Maisha ya Boarding enzi zile

Maisha ya Boarding enzi zile

kombaME

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
2,115
Reaction score
2,819
Wakuu wazima,

Maisha yanatembea kwa spidi sana, enzi hizo boarding schools zilikuwa ni sehemu ya mafunzo ya maisha mtaani, yaani ukipiga miaka minne boarding basi tayari una cheti cha kupambana popote dunian na kukabili maisha yoyote, ilikuwa si mchezo, jinsi ya kupata msosi ni noma, ukienda kwenye kulala nako si mchezo, walimu sasa wa shule za boarding enzi hizo walikuwa wanajua kulea na kunyoosha hasa, hata uwe mtukutu vipi ukipelekwa boarding unanyooka, wazazi wenye watoto watukutu boarding ndo ilikuwa tegemeo Lao.

Nakumbuka form one enzi zile ilibaki kidogo tu nikusanye virago nirudi home maana ni km Guantanamo hivi shuruba zake, kila kitu tabu tupu yaani..

Tukumbushane visa ulivyofanyiwa au kuwafanyia wenzako enzi ukiwa boarding .

Twende pamoja tukikumbushana lile life la jeshi ukiwa boarding.
 
Tulikuwa tunaamshwa saa 10 kwenda mchakamchaka na viboko juu, aisee yale maisha sitayasahau.
 
Nakumbuka mwl m1 alituambiaga definition ya maisha ya boarding:

Maisha ya boarding ni mjumuiko na mkusanyiko wa shida na tabu na chembechembe ndogo sana za raha.

R.I.P mwl mtanzania ( hiyo ndio nickname yake )
 
Ni shule gani mkuu?
 
Maisha ya "nyakato secondary", bukoba ni moja kati ya naisha ya boarding ambayo sitokuja kuyasahau. Namukumbuka yule teacher aliyekuwa akisema hii ni JKT siteti namba moja duh!
 
Nakumbuka kipindi tupo form 1 boarding (shule fulani porini kule, baridi kama URUSI full kukopa kuoga miezo mpaka tukirudi uraiani),

DOMITORY letu lilikua na ma Proffessor wa wizi, lilikua linajulikana kama Dom La Maangamizi. Kuanzia Form 2 mpaka Form 6 walikua wanalitambua varangati letu, likikatiza mitaa yao wameumia. Hata kama umesahau sabuni iliobakia kama kipande cha karanga au umesahau soxi moja iliotoboka kama chujio hauikuti.

Tulikua ma bingwa wa kuiba mpaka MAANDAZI yaliokua kwenye karai la mafuta ya moto kwa mkono bila kisaidizi chochote, na kuvunja madirisha ya jikoni kuiba chakula hata kama hakijaiva vizuri.

Mwisho ilibidi uongozi wa chuo watuletee viongozi wa dini kutufanyia maombi maalum Form 1. (aliepitia maombi haya anicheki PM, tukumbushane varangati letu kwenye hio shule).

Ila kuna mwalimu alikua anaitwa Mr Michael Mkanda a.k.a Mr Izraeli Mtoa Roho, alikua siku akila ganja/konyagi zake anagawa dozi kama hana uzazi dadeki. (Aliekuwemo na asiekuemo mtasimulia). Ila siku tunafunga shule alikua halali tunavorusha mawe juu ya bati/madirisha yake.
 
Mimi nikiwa olevel Mkuu secondary Rombo
Advance Form five walipokuwa wakija
Mimi nilikuwa kiongozi wajikoni
Siku ya wali wapishi walikuwa wananihifadhia ndoo zangu mbili
Za wali
Saa tano usiku nauza saa mia mbili kwa advance hapo nikiwa form three
 
Maisha ya "nyakato secondary", bukoba ni moja kati ya naisha ya boarding ambayo sitokuja kuyasahau. Namukumbuka yule teacher aliyekuwa akisema hii ni JKT siteti namba moja duh!
Nimepita pale 2012 nilikua Ruhinda bweni la mwisho kabisa kuelekea pyramid....asee asikwambie mtu ile n JKT mchaka mchaka kwenda bugashani,BLTC bado issue ya kulima,ukienda kuangalia mpira nje ya shule jiandae kula nyama zilizoganda...Nyakato mama
 
Nimepitia coment zote bado sijaona mlioteseka,wengi wenu mmeingia shule za bweni mkiwa sekondari na sisi tuliosoma Tosamaganga iringa kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari tuseme nini?
 
