Maisha yetu hapa duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha yetu hapa duniani

Discussion in 'Great Thinkers' started by Shayu, Aug 2, 2016.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Aug 2, 2016
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 502
  Likes Received: 640
  Trophy Points: 180
  Siku zetu zinakwisha hapa duniani tukiwa tumevaa miili tofauti kwenye uhai wetu. Kwanza utoto kisha ujana na uzee. Tunaishi, tunakufa tunaacha kizazi kingine kikiendelea kuishi.

  Maisha yetu hapa duniani ni kama hadithi ni kama kitabu kilichofunguliwa na kusomwa na mwisho wetu ni kama kitabu kinavyofungwa. Matendo yetu yote mabaya na mazuri kurasa zake zinafungwa kwa kifo. Unapokufa ukurasa wako unafungwa. Na kitabu kimefika mwisho.

  Lakini mtu mwenye hekima yuko makini kutenda matendo yenye adili na mema. Kwakuwa anapenda kuwa mwenye amani na kufa kama mtu aliyeko usingizini.

  Wakati mwanzo ulikuwa kijana mwenye nguvukama tai, lakini utakuja kushikilia mkongojo. Hili ni muhimu kufahamu kama kijana na utengeneze maisha yako sasa kwa kumjua Mungu.

  Muda unakwenda na mabadiliko ndani yetu yanaendelea kufanyika. Kumbuka uliwahi kuwa mtoto na sasa uko kijana na uzee unakufuata.

  Na unapaswa kujua kwamba kaburi linakukaribia kadiri unavyoendelea kukua.

  Hauwezi kuendelea kuwa nao mwili huu unaoutumia kutembelea na kuutumia kutendea uovu ama wema hapa duniani.

  Fahamu kwamba roho yetu tunaitengeneza kuwa ya mtu mwema au mwovu kwa matendo yetu. Tenda mema kwa watu wengine . Na kuwa na roho nzuri.

  Na ni Mungu ndiye atakaye tuhukumu wote kadiri ya matendo yetu.

  Mambo yote tunayoyahangaikia tukiwa hapa duniani hatutaweza kuondoka nayo tukifa.

  Bali yale mema tuliyotenda tukiwa hai yataendelea hayatokufa. Yatabaki mioyoni mwa watu kizazi hadi kizazi yatahadidhiwa. Roho ya mtu mwema haifi.
  Hukaa mioyoni mwa vizazi na vizazi.

  Kizazi cha waovu kitasahaulika.
   
Loading...