Maisha ya viongozi

Basi Nenda

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
20,190
45,922
ni watu kama wengine tu ,lakini umewahi kujiuliza nyuma ya ulinzi mzito na ukuta mrefu kuna nini ? wanaishije ? wakitoka kazini wanafanya nini ? wanakula nini ? wanalala wapi ?
hasa ukizingatia viongozi wote wababe ki ukweli huwa hakuna watu wengi wanaojua wanalala wapi,mtu kama saddam hussein hakulala nyumba moja siku mbili mfululizo,gaddafi alilala chini ya ardhi, nk,
yafuatayo ni maisha binafsi ya viongozi ambao wengi huwaita ma dikteta na huogopwa mno ila ki ukweli viongozi hawa waliogopa watu ,raia hivyo walijiwekea ulinzi

1.ADOLPH HITLER
alikuwa na nyumba nyingi ikiwemo ile maarufu iitwayo belghof iliyopo milimani, hitrel hakukaa sana ikulu bali alipendelea kuishi kwenye makazi yake hasa belghof ambapo aliweka ma handaki na ulinzi wa hali ya juu,ni hapa belghof ambapo uingereza ilituma mwanajeshi sniper amuuwe hitrel lakini ikashindikana ,mara nyingi hitrel alipendelea kunywa chai muda wa jioni na alikua ni vegetarian yani hali nyama,aliajili ma house girl wadogo ki umri ili waweze kufanya kazi za ndani ikiwemo kumpikia,hitrel hakuwahi kuoa katika kipindi chote cha uongozi wake ila alimuoa eva braun aliyekua mpenzi wake wa muda mrefu masaa machache kabla hawajajiua ,binti huyu alimlazimisha sana hitrel amuoe kabla ya hapo ila hitrel alimpa jibu,nimefunga ndoa na nchi ya ujerumani, lich ya kukataa ndoa ila hitrel alimpenda binti huyu na alipata hofu alipochelewa kurudi nyumbani kwani alipenda kufanya mazoezi nje ya nyumbani, eva braun licha ya kuwa na hitrel ila hakuruhusiwa kukaa sebuleni wageni wakija,isipokua wageni wa karibu mno na hitrel,wajerumani walifichwa juu ya uwepo wa mwanamke huyu ,hitrel alikua ni mtu asiyeongea sana hovyo, hata baadhi ya ma house girl wake hawakuwai kumuona uso kwa uso na walipewa maelekezo wakisikia anakuja yani sauti za nyayo zake waende mbali yani waepuke kujionesha kwake Berghof.jpg Berghof.jpg Bundesarchiv_B_145_Bild-F051673-0059,_Adolf_Hitler_und_Eva_Braun_auf_dem_Berghof.jpg hitrel hakuwa mtu aliyeendekeza mapenzi hakuwa na muda sana na wanawake ,watatu kati ya wanawake aliowahi ku date naye walijiua kisa hakua na muda wa kuspend nao,,enzi hizo alizushiwa kuwa hana kengele moJa,hapigi mechi nk


2.GADDAFI
kiongozi huyu wa libya aliogopa sana kuuwawa na alitoa maelekezo kwa walinzi wake wasiruhusu aguswe na mtu yoyote yule na pale alipoguswa na wananchi alionekana kuwapiga makofi walinzi wake kwa uzembe wa kuruhusu aguswe, aliogopa sana kujiweka na watu hakuamini watu na nyumba zake zote alijenga mahandaki kwa chini, hata walinzi wake hawakujua analala wapi kwani ma handaki yalikua makubwa unaweza kuendeshamo gari za golf zile ndogo na ndizo alizitumia kutembea chini ya ardhi,ma handaki hayo aliyaunga na hotel kubwa za libya na viwanja vya ndege, inatajwa kuwa gaddafi alikuwa anawabaka walinzi wake wa kike waliokua ni ma bikra, walipopata mimba aliwatoa kwani nyumba zake zina hospitali kwa chini, alipenda majumba mazuri na ndege za kifahari . 31ss2.jpg col-muammar-gaddafi-libya.jpg lk.jpg


