Maisha ya Mtanzania na total lockdown

Maisha ya Mtanzania na total lockdown

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,349
Middle class watamudu total lockdown. Wale wenye uwezo wa kuwa na:
Kilo 10 mchele
“. “. Unga wa mahindi
“. “ unga wa ngano
“. 5. Sukari
Galoni la mafuta ya kupikia

Hii ni 15%ya Watanzania wanamudu maisha haya, wengi wao ni wenye ajira na biashara za za kuzungusha milioni kuendelea.

Kuna vijana wanaishi kwenye chumba. Hawa wametoka vijijini kujaribu maisha mjini. Huwa wana ishi 5-6 katika chumba kimoja. Wana handset moja kila mtu ana SIM card yake. Anaetaka kutumia simu anaingiza sim card.

Hawa wanaratiba ya kununua chakula. Kila mtu na wiki yake. Asubuhi inabidi waamke wakasake vibarua. Ile wiki ya kununua chakula huwezikuweka kitu. Inabidi ununue unga, mboga, mkaa, na mazagazaha kama yote. Upike chakula ule na wenzako.

Usipokuwa kwenye zamu ya chakula ndiyo unaweka pesa. Lengo ni kupata mtaji wa kusimama. Ukishasimama unaondoka mwingine anapigiwa simu kijijini aje mjini.

Hawa utawakuta sehemu kama Mahakama ya ndizi, wanashusha mizigo ya mazao na kupakia mizigo iliyonunuliwa kwenye magari ya wateja.

Kuna wajane, walikopa mikopo kwenye vikoba sasa wanapika mama ntilie, maandazi na chapati. Kila wiki kuna hela ya kurudisha kwenye vikoba, kodi ya nyumba na chakula cha watoto.

Kuna Wauza baa nao wanatakiwa kulipa kodi.
 
Ikumbukwe itakua tu hapo dar

god is good
 
Shughuli kwa wauza bar na wale wa mpango wa kando biashara sasa imeingia shubiri kila mtu yupo kwa lockdown
 
Matajiri hua hawawazii msosi
EI18xZUWoAAEgTP.jpg
 
Hata huko waliko issue lockdown, walisema siyo Mandatory, ni kama unaweza ili kupunguza kusambaa kwa maambukizi.
 
Kwan ikitokea vita itakuwaje? Kuna wakati sisi kujadili tena itakuwa ni lazma kama hali itaendelea hivi sure ni ngumu ila ikidibi tutafanyaje sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lockdown haiwezekani kabisa kwani biashara nyingi zitafungwa na biashara zitakazosalia ni za chakula tu
Fikiria ni % ngapi inayotegemea kufanyakazi ili ale kwa siku?
Tofauti na wauzaji wa chakula na bidhaa za aina hiyo
Hizo zingine zinaajiri mamilion ya watu na wote wakae nyumbani haiwezekani

Lockdown ya Zimbabwe siku ya kwanza tu watu wametoka na madumu matupu ya maji na kuanza kutoka nje police wameamua kuwapanga wenyewe chezea njaa wewe


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Hata huko waliko issue lockdown, walisema siyo Mandatory, ni kama unaweza ili kupunguza kusambaa kwa maambukizi.
Key workers wanakwenda kazini kama kawaida na walimu inabidi waendelee kuwaangalia watoto wa key wokers.
 
Back
Top Bottom