Maisha ya depo

Wadogo zangu wote hawajaenda Kwa mujibu tulikataa na wanangu hawataenda,mateso matupu
Wa kiume ungewaacha waende. Kuna Cha kujifunza. Wa kike naunga mkono maana mateso yakizidi wengi wanagawa Ili yapungue. Tuliwaambia madawili wetu tupo tayari kuteseka kwa ajili yao ikiwa watawakataa maana sana sana hawezi kukupa adhabu peke yako anagawa kwa kombania au platoon au kibangala.
Tulikubaliana lengo letu ni kwenda chuo na sio ukimwi ila Kuna waliogawa kwa Raha zao. Mwisho tunapimwa HIV waliongezeka tofauti na tulivyopimwa mwanzoni. Maana hairuhusiwi mgonjwa kushiriki mazoezi.
 
Aseehh..inaumiza mnooo...ni WA kike watupu Kwa kweli jeshi ni mtihani mtupu
 
Kwa iyo mwishoni wenye ngoma walikua wengi
 

MAISHA YA DEPO

SEASON-3

EPISODE 18


Baada ya utambulisho wa ma-SIR MEJA walifuata ma-ODARI KOPLO wakaja makamanda akina Mochiwa, Kalaghe na wengineo mwisho wakamalizikia makarani na mwisho japo si kwa muhimu ila ni muhimu tukatambulishwa ma-ST ambapo muundo ulikamilika kwa mfumo huo.

“Haya makamanda wangu mnaweza kwenda kukaa nafikiri wamekwishawaona” Matroni aliwaruhusu viongozi hao walioko mbele kutawanyika.

“Eeh yote kwa yote nafikiri tumemaliza maana naona mmenuna KURUTA zisije laana zenu zikanushukia hapahapa nilipo maana kusema kweli DOSO jumlisha njaa duu siyo poa Mungu awape ahueni kwa kweli”.

“Baba paroko nakumbuka nilikukatisha nikakwambia nitakupa nafasi mwishoni sasa nafasi yenyewe ni hii ila wakati huu unaipata kwa masharti yaani utakachoongea kiwe kifupi mno”.

“Sawa mkuu huohuo muda mfupi unanitosha sana” alijibu LUTENI Novath.

“Sasa afande nawaona kabisa hawa watu wa Mungu wamenuna sasa ombi langu ni kuwa kabla hawajaenda kula nataka watabasamu ili wakila wale wakiwa na furaha kwenye nyuso zao”.

“Sawa mkuu”
“Utaweza?”
“Hata usijali mkuu”
“Bwana usijekuongea muda mrefu ujue utawakera hawa binadamu”
“Hata usiwaze nakuhakikishia Bosi wangu”.

“Sawa hakuna shida mwanzo niliwaona KOMBANIA nakumbuka mlicheka sana meno thelathini na mbili yote yalikuwa nje sasa nina uhakika nimechagua mtu sahihi naomba kwa dakika chache watu hawa nao nione meno yao angalau kumi yakiwa nje”.

“Anhaah sawa afande asante sana kwa kunipa fursa hii namuomba yule KURUTA St wa kiume Danger COY aje mbele” baba paroko aliniita nami bila kuchelewa nikadabo pale alipo.

Nilipofika afande alilielezea tukio alilosimuliwa na afande Kalaghe tukiwa KOMBANIA nakumbuka uwanja mzima uliripuka kwa vicheko vilivyochukua muda kukoma.

“KURUTA wiih”
“Waah”
“Wiih”
“Waah”
“Ewaah”
“Ewiih” Matroni ilibidi awakatishe kutoka kwenye vicheko vile.

“Uzuri mhusika mwenyewe tuko naye hapa ngoja tumsikilize hujambo KURUTA”.

“Sijambo”
“Enheeh unajisikiaje kwa sasa?”
“Najisikia vizuri tuu”
“ mwanzo ulikuwa unajisikiaje?”
“Aah hali haikuwa nzuri afande”
“Kwanini?”
“Nilikuwa naona mapichapicha tu usoni”
“Mapicha gani hayo tuambie”.

