Maisha ya mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha ya mtanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by taffu69, Feb 22, 2011.

 1. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Najaribu kufikiria jinsi bei ya bidhaa zinavyopanda kwa kasi ikilinganishwa na kipato halisi cha Mtanzania. Wakati wa siku za mwisho wa juma nilizunguka kwenye maduka ya mtaani kupata mahitaji ya nyumbani lakini nilishtushwa mno kwa bei nilizozikuta; mfano:

  1. sukari shilingi 2,000/kilo
  2. mchele shilingi 1,600/kilo
  3. maharage shilingi 1,900/kilo
  4. nyama shilingi 5,000/kilo
  5. mafuta ya kupikia sh. 4,000/lita
  6. gesi ya kupikia sh. 47,000/mtungi
  7. maji sh. 200/dumu

  Nikiangalia hali hii na kauli za JK wakati wa kampeni za "ARI ZAIDI", "NGUVU ZAIDI" na "KASI ZAIDI" sipati picha ya mustakabali wetu Watanzania.

  Tutaweza kweli kuyamudu maisha ikizingatiwa kwamba mahitaji mengine ya msingi kama matibabu, elimu kwa watoto, umeme na mengineyo bado yanatukabili? Waungwana naomba ushauri katika hili.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Haya tumeyataka wenyewe, tulikuwa na nafasi ya kurekebisha hii tukaamua kuendelea na mfumo huu huu, so kurekebisha ni ngumu tusubiri hadi twenty fifteen. Improvement is impossible without a change!
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Mafuta ya kula eti zakaria anatoa malaysia na mengine huja kwa njia za panya toka zanzibar,wakati malaysia ndio walichukua mbegu ya mawese toka kigoma leo wao ndio tunawategemea kwa mafuta ya kula!huu ni upumbavu,ujinga wetu!tuna mbegu za pamba,alizeti,karanga,makweme,nazi,mawese nategemea bei ingekua chini ya mafuta hapo hapo tuka export
   
 4. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  maji ya uhai lite Tsh 600/-
  petroli lita 1900/-
  umeme wa luku unit ----
  kinachonishangaza,mwaka wa fedha wa Tz ni June/July ila vitu vinapanda from January ,Whyyy???

  serikali inazidi kusinzia ktk masuala ya uchumi na kipato cha watanzania.

  mbinu kubwa kutoka ktk hili nashauri wataaalam wa serikalini waache siasa.
  tupunguze matumizi yasiyo ya lazima.
  tutumie Gas yetu kama source kubwa ya kuendesha mitambo yetu na vyombo vya usafiri kama nchi za malysia,thailand etc.
   
 5. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kibaya zaidi mafuta hayo wanaingiza nchini bila kulipia ushuru wakidai wanaingiza mafuta ghafi wakati mafuta wanayoagiza ni yale yaliyosafishwa na wanachofanya ni kujaza kwenye galoni na ndoo pekee,
   
 6. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nikiskia maandamano ya kumng'oa mkwere na chama chake nitashiriki kikamilifu yaan kwa 100% kwan wao kwa uzembe na kutojali ndo wamechangia haya, na ukiuliza atasema SIJUI
   
 7. Jayfour

  Jayfour Senior Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ugumu niuonao mimi si kuiondoa serikali iliyopo madarakani la!..bali kumpata mtu sahihi anayeaminika ili ajitolee kikamilifu kuwatumikia wananchi ambaye yupo tayari kufa kwa ajili ya waTZ, ndipo waTZ tutakuwa tayari kupoteza maisha kwa ajili yake.
  Ninachokiona sasa kwa hawa wanojiita watetezi wa wanyonge ni kutafuta chance ili kujinufaisha...
  Utakumbuka jk tulimwamini kama mtu ambaye angewaletea unafuu waTZ tukiamini anawajua vilivyo walalao hoi lkn ndiye kiongozi anayeleta ugumu wa maisha kwa kasi ya ajabu.
  Muda utafika..'baada ya dhiki huja faraja'
   
 8. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kauli hii haiwatendei haki watanzania walioamua kumchagua kiongozi wa ukweli lakini kwa ghiliba za walafi wakaamua kuparaganyisha mambo kwa makusudi. watz sasa ni kama tupo msibani tu kila mahali kilio. Ingawa waswahili wanasema 'msiba na nyemi', msiba wetu hauna nyemi katu!!


  Amani yetu inatumiwa vibaya.
   
Loading...