Kilongwe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2008
- 423
- 116
Swali ambalo mara nyingi huwa ninajiuliza ni kuwa, maisha yatakuwaje siku bila Internet au kompyuta au simu? ni dhahiri kuwa maisha yatakuwa ya upweke yenye visirani vingi. Ukweli ni kuwa Internet imetuletea mabadiriko mengi sana, sio tu imeweza kurahisisha utendaji kazi na kuwa sehemu ya kazi bali pia imeweza kuufanya ulimwengu kuwa mdogo na wenye ushirikiano.
Tatizo kubwa la binadamu ni mazoea, kwani kama wewe unasoma makala hii, ni dhahiri utakuwa tayari umeshazoea Internet na baada ya kuzoea utakuwa umeonja faida zitokanazo na Internet, ni kweli kabisa, siku atakapotukoza, tutammiss sana Bw Internet.
Internet imeweza kuondoa siri na maficho ambayo hapo zamani ni wachache mno walikuwa wenye uwezo nayo. Kwa maneno mengi tunaweza kusema, internet ni mkombozi wa mwanadamu. Katika siku za karibuni kumetolewa takwimu ya matumizi ya internet na vinasaba vyake, mwenye macho haambiwi tazama, hebu tuangalie kwanza. Halafu tutakuja na tafakari juu ya umuhimu au maana ya takwimu hizi kwa Tanzania.
Original Post: AfroIT