Maisha ya chuo na baada ya kumaliza chuo

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Wakati niko chuo nilikuwa nawaza tu kwamba punde nikimaliza tu naenda kushika hela kitaani. Tena nilikuwa naulizia na mshahara kabisa na kuupangia bajeti kabla ata sijamaliza.

Starehe nyingi za chuo asa kuwa na watoto wakali ilifanya nisahau kama kuna shida maisha baada ya chuo.

Wasichana kila sehemu ukigusa tu imo unajichukulia mtoto mkali sana sana boom likitoka we unajivutia tu kiroho safi.

Kiukweli maisha ya chuo matamu sana ukiondoa sup na vitest vya kudundisha moyo ila baada ya hapo kuja kitaa nikajua kwamba maisha siyo ndoto ukiota basi unapatia ila ni msoto mkali.

Yale mawazo ya chuo yanabaki kuwa mawazo tu lakini hayana ukweli ndani yake. Alafu ukimaliza chuo ata kama haujatusua ndugu wanajua na wana kufanya tegemeo lao. Kiukweli maisha baada ya chuo yanaitaji akili nyingi zaidi ya mitihani au sup za chuo.

Vipi kwako maisha ya chuo na baada ya apo yapoje.
 
Kipindi namaliza chuo niliajiriwa january mwaka 2014 sijawahi kaa nyumbani kivile ila sasa nakula bata sana sijui kama nitajenga aisehh maana kushika 800k kwa mwezi sijawahi kufikiria

ila acha nifikishe 30 hivi ndo ntatulia maana mapenzi yenyewe nimeyajua nikiwa na miaka 25 acha niendelee kukua
 
Binafsi najutia kuponda raha chuoni na pesa ya boom... maybe ningejibanabana kwa sasa ningekuwa hata na boda boda nakula vichwa kitaani...... ila mpaka sasa life la kitaa limenipiga fimbo si mchezo mavyeti nimeyafungia ndani....

Labda niwakumbushe vijana wenzangu mlioko chuo mkumbuke ku balance hilo boom life la kitaa ni zaidi ya chuo kikuu asikwambie mtu..... Yaani inshort ukija kitaa unaanza upya... maisha ya huku hayana ubishoo wa chuo...:(:(:(:(
 
Vip mkuu ulikuwa na daraja siyo bure
 
We acha tu alafu boom linapenda simu Kali na Laptop za mauzo .
 
Bandiko lako limesheni ukweli na uhalisia wa maisha baada ya chuo, Ni fundisho tosha kwa vijana.
 
Back
Top Bottom