Hawalimi tena na kupangiwa zamu za kuhudumia banda la nguruwe?? Kwenda ulokoni na kuangalia mpira kwa mzee katemana....Kuna kipind linapita gharika la ukaguzi wa simu asee hata kama una SIM card inakula kwako
 
i
Toka ilipo jengwa upya nilijalibu kuwa ulizia Madogo wakadai kulima ni kama sehemu ya adhabu . Nakumbuka kipindi bado nasoma pale kulikuwa na laia wanajiita special duty .

Kazi yao ilikuwa ni kuudumia nguluwe (shambani hawaendi, hawafanyi usafi, hawasombi maji ya jikoni na Nazi nyinginezo) .

Ulokoni ilikuwa ni kawaida ,lakini ukikamatwa ilikuwa ni hatari.

Kuhusu mpira kulikuwa na TV mbili( ya DH ilikuwa inatumia AZAM TV- hii ilikuwa ni ya wote kifurushi chake kilikuwa kinalipiwa na shule ,sifahamu kwa saizi utalatibu ukoje .

Na yawadau hii ilikuwa ni maalumu kwa mpila, kifurushi chake kilikuwa kinalipiwa na wanafunzi -wadau wa mpila)

kuhusu simu , magharika yalikuwa ni kawaida . Msimu wa saspensheni ulikuwa mwezi wa
7&8 hii ilikuwa inawahusu zaidi form6 ili kuwa tishia form5, nakumbuka kuna jamaa aliingi shuleni usiku wakati was kufungua likizo ya mwezi wa 7 ,aka kamatwa na simu usiku huohuo. Akalazwa administration ,asubuhi aka ludi nyumbani.
 
Wakuu wazima,

Maisha yanatembea kwa spidi sana, enzi hizo boarding schools zilikuwa ni sehemu ya mafunzo ya maisha mtaani, yaani ukipiga miaka minne boarding basi tayari una cheti cha kupambana popote dunian na kukabili maisha yoyote, ilikuwa si mchezo, jinsi ya kupata msosi ni noma, ukienda kwenye kulala nako si mchezo, walimu sasa wa shule za boarding enzi hizo walikuwa wanajua kulea na kunyoosha hasa, hata uwe mtukutu vipi ukipelekwa boarding unanyooka, wazazi wenye watoto watukutu boarding ndo ilikuwa tegemeo Lao.

Nakumbuka form one enzi zile ilibaki kidogo tu nikusanye virago nirudi home maana ni km Guantanamo hivi shuruba zake, kila kitu tabu tupu yaani..

Tukumbushane visa ulivyofanyiwa au kuwafanyia wenzako enzi ukiwa boarding .

Twende pamoja tukikumbushana lile life la jeshi ukiwa boarding.
Umenikumbusha nilisoma Shule moja ya jeshi baada ya brother kuondoka niliitwa nikawa natembea tu,daah nilikula buti kadhaa na mp,kufika bwenini wakaja form two na 3 kupokonya vitu nilikuwa na sukari na mikate,kesho yake baada ya assemble,gwaride namm nilichelewa kidogo wenzangu walikuwa wanajua baadhi ya matendo,nilikula buti na wale makoplo sitasahau kabisa,ndani ya siku moja sina hamu na ilikuwa no way uwasiliane home hadi uende kwenye call box za ttcl.Walikimbia wengi sana ile form one but nilijikuta nimekuwa sugu Staki tena kuhama na ndo Shule iliyonitoa
 
Back
Top Bottom