Maisha ya kijijini ni rahisi kuliko ya mjini ?

Maisha ya kijijini ni rahisi kuliko ya mjini ?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
65,296
Reaction score
112,117
Kwa nini kuna watu wengi hufikiri maisha ya kijijini ni rahisi zaidi kuliko ya mijini ?
Screenshot_20261113-221534~2.jpg
 
Kwa nchi za Africa hakuna anayependa kukaa vijijin ni shida tu, coz huduma za kijamii bado duni sana ukifananisha na nchi za wezetu zilizo endelea .
 
Nimekaa vijijini hizo distractions & financial pressures zipo sana!

Ukitaka ujue nenda misimu ya kupanda na kuvuna, na muda watu wanapeleka mifugo minadani.

Watu wanakopa sana.

Social life sio nzuri. Binti wa form 2 anatiwa mimba watu wanachekelea. Kutwa kuwaza uchawi, majirani hawaongei wakihisi wanalogana. Hii inaleta unafki mkubwa na umbeya.
 
Kwa nini kuna watu wengi hufikiri maisha ya kijijini ni rahisi zaidi kuliko ya mijini ?
View attachment 3709602
Maisha ya kijijini ni mepesi kama unawaza kula na kulala, ila kama unataka kupiga pesa maisha ya kijijini ni magumu sana, hakuna mzunguko wa pesa , nyumba moja ukutane na nyumba nyingine ni kipengele, unaweza ukatembea kilomita za kutosha bila kuonana na mtu hata mmoja.
 
Maisha yameishakuwa changanyikeni siku hizi hakuna cha kijijini wala mjini, yote yanataka hela tu. Misosi inayoliwa mjini ndiyo hiyohiyo inaliwa kijijini. Umeme, maji mwendo ni uleule
 
Zamani gharama za maisha ya kijijini na mjini zilitofautiana ila siku hizi ziko sawa, bajeti ya kuishi mjini ndiyo hiyohiyo ya kuishi kijijini, hata uende mashambani mwendo ni huohuo. Nyumba za mjini ndio hizohizo za kijijini, tembe, nyasi zimeishatoweka vijijini, nyumba ni kama za mijini tu, umeme upo kijijini, tena mpaka vitongojini, hata utake kuishi maisha ya kijima porini hutaweza kama ume adapt maisha ya mjini
 
Back
Top Bottom