Mfilisti
JF-Expert Member
- Sep 24, 2015
- 3,729
- 19,466
Mtanzania leo siyo tu maskini, bali amegeuzwa kuwa mtumwa wa mifumo ya kifisadi. Kodi yake inanyonya damu yake, lakini matunda yake yanaliwa na mafisadi wachache waliovaa suti na kujipa heshima za “viongozi.” Hawa ndio mabwana wa jasho letu wanakaa ofisini/Bungeni wakisaini mikataba ya kifisadi, wakigawana rasilimali za taifa kana kwamba ni urithi wa familia zao.
Wananchi wanapiga kelele kuhusu bei za bidhaa, gharama za maisha na ukosefu wa ajira, lakini viongozi wanakula bata, wakijenga majumba, wakisomesha watoto nje ya nchi, na kufuja mali bila hata aibu. Wametengeneza tabaka dogo la “wanaoishi peponi” juu ya mgongo wa wananchi wanaoishi motoni.
Huduma za afya zimegeuzwa kuwa biashara, elimu ni dili la wachache, barabara zimejaa mashimo kama vidonda vya taifa, huku wakubwa wakiendelea kuhubiri porojo za maendeleo hewani. Huu ni usanii wa kisiasa, na wananchi ndiyo wahanga.
Mtanzania wa kawaida leo hana tena heshima wala thamani mbele ya dola lake. Taifa limeuzwa vipande vipande. Na waliotufikisha hapa wanatembea kifua mbele, wakituzomea kwa majukwaa kwa maneno ya kejeli wakijinasibu eti sisi ni wachache kuliko wao.
Huu ndiyo ukweli mchungu: Watanzania tunateseka kwa sababu tumekabidhi nchi mikononi mwa majambazi waliovaa suti wakijiita viongozi, Tumeuza nchi kwa vipande vya Kanga na Shilingi Elfu ishirini.