Maisha ya Mtanzania na total lockdown

Maisha ya Mtanzania na total lockdown

Key workers wanakwenda kazini kama kawaida na walimu inabidi waendelee kuwaangalia watoto wa key wokers.
Mashule yalifungwa, walimu na wanafunzi wako majumbani mwao, wapo walioweza kuendelea kusoma kwa online na wapo ambao wamesuasua mpaka sasa.

Hakuna cha mtoto wa key worker, kila mtoto yuko nyumbani kwao, Daycare pia zimefungwa, kila mtu akae na watoto wake nyumbani.

Niliangalia website ya CNN, wakisema kufanya hivyo kumepunguza rate ya maambukizi miongoni mwao. Lakini wengi wanalalamika kukaa nyumbani bila kuambiwa ni kwa muda gani. na wengine wanaomba hospiutali ziwe na day care kwa ajili ya staff wenye watoto wadogo, lakini imeshindikana. Hakuna anayeweza ku ensure safety ya watoto hasa wakati huu, hivyo ikaamuliwa staff mwenye watoto wadogo anaweza kukaa nyumbani na atalipwa.
 
Middle class watamudu total lockdown. Wale wenye uwezo wa kuwa na:
Kilo 10 mchele
“. “. Unga wa mahindi
“. “ unga wa ngano
“. 5. Sukari
Galoni la mafuta ya kupikia

Hii ni 15%ya Watanzania wanamudu maisha haya, wengi wao ni wenye ajira na biashara za za kuzungusha milioni kuendelea.

Kuna vijana wanaishi kwenye chumba. Hawa wametoka vijijini kujaribu maisha mjini. Huwa wana ishi 5-6 katika chumba kimoja. Wana handset moja kila mtu ana SIM card yake. Anaetaka kutumia simu anaingiza sim card.

Hawa wanaratiba ya kununua chakula. Kila mtu na wiki yake. Asubuhi inabidi waamke wakasake vibarua. Ile wiki ya kununua chakula huwezikuweka kitu. Inabidi ununue unga, mboga, mkaa, na mazagazaha kama yote. Upike chakula ule na wenzako.

Usipokuwa kwenye zamu ya chakula ndiyo unaweka pesa. Lengo ni kupata mtaji wa kusimama. Ukishasimama unaondoka mwingine anapigiwa simu kijijini aje mjini.

Hawa utawakuta sehemu kama Mahakama ya ndizi, wanashusha mizigo ya mazao na kupakia mizigo iliyonunuliwa kwenye magari ya wateja.

Kuna wajane, walikopa mikopo kwenye vikoba sasa wanapika mama ntilie, maandazi na chapati. Kila wiki kuna hela ya kurudisha kwenye vikoba, kodi ya nyumba na chakula cha watoto.

Kuna Wauza baa nao wanatakiwa kulipa kodi.

Kwa Umasikini wangu wa Kutukuka nilionao GENTAMYCINE kama hii ' Lockdown ' yenu itatangazwa na kuanza rasmi nchini Tanzania naomba nichukue nafasi hii ya mapema kabisa kuwakaribisheni nyote katika Mazishi yangu kwani najua hiyo ndiyo itakuwa ' Tiketi ' yangu muhimu ya Kuniachanisha hasa na hii dunia. Hapa tu ' Lockdown ' haijatangazwa ' cha moto ' nakiona huku shida zikinijaa hadi katika Kope zangu za Macho sasa ikitangazwa si ndiyo itakuwa balaa kabisa? Ewe Mwenyezi Mungu tusaidie Baba!
 
Kwa Umasikini wangu wa Kutukuka nilionao GENTAMYCINE kama hii ' Lockdown ' yenu itatangazwa na kuanza rasmi nchini Tanzania naomba nichukue nafasi hii ya mapema kabisa kuwakaribisheni nyote katika Mazishi yangu kwani najua hiyo ndiyo itakuwa ' Tiketi ' yangu muhimu ya Kuniachanisha hasa na hii dunia. Hapa tu ' Lockdown ' haijatangazwa ' cha moto ' nakiona huku shida zikinijaa hadi katika Kope zangu za Macho sasa ikitangazwa si ndiyo itakuwa balaa kabisa? Ewe Mwenyezi Mungu tusaidie Baba!
Wewe mzee kumbe upo hai

Kuna mahali fulani hapa Kigali nilidanganya nimeagizwa na wewe kazi fulani fulani basi wakanipokea na kunihudumia kwa bashasha sana
 
Wewe mzee kumbe upo hai

Kuna mahali fulani hapa Kigali nilidanganya nimeagizwa na wewe kazi fulani fulani basi wakanipokea na kunihudumia kwa bashasha sana

COVID-19 imeshakuingia hadi ' Ubongoni ' mwako ndiyo maana una ' Popomika ' hivi au?
 
Huku kwetu itakuwa ni mateso kusema kweli.
 
Eee MUNGU wa Abraham,Isaya na Yakobo.Ambaye Ndiwe MUNGU Huyo Huyo Uliye Ndiye MUNGU wa T.B.JOSHUA.,"Utuhurumie",Gonjwa Hili 'Corona' lisiitese kwa Sana TANZANIA.Maana ndio ahadi YAKO kwetu kwa neno lako Zaburi 91:10 KWAMBA,Mabaya hayatatupata sisi,Wala tauni haitaikaribia hema(nyumba )zetu.Na iwe hivyo kwa Gonjwa Hili la COVID-19.Have mercy oh Lord.In JESUS CHRIST NAME We pray .AMEN.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Total lockdown kwa mbongo haiwezekani,mnataka matatizo bureee
 
Hapa sasa ndo utataman kijijin kwa bibi, sasahivi.. mpunga,viazi,mahindi,kunde na karanga za kumwaga,yaan lock dowb hata miezi sita tunakula tu vyakula asili na maziwa.karibu kijijin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom