Mi sijataja kilimo.
Nimezungumzia fulsa za kuanza nazo bila mtaji Mkubwa
Kuna kuvuna Asali bure msituni na kuiuza.
Kuna kufanya uvuvi hasa kwenye vyanzo vya maji kama Mito, Maziwa nk.
Kuna kuuza mkaa, miti ipo ya Bure.
Kuna uwindaji wanyama Nk.
Kilimo, kuna baadhi ya maeneo Yana mvua za kutosha na hayahitaji mbolea za kununua kukuzia mazao.
Mfano maeneo ya, Idodoma, Itipi, Malolo, Nziha, Kilosa na Ifakara Mkoa wa Morogoro
Kuhusu kuvuna asali siwezi kuzungumzia maana sijui lolote,ila hayo mengine yaliyobaki yanahitaji mtaji,tena mtaji wa uhakika maana unaweza usipate matokeo kwa wakati na mda mwingine hasara kabisa
Kama wewe ni kijana, huna connection wala muelekeo wowote rasmi wa maisha, Dar ndio the best place pakukimbilia. Ramani zote za kimaisha zinaanzia Dar au kuishia Dar. Liwe jua iwe mvua, Dar huwezi kukosa chochote.
Mkuu nimefika Dar mwaka jana mwishoni! Ukweli usemwe, hapa sitoki, nastaafia hapa hapa hata iweje! Dar fursa kibao ni wewe tu!! Nilikuwaga sijui kama Dar wanafakamia hivyo kuku wa kisasa! Niikuwaga sijui kama nyama ya ng'ombe Dar inauzwa 10k kwa kilo tena ile ya daraja la chini kabisa!!