Maisha ya Mtumishi wa Serikali ni Magumu mno. Mungu aingilie kati

Innay

JF-Expert Member
Aug 22, 2014
297
291
Binadamu anapokuwa hana wa kumtegemea pale anapokata tamaa humrejea Mungu wake na kumuomba aokoe jahazi.

Tunaishi ka gidigidi.

Tuliahidiwa ahadi hewa, muda unayoyoma, hewa tupu.

Hali ni mbaya. Na hakuna matumaini. Rais Magufuli kuwa na moyo wa utu.

Hebu tizameni wenyewe hii. Ninaona aibu hata kujivunia. Miaka mingi kazini.

IMG_20200328_084003_721.jpg


Mungu atusaidie tu. Tizameni makato.
Vyama vya wafanyakazi viko wapi.
 
Mleta mada niko kinyume na wewe, badala ya mungu kuingilia Kati Kwa watumishi hebu awaangalie angalau vijana wanaoishi kwa kuokota chupa za maji na kwenda kuuza sh 100 @kg, acheni kukimbilia mikopo ili mnunue Noah ili mtese mjini, nyie wanachama wa CWT wengi wenu akili ya kunguni, mnavuta mikopo kabla hamjawa na plans za maana na hela Ya mkopo, matokeo yake mkikatwa mnaona mshahara mdogo, mimi nashauri mungu ahangaike na kada zingine kwanza
 
Maisha ya wafanyakazi sio magumu Kama unavyojaribu kuelezea. Wanauhakika wa chakula Lakini Hawana Uhakika wa anasa.

Mtazame mama mwenye watoto wanne Anaelea watoto wake peke yake kwa kutembeza machungwa, akikusikia ataona unamdhihaki Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo Mama anayetembeza machungwa ananitegemea mimi mambo yawe mazuri ili badala ya kukopa machungwa ninunue kapu zima.
 
Back
Top Bottom