3.SADDAM HUSSEIN
alikuwa msafi sana,ili ukutane naye uliweza kusubirishwa hata saa 24 ndio umuone,na uwe msafi,unaelekezwa jinsi ya kumshika mkono,hatua ya kukaa nae ,ofisi yake kila week madokta walicheki na kukadiria kiwango cha ubaridi kwa ajili yake, aliamka mapema mno na kuanza kufanya usafi wa mwili wake kila siku,alikua halali kila siku nyumba moja,leo akilala hapa kesho pale kwa sababu za kiusalama,at his free time rais huyu alipenda kwenda mto tigris na familiia yake ku enjoy,pia alimiliki meli kubwa mbili kwa ajili yake tu, alitumia muda mwingi kusali pia alikiua akipenda kula nyama hivyo uzito wake ulikua ukiongezeka linakua swala la kitaifa watu wote mnashauriwa muache kula,aliandika hadi vitabu kuhusu kula,kuna wakati iraq ilikumbwa na njaa na ikanyimwa msaada wa chakula na jumuiya ya kimataifa,saddam alipoambiwa na watu wake kuwa njaa ni kali alijibu,tukila ipo siku tutakua minyoo hivyo tujenge miundombinu na majumba,matokeo wake watu walikufa njaa,wakati wa vita ya kuwait aliwataka wananchi wachangie dhahabu kwa ajili ya vita,baada ya vita kuisha wakati wa birthday yake saddam alionekana mtaani amebebwa na kagari ka dhahabu za wananchi huku akuvutwa na farasi article-2003044-0C875B5800000578-389_964x615.jpg

4.AL HADJI,DOCTOR,VC,CBE,MC IDD AMIN
big dady kama alivopenda kujiita na kuitwa na watoto wake alipenda kula vizuri,kuku na chips za KFC alizila mno miaka hiyo,pia alikuwa anakula machungwa 12 kila siku,alipenda magari ya bei mbaya kama vile range rover na benz,ila licha ya yote haya big dady alikua usiku halali sio kuwa ana kazi nyingi kama the man from chattow NO aliogopa kuuwawa, hakuamini hata walinzi wake,akilala anaota ndoto za mangamungamu, haya yamewahi kusemwa na mmoja ya mabinti zake huko youtube kwenye dcummentary inaitwa INSIDE A LIFE OF A DICTATOR , alikufa kutokana na kidney failure
 

Attachments

  • sss.jpg
    sss.jpg
    107.6 KB · Views: 33
  • patrimoinemobutu__Small_.jpg
    patrimoinemobutu__Small_.jpg
    27.2 KB · Views: 44
  • methode_times_prodmigration_web_bin_0c4b26f4-6870-39e5-a37c-66c7758c37a5.jpg
    methode_times_prodmigration_web_bin_0c4b26f4-6870-39e5-a37c-66c7758c37a5.jpg
    51.4 KB · Views: 38
  • col-muammar-gaddafi-libyaio.jpg
    col-muammar-gaddafi-libyaio.jpg
    80.5 KB · Views: 34
  • image-01116.jpg
    image-01116.jpg
    132.2 KB · Views: 41
  • france-views-alpes-maritimes-cap-martin-aerial-view-of-villa-del-mare-owned-by-president-mobut...jpg
    france-views-alpes-maritimes-cap-martin-aerial-view-of-villa-del-mare-owned-by-president-mobut...jpg
    141.2 KB · Views: 32
  • image-0712.jpg
    image-0712.jpg
    100.3 KB · Views: 31
Naamini vitu vyote walivyovipenda na kuvitumia kwa "ulafi " walizikwa navyo hao malaika.Ingawa umemuacha mukubwa kabisa.Papaa mwenyee. Le grande patrol Kukungweno Zabanga wa Zabanga mwana Kongolo le magnifique Mobutu 😂😂😂😂
hahaha eti malaika, una mtafuta mtu ww, kuhusu mobutu hizo picha za nyumba yenye furniture za dhahabu ni nyumba yake inaitwa villa del mare ipo cap martin ufaransa,alipenda dhahabu chooni,
 

Attachments

  • image-0712.jpg
    image-0712.jpg
    100.3 KB · Views: 27
Uchambuzi mzuri lakini mtu mashuhuri hivi ambae hata ambae hajaenda shule anamjua, wewe unambadilisha jina
Sasa hii habari ikija kufukuliwa miaka 500 ijayo watasema ni watu 2 tofauti

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Uchambuzi mzuri lakini mtu mashuhuri hivi ambae hata ambae hajaenda shule anamjua, wewe unambadilisha jina
Sasa hii habari ikija kufukuliwa miaka 500 ijayo watasema ni watu 2 tofauti

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
asante mkuu,nita edit
 
Back
Top Bottom