“Kusema kweli afande kuna muda nilikuwa namuona Israeli anapita mbele yangu sijakaa vizuri naona kama jeneza linapita usoni mwangu halafu waliolibeba siwaoni mara kuna kipindi naona watu wanachimba kaburi yaani yalikuwa ni mauzauza matupu” bwana wee watu waliangua vicheko siyo poa.

“Daah hii kali unaitwa nani KURUTA” aliniuliza jina langu Matroni Neema nami nikamtajia.

“Anhaah jina siyo geni wewe sio yule rafiki yake na KOPLO wa dukani aliyekuita pale KOMBANIA usiku”“Ndiyo mimi afande”.

“Aaah we dogo wewe sawa bwana asante kwa kutuvunja mbavu mana nilitegemea meno angalau kumi ila kusema ukweli nimeyaona meno yoote thelathini na nje mbili haya bana rudi kwa wenzako KURUTA”.

“KURUTA wiih”
“Waah”
“Ewaah”
“Ewiih”
“Kwanza tukushukuru baba paroko na KURUTA pale ama kweli hatukukosea kuwachagua mmeupiga mwingi ni kama watu wanataka kuhamia Danger COY vile itoshe kusema watu wa DANGER mmebarikiwa sana”.

“Wakaribie tu tutawapokea kwa ukarimu maana hata maandiko yameibariki nyumba yenye kupokea wageni” alidakia LUTENI Nova.

“Asante sana mtumishi, sikia kutoka kwangu KURUTA”
“Niwape poole kwa yoote mliyokumbana nayo siku ya leo japo bado haijakamilika ila kuna kitu cha muhimu mno kukazia kabla sijawaruhusu mkamsalimie MZABUNI japo najua muda umeenda ila mnipe sekunde chache tu mtanishukuru”.

“Jambo la kwanza kukazia ni kuwa hiki mlichokutana nacho leo ni sehemu ya kile mtakachokutana nacho siku arobaini na mbili za wiki sita hivyo mjiandae kiakili na kisaikolojia hilo la kwanza”.

“Jambo la mwisho niliwapa kazi makamanda wangu ya kuwatambulisha maeneo ya kikosi na nina uhakika wamefanya hivyo sasa sina shaka waliwaonesha hayo maeneo kuwasisitiza kutofika bila ruhusa yao”.

“Sasa kwa kukazia ni kwamba si maeneo hayo tu mliyotambulishwa bali hata yale msiyotambulishwa hamtakiwi vilevile na isije ikatokea ukaenda ukiwa peke yako ama bila ya ruhusu ya kamanda wako hili ni onyo na mimi nawapatia”.

“Zingatieni hili na mwisho kabisa niwapongeze kwa awamu nyingine kwa hatua hii mliyofikia mwisho wa yote hakuna la ziada niwaruhusu mtawanyike kwenda kwenye chakula tukutane tena KOMBANIA baada ya mlo na niwatakie mlo mwema.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Huu ni mwisho🔚 wa msimu wa tatu wa simulizi ya MAISHA YA DEPO.

Oya doja la doso Aiylan wasalan na ndugu yangu zee la masongi kabwela wa kutupa Poor boy bila kuusahau mdomo wa mafulusi moneytalk na swahiba wangu MombaDier njooni tumalizie hii halafu tukutane msimu ujao 🔚.

🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜

🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜🔜
 
Kwa jinsi unavosimulia kupitia location mbalimbali hii ,inaonesha moja kwa moja ni 838KJ
Swahiba yangu Toofast tumekamilisha utambulisho wa camp vipi kwa ukiangalia maeneo yaliyotambulishwa bado unasimamia hiki ulichokisema? 😊
 
Asante mkuu kwa burudani
Vipi tuutarajie lini tena muendelezo wake
 
One love mwanangu
 
HEY kichekesho cha kambi, asante kwa burudani kaliii,, nasubiri nione msimu unaishaje, je kuna watu wanashuka daraja au wote mnatobo!!!!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…