Maisha ya saiv tofaut na zaman

Maisha ya saiv tofaut na zaman

Nakuchukia sana

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2025
Posts
489
Reaction score
938
Kipindi ninapokuwa enzi ya `90 maisha yalikuwa kwenye,msingi ya kiamadili.Na heshima ilidumu,matukio ya kikatili hayakuwepo tofauti na sai.Ila hii karne ya 21 imezidi,matukio kila kukicha.Moyo upendo haupo tena,chuki ndio imetawala.
 
Haya ndio maendeleo yenyewe
 
Haya yote ni matokeo ya kutelekeza baadhi ya mila na desturi zetu zilizokuwa nzuri na kujikita kwenye utandawazi na kubeba yote pasipo kuchuja.

Malezi ya hovyo ndani ya familia na jamii yamepelekea mmomonyoko wa maadili. Imesababisha ongezeko la single mothers ambalo ni bomu linalosubiri kulipuka.
 
Haya yote ni matokeo ya kutelekeza baadhi ya mila na desturi zetu zilizokuwa nzuri na kujikita kwenye utandawazi na kubeba yote pasipo kuchuja.

Malezi ya hovyo ndani ya familia na jamii yamepelekea mmomonyoko wa maadili. Imesababisha ongezeko la single mothers ni bomu linalosubiri kulipuka.
Mungu akupe maisha marefu sana jerry...
 
Napenda maisha za zamani .
Niliwahi kusema hivi
Napenda maisha ya tisini..
Bora ningezaliwa miaka ya 60 sasa hv ningekua na umri wa bibi yangu an sasa hv mimi ningekua kikongwe nipp zangu mtwara msanga mkuu...

Vishu Mtata
 
Napenda maisha za zamani .
Niliwahi kusema hivi
Napenda maisha ya tisini..
Bora ningezaliwa miaka ya 80 sasa hv ningekua na umri wa bibi yangu an sasa hv mimi ningekua kikongwe nipp zangu mtwara msanga mkuu...

Vishu Mtata
mtu wa themanini awe bibi? Labda alizaa mapema sana na sekondari hakwenda
 
Maisha yamebadilika pakubwa sana, hata ndoa za sasa ni tofauti na za zamani. Za sasa hivi wanandoa hawadumu, zimejaa tamaa na usaliti, hakuna uvumilivu, miaka kumi hazifikishi zinavunjika mapemaa
 
Ikiwa ninyi watu wazima mmeshindwa kujiheshimu ni nani atakuwa na maadili??

Maadili ni nn kwanza ?

Ikiwa ndugu ndo wanagombania Mali kwa nguvu mpk wengine kutoana uhai huo upendo utoke wapi ?

Maadili yanaanzia kwako, km huna usiilaumu jamii maake wewe ni matokeo ya jamii yenyewe

Em rudi hapo komakundi ukatambikie kwanza
 
Sio bibi tu, amesema kikongwe.

Nimeshtuka sana kuona sisi wa themanini tunaitwa vikongwe

Kwa mara ya kwanza naona kikongwe wa miaka 40
kama wa themanini wanaitwa vikongwe wa sabini wataitwaje? Hawa watoto wa sasa wanazeesha watu haraka sana. Kijana wa miaka 40 anaitwa mzee!
 
Samuya ameongeza chuki na ukatiri kwa upande huu wa Tanganyika, mhhh! Mwaka huu wa 1980 mimi nilikuwa LY.
 
Maisha yamebadilika karibu kila kitu, kila sehemu, kila idara. Mijini na vijijini maisha yamebadilika mpaka mitindo ya kuvaa na kula, maisha ya kiroho nayo yamebadilika ni mpaka kwenye dini zote angalia sikukuu za kidini zinavyosherehekewa tofauti na zamani. Maadili ya dini nayo yanapuuzwa siku hizi, ndoa haziheshimiwi, watu wanachepuka na kuingilia ndoa za watu bila hofu ya Mungu. Watu wanaona kuishi bila ndoa ni fasheni na jamii inaona poa tu na masingo mama wanazidi kuongezeka huku wakiyaona maisha hayo ni bora kuliko kuishi kwenye ndoa
 
Mmomonyoko wa maadili umekuwa mkubwa sana sana siku hizi. Zamani ukipiga na kuumiza mke wako lazima utaadhibiwa kimila umpe mchuzi wa ng'ombe au mbuzi kulingana na ukubwa wa kosa, utajua utampata wapi huyo mbuzi au ng'ombe wa mchuzi. Huko makanisani ukifanya dhambi ya uasherati/uzinzi unatengwa ushirika au unafukuzwa kabisa uwe mmataifa! Siku mapastari hawaangalii hilo, wanakuambia ukifukuza watenda dhambi utapunguza matoleo, wanasema acha ngano na magugu vikue pamoja, ni Mungu tu ndio atachambua kipi ni ngano na kipi ni magugu!
 
Kipindi ninapokuwa enzi ya `90 maisha yalikuwa kwenye,msingi ya kiamadili.Na heshima ilidumu,matukio ya kikatili hayakuwepo tofauti na sai.Ila hii karne ya 21 imezidi,matukio kila kukicha.Moyo upendo haupo tena,chuki ndio imetawala.
Maisha yako hivihivi tangu zama za kale tofauti inakuwa ni environment uliyopo.
Wizi, umalaya, uuaji, uongo, unafiki, uchoyo na mengineyo yote yalikuwepo hata kabla ya Wazungu na Waarabu hawajafika Afrika.
 
Sio bibi tu, amesema kikongwe.

Nimeshtuka sana kuona sisi wa themanini tunaitwa vikongwe

Kwa mara ya kwanza naona kikongwe wa miaka 40
Daaah sijapiga mahesabu ya fasta fasta ila sijamaanisha mtu wa 40 ndo kikongwe mkuu 😂😂😂😂😂🙌🙌🙌🙌🙌
 
Napenda maisha za zamani .
Niliwahi kusema hivi
Napenda maisha ya tisini..
Bora ningezaliwa miaka ya 60 sasa hv ningekua na umri wa bibi yangu an sasa hv mimi ningekua kikongwe nipp zangu mtwara msanga mkuu...

Vishu Mtata
Kijana zamani kula mishangazi ilionekana kama laana, sijui kama ungedumu maana wanakijiji wangekuua kijana mchungulia nyuchi za wamama waliokizidi umri.
 
Back
Top Bottom