huwa wanawachukulia kama wafanyakazi so ni kufanya kazi upate mshahara Ila hizi sehemu zingine huwa wanajisahau na kuanza kutaka haki sawa na kila mtu. Mwisho wa siku inaibuka dharau, jeuri na udhembe kwa kuona anawamudu
 
Waarabu makatili sana ndiomana hawaoni shida kujitoa muhanga..!!
 
msichana huyu unayemfanyia hivi, ndiye huyo huyo kesho unaenda kazini unamwachia mtoto mdogo hapo nyumbani na unarudi unamkuta mtoto salama!!...inafikirisha sana
 
Wamama wenye sura za namna hiyo wanakuwaga na rohoo mbaya sana.
Kabisaa yaani 100 percent. Kuna mama mmoja nilienda kufanyia kazi kwake miaka fulani ana sura ya hivyo. Ni ana roho mbaya Iddy Amini arudi shule. Bahati mbaya nilikuwa naharisha tumbo linauma. Hadi kuingia uani naogopa kishenzi sababu ya ukali wake anaweza akakujazia nzi. Ikawa kila tumbo likivuruga natoka naenda kunya sokoni

Anakaa na kadada pale anakanyanyasa vibaya mno yaani kuna time hadi unatamani uingilie kati umkingie kifua yule dada kwa anavyomtenda.

Yaani hadi inafikia time unawaza au ndio nime-meet live na shetani mwenyewe tunaemsoma kwenye baibo?
 
Yaani kama ulikiwepo, mshahara wake kwa muda, nguo namnunulia na wanangu, chakula anakula anavyopenda. Siku moja akaleta bwana ndani. Akajificha mabandani baada ya mwenyewe kuingia. Jamaa akasepa kipakapaka, unajua paka akikimbia kiwiziwizi,
Mimi sina huruma kwa hiyo picha kwa kweli,sehemu yenye utulivu hawakai ni vituko kuvimba,kisirani na Jeuri .
 
Mimi nina dada yangu ana roho mbaya mpaka sisi familia tumenyoosha mikono juu๐Ÿ™Œ๐Ÿปila ana Mfanyakazi wake huu mwaka wa 5 ukifika pale mpaka unajiuliza huyu binti hana wazazi aondoke mahali hapa maana si kwa kazi zile bila kupumzika.
 
Binadamu ni kiumbe katili akiamua, then unakuta watu kama hao eti ni watu wa ibada sana ๐Ÿ˜ณ shetani mwenyewe sometimes anatuoneaga huruma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