Hapo ni sawa na mdada anayetaka kuacha shule ili aolewe. Yaani kuolewa kupo tu, hata akiwa na elimu yake ataolewa tu, na wewe vile vile biashara zipo tu, maliza kwanza hilo la shule. Usikimbilie penye wepesi fanya gumu kwanza hayo mepesi yatakuja tu. Wazazi ndio wanauchungu sana na wewe na wao wanajua nini ni jambo zuri kwako. Nakupa siri moja ukimaliza shule hutowaza tena kwenda kuuza juice ya miwa utawaza kufanya vitu vikubwa zaidi. Ila ukitaka kupauka mtaani acha shule kimbilia mtaani. Shule kweli haina maana lakini uwe nayo kwanza, kama hauna inakua ina maana sana.