Maisha ya Familia na Crisis ya Beki 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha ya Familia na Crisis ya Beki 3

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sumba-Wanga, Mar 13, 2012.

 1. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  wanajamvi wenzangu,

  Habari za jioni.

  Kumekuwa na shida sana ya kupata na kuishi na hawa beki 3. Ni muhimu sana kwa maisha ya familia.

  Familia yangu inahangaika sana. watoto bado wadogo, maisha magumu lazima tufanye kazi ili kuweza kusukuma gurudumu mbele.

  Kama hiyo haitoshi, beki 3 wa siku hizi wamekuwa hatari sana, wengine wanawafanyia watoto mambo mabaya sana, wengine ni wachawi, mradi ni shida na mkanganyiko kwenye maisha ya familia. wazazi tunahangaika, watoto wanatabika. kazini hakukaliki, basi ni shida tupu.

  Wenzetu, unafanyaje?
  Mnapataje hawa beki 3?
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  toka kuanzishwa kwa shule za kata
  huwezi pata housegirl kama zamani.....

  unless uwe tayari kuwalipa better ....na sasa mshahara wao nasikia unaanzia elfu sitini....
  ukitaka fanya kama wahindi wa city centre dar...
  wanawalipa vizuri but hawalali majumbani
  wanakuja na kuondoka na jumapili hawaji......na ukiwataka
  unamuuliza housegirl yeyote wa wahindi city centre atakuletea.....
   
 3. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ni rahisi kuwapata, but kuwapata ambao hawatakuwa na tabia ulizoorodhesha hapo juu ni kazi kweli kweli. Labda cha kukushauri, tafuta mtu unayemfahamu if possible toka kijijini kwako/mkeo, be careful na tabia zake na ikibidi mchukue akiwa na akili zake timamu. Mimi nilimchukua aliyezalishwa na kutelekezwa. Anajua machungu ya maisha na pia anajua kulea watoto, im happy.
   
 4. Reserved

  Reserved Content Manager Staff Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 750
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duh siku hizi ni balaa mkuu
  Wasichana wameerevuka hata kule ambako kulikuwa wanasema wanapatikana imekuwa issue sana
  Shule za kata nazo zinawaondoa kwenye ufanyakazi wa nyumbani na kwenda kusoma
  hawataki tena kufanya kazi za nyumbani
  Ni balaa sana kwa sasa
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  siku hizi taabu tupu,
  hata uwape nini hawaridhiki...
  Tena wengine wanafanya mambo ya ajabu ukisikia unabaki mdomo wazi?

  Ila wapo wachache wametulia....

  Lakini kama mama ni makini...
  Yupo karibu na watoto
  anasimamia nyumba kwa hali ya juu...
  Kidogo inasaidia......

  Na usiombe upate hg mwenye agenda mbili mbili......
  Lazima amtege faza house.......................
   
 6. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu umesema kweli, kuwapa msharaha kama huo sio shida, mradi afanye kazi.

  Ukipata bek 3 wa kuja na kwenda, kazi ni kwa watoto wanaokwenda shule mapema sana asubuhi: mwa mtaji huo Beki 3 lazima alale hapo hapo, Maanaa baba na mama wanaondoka saa 11 asubuhi!

  Life is very challenging!
   
 7. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni kweli, lakini wakati mwingine aliyezalishwa na kutelekezwa huwa ana wasi wasi na mwanae muda wote na anaweza asitulie. Nilishakuw anaye mmoja, kila siku simu kutoka Kijijini.
  Mkuu, hata hivyo, kama ukipata kama huyo please ni pm
  Familia yangu iko at the cross road.
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kwa maana nyingine ni maendeleo kwa wao wenyewe na familia zao, ingawa tuna suffer.
  Hata hivyo, ni kuwaombea kila la heri.
   
 9. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135  This is the worse party of it....we have to live with it, hakuna jinsi, tunawahitaji sana.
   
 10. d

  dav22 JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  du aisee....
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  ngoja nikupe kaeksipiensi kangu kidogo.

  Unapoletafuta au kuletewa beki 3, mfanyie intavyuu hata kama ya sekunde 2.

  Usichukue aliyezaa na kumwacha mtoto kwao hasa kama watoto wako ni wadogo, ni ngumu sana yeye kuwapenda.

  Mtu aliyekubuhu kwenye uzinzi si mzuri, anaweza acha watoto ndani na kwenda kupigwa kizizi. Anaweza hata lala huko huko.

  Mlipe hela ambayo ataridhika, kama unaweza kuvuka kidogo expectation zake inasaidia.

  Mpe uhuru usiodhuru familia, sio kila saa unamfuata mgongoni. Usitake 'perfection' coz no one is that perfect.

  Mpe muda wa kujifunza na kuelewa rules za familia.

  Mie wangu nimekaa naye miaka 4, wala hana hata dalili za kufikiria kuondoka. Ni mie mwenyewe kanichosha maana hataki ku-grow kikazi lol
   
Loading...