Twinawe
JF-Expert Member
- Oct 3, 2016
- 2,411
- 5,289
Mimi ni kijana umri miaka 21 ,nimemaliza kidato cha sita mwaka jana ila matokeo hayakuwa vizuri nilikosa credit moja kuwa nA kigezo cha kusoma degree.
Hivyo nilijiunga kusoma diploma ya IT chuo kimoja hapa Tanzania japo nilikubali kusoma shingo upande kutokana na msukumo wa ndugu na wazazi maana Mimi nilikata tamaa ya kusoma baada ya matokeo. Nilitamani kujiajiri japo Hakuna mzazi au ndugu aliyebariki mawazo yangu. Hata ndoto yangu kusoma degree ulikuwa kusomea mambo ya biashara au utawala maana ndoto yangu kubwa ni kujiajiri.
Tangu nije hapa chuoni mwaka jana mambo hayaendi masomo magumu nafeli japo sio Sana lakini nasoma kwa kutumia energy kubwa stress haziishi hasa likija swala la ukata wa pesa. Pesa imekuwa mgumu Sana kutoka kwa wazazi kutokana na kipato chao hata majukumu yanayowakabili.
Wazo nililonalo ndugu zangu nataka nijiajiri japo sina mtaji kama cash ila kuna Wazo ninalo nawaza Kusitisha masomo japo sitawaambia wazazi, nataka Ada watakazonitumia ndo uwe mtaji wa biashara ninayotaka kujiajiri. Nataka niende veta wanichongee machine ya kukamua juice ya miwa nataka nianziea hapo nifungue na kimghahawa cha kuuzia watu wa vipato vya chini ila Wazo kuu biashara ninayotaka kufanya ni biashara ya mazao hasa katika mikoa ya mbeya, morogoro, mwanza naleta bidhaa dar pia mungu akisaidia niwe nA mashine kubwa za kusaga maindi na kukoboa napunga.
Naombeni mawazo ndugu zangu nakoelekea kuzuri au ndo nimepoteza mwelekeo namtafuta majuto na laana.
Nakaribisha mawazo yenu na ushauri mnishauri kama mtoto wako au ndugu wa muhimu Kwako. Nimechoka na Maisha ya kutumiwa elfu kumi kila wiki