Maisha ya mkulima yanaweza kuboreshwa zaidi.

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Nilisoma habari ya mwanaume wa kizungu alizaliwa mwaka 1920. Alieleza kuwa walizaliwa watoto 10 na wote walikua na kupata miji yao. Baba na mama walikua wakulima. Nyumba yao ilikua mbele ya shamba lao. Shambani walifuga nguruwe, ng’ombe na kuku. Walilima nyanya, caroti, vitunguu, kabeji na viazi mbatata.

Asubuhi kabla ya kwenda shule walipewa majukumu, watoto wa kike walimsaidia mama kusafisha nyumba na kutengeneza chai. Wakiume walisafisha mabanda ya mifugo, kukamua maziwa na kuokota mayai na kuwapa wanyama chakula.

Anasema mahitaji yaliyotoka dukani ni sabuni, mafuta ya kula, dawa ya meno, sukari, chumvi, mchele na unga wa ngano. Mikate iliokwa nyumbani, mayai, maziwa na nyama vilipatikana kutoka kwenye mifugo.

Tafakari niliyokuwa nayo, kwa ardhi yetu tuliyonayo, ni kitu gani kinawashinda wakulima wetu wengi kuishi maisha waliyoishi wazungu miaka 80 iliyopita? Tufanye nini kuboresha maisha yetu?
 
Mitano tena
JamiiForums475678377.jpg
 
Back
Top Bottom