Maisha ya connection yanatutesa vijana.

Hutendei haki hii kuwa reply tu. Embu post kwenye thread yake kabisa.
 
Sasa mkuu kutongoza demu Kuna uhusiano gani na interview ya kazi.
Kama wako fair wangekupa tu kazi,shuleni ndio kosa kutongozana lkn uraiani au kazini sio kosa kumtongoza mtu.
Blaza kazi nilikosa halafu wakaja kulirudia tangazo tena nikapotezea sikuomba ila sasa hivi nakula kuku kwa mrija maisha juu ya mstari
 
.
Kila mmoja ana experience yake katika kuhustle, kashapitia yote hayo uliyoyasema na maana katambua kilichomkwamisha yeye ni connection. Hivi unajua kwamba hata katika usaili ule wa mwaka Jana/juzi wa TRA kuna watu walikua wana ile screening test kabla ya usaili.
La msingi ni kumuambia azidi kupambana this is the jungle and not ridiculing him/ her.
 
Seem nyingi bila conection hutoboi, mwaka huu kunakaz zilitangazwa mahali nilikua lile eneo, watu wakatuma maombi weee, kumbe hata kabla ya deadline interview ikafanyika kimya kimya hapo ndo nilichoka, yaani lile tangazo lilikua bosheni tu, pata picha interview imefanyika kimya kimya kabla hata ya deadline ya tangazo siku tatu kabla, madogo wakawa wanaendelea kupeleka maombi wahusika wanawachora tu, kunadada alitoka mwanza kufika kuambiwa interview ilishafanyika hata kabla ya deadline kidogo azimie

Nakuna dogo hakuitwa interviw flan mwez wa 4 hakua na vyeti HR alimtimua sijui simu ilipigwa toka wapi dogo akaitwa, dogo alikuja kavaa iv vijinsi vya kubana na kobazi za kuogea kama kwake vile, akagonga interview bila hata vyeti na yupo mzigoni, ndo nikajua bongo bila connection ni msoto mkubwa, tena kwa awamu hii vinafasi vya ajira vinavyokua kiduchu ndo vimeongeza huu urasimu
 
Yes wewe ndio umeongea point.
Kupata kazi mtu mmoja kirahisi haiwezi kuwa reference kwa watu laki saba waliokosa kazi na wapo mtaani.
Kuna watu wengi wamejawa na maswali kichwani kwamba zile interviews za serikalini unatakiwa ufaulu kwa kiwango gani ili upewe kazi.
Maana mtu unafanya interview maswali yote unayapiga kwa uhakika na confidence kabisa halaf mwisho wa siku kimya tu.
 
Pole sana mkuu.
Hicho ndicho anachokiongelea mtoa mada ila Kuna viazi hawaelewi kwa sababu waliitwa na kupewa ofisi kichwani maji matupu.
 
Mmeona ushuhuda huu wadau.
Halaf wale mbulula wataendelea kubisha tu ili mradi aonekane kucomment.
 
Wapo fasta kuweka kufuli kwenye biashara za watu.. Kweli wahenga walikuwa sahihi kusema mwenye shibe amjui mwenye njaa.
 
Mkuu hizo categories zote za kiubaguzi zipo wala usikatae.
Kwa mfano watoto wanaoishi masaki au mbezi beach automatically anakuwa na connections nyingi ukilinganisha na watoto wa tandika, gongolamboto,tandale hata Kama wote ni wa kabila moja.
Nadhani haujaelewana. Racism maana yake ni ubaguzi unaohusisha rangi baaaaasi si vinginevyo.

Kuna nepotism, huu ni ubaguzi kwa misingi ya kiundugu nadhani ndilo neno ulitakiwa utumie.

Zipo nyingi sana so kabla haujatumia neno jaribu kujifunza ukajua maana yake.....
 
Went wanasema vyeti sio ishu hata kuchongesha wachongesha,Suala ni NANI ANAKUJUA
 
Sasa racism inaingiaje wakati wote tunaochangia hii mada ni waswahili.
Mimi nilihisi yeye aliyetumia Hilo neno amechanganya ndio maana nikajiongeza na si kwamba sijui maana ya hilo neno.
 
Bila connection hata tangazo la ajira unaweza usilione wala kulisikia.
Kumbuka sio vijana wote wanamiliki smartphone au pc
 
Wapo fasta kuweka kufuli kwenye biashara za watu.. Kweli wahenga walikuwa sahihi kusema mwenye shibe amjui mwenye njaa.
Ndio hivyo nawashangaaga sana.
Wanafikiri kuwa msomi ni kuongea kiswanglish wakati kichwani ni empty.
 
Kwahiyo hapo kwenye kuzungukwa na masikini unamshauri nini huyo mlalamikaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…