Maisha ya binadamu na dhana ya Uongo!

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
35,744
Reaction score
86,370
Dhana ya Uongo imekuwa ni maisha yetu ya kila siku japo si jambo linalojadiliwa kwa upana sana ila athari zake zipo kila sekunde!.

Katika jamii nyingi uongo si jambo linalopendwa na vyombo vya sheria humtia hatiani mtu yoyote atakaebainika kusema uongo!, Hata hivyo ukiuzungumzia uongo basi upo karibu kuuzungumzia "UKWELI" hizi dhana mbili ni kama sarafu yani kichwa na mwenge.

Sifa moja wapo ya ukweli ni huwa unathibitika na ukishindwa kuuthibitisha ukweli maana yake ukweli huo ni uongo!, ila kuna baadhi ya vitu ni kama sheria za ulimwengu zinatuwia ugumu kwenye kuthibitisha.

Kwa maisha yetu haya yaliyogubikwa na kila aina ya shughuli za kisiasa,uchumi, mapenzi, sayansi na sanaa ni ngumu sana kuuepuka "UONGO!".
Kwani kwa hulka zetu mtu hudanganya kwasababu anazozifahamu yeye na kwa manufaa yake, kwa wengine uongo ni sanaa na kwa wengine uongo ni sayansi, kwa lugha ya picha naweza kusema uongo ni kama shuka linalofunika ukweli.

Kwanini watu tunadanganya..?
watu tunadanganya kwasababu ya hisia na vilevile kimantiki.

Kihisia huwa tunaficha jambo fulani ili lisijulikane maana tunajua tukisema ukweli tunaweza kuchukuliwa hatua, kimantiki imekaa sana kifaida hii inaingia sana kwenye maswala ya uchumi napia mtu hudanganywa kutokana na vile anapenda kusikia nini!.

Binafsi kwenye hili ndio naona ni kama hesabu kwani unamdanganya mtu kutokana na vile anahitaji nini kusikia hata kama haina faida kwako!.

Tunadanganya pia kwasababu uongo muda mwengine hununua muda, huponya navilevile huweza kuwafanya watu watizame kitu katika namna yatofauti ama vile anavyohitaji mdanganyaji!.
sio kwamba naupamba uongo ni vile uongo unaweza kuwa namanufaa fulani fulani ukiwa upande wa unufaikaji!.
yapo pia madhara ya uongo ila hutegemea na jambo gani kwani uongo pia huweza kupelekea hata kifo!.

Uongo hutumika kwenye uongozi kama dhana yakuwatuliza watu kwani muda mwengine watu kuambiwa ukweli huweza kuleta mtafaruku ambao huvunja amani yote!. kwajinsi nikilitazama hili swala la uongo sisiti kusema uongo ni sehemu ya maisha ya binadamu kwani watu huweza hata kuongopa kwa kutumia matendo!.

Uongo katika ujasusi ni kama siraha hili sote twafahamu majasusi hutumia dhana hii aidha kujilinda au kuangamiza ama kuhitaji jambo fulani.

Uongo kama uponyaji ama tulizo, zipo baadhi ya taarifa kuwapatia watu wenye matatizo ya afya huwaletea shida sana hivyo dhana hii hutumika pia ili kuweza kuwatuliza ili yasiwafike yakuwafika hapa tunasema kutumia hekima ya kibinadamu!.

Kwa uchache naweza kusema dhana hii ni pana sana hivyo sitaweza kugusia katika kona zote ila iwe ni kwa siri ama sio kwa siri inahitajika uwe na uelewa mpana katika kuimudu dhana ya uongo yani ipo hivi.
Kwa mdanganyaji hii ni siraha inayohitaji uwe na akili sana yakuitumia pia kwa mdanganywaji huu ni mtego usipoweza kuutegua utakuangamiza!.

Nina swali kwako msomaji je, unafikiri ipo haja yakuanzisha sheria yakumlinda mtu aliesema uongo ambao umeweza kumsaidia mtu mwengine...?

Vilevile nina hoja na swali ndani ya hoja!.
Katika vitabu vya dini yani biblia na Quran vinautaja uongo kama dhambi na kitu kisichofaa ambacho kinaweza kumpeleka mtu motoni!, sasa je, vipi ikiwa uongo huo unamsaidia mtu kiafya (kumuepusha asife n.k) ni vyema kumuongopea au ni bora kumuambia ukweli pasipokujali kitakachomkuta ikiwa unafahamu ukimuambia ukweli nini kinaweza kumkuta, je kwenye hili tunaacha dini iongee au hekima..?
 
Uongo ni asili yetu na haukwepeki.

Kuna magonjwa ya akili ambayo moja ya dalili zake ni kushindwa kusema uongo.

Naamini sheria zimekaa kimuktadha sana. Lazima kuna muktadha unaruhusu sheria kumlinda muongo.

Dini hazituzuii kusema uongo na haziwezi kufanya hivyo. Zinatupa miongozo ya kutazamia.
 
Miongozo gani hiyo mkuu..?
 
Muongo na muuaji hawana utofauti kabisa,, sipendi kudanganya na sipendi kudanganywa ila jamii iliyo nizunguka sasaπŸ˜„πŸ˜„ wamejaa waongo na wanafki ni wananikera mpka basi,,, Jitu linakudanganya ukigundua ukweli,utaskia "ooh nilikua sitaki kukuumiza" madafaka
 
Kuna siku natoka job naenda hom nikiwa njian gafla nakutana na gari jeus vx8 kuna njemba ikachomoka ikanisimamisha kwakuwa mwenyewe najiamin nikamfuata afu nikamuangalia kwa macho flan ya dharau akauliza boss wako yupo ofisin kiufup bos alikuwa hajatoka ila taa nyekundu ikawaka ikanambia hawa c watu wema nikafikiria kwa kina jamaa kama akapaniki akaniuliza kiukali dogo inamaana hujanisikia asee katk vitu sipend kuniita dogn hata kama umenizid umri nikamjibu fasta we matako nin c nimekwambia hayupo au unasikilizia makalio afu nikasepa kumbe wale jamaa ni watekaji walienda had ofisn kuhakikisha lengo wakamteka bos niligundua hilo baada ya siku ya pili boss kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha kwakuwa mwenyewe mtoto wa kitaa na ninajua mazingira ya majambaz na uhun uhun mana some time nakulaga tizi na wahun majambalika bas nilimfuata nikamkuta ameteswa vibaya ila nilifanikiwa kumuokoa hapa tunaongelea nilitumia uongo kumuokoa kwa kusema bos hayupo kumbe yupo ila walienda wakamkuta
 
Kama boss yupo vizuri ni jambo jema.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Umeleta hoja pana sana hii.

'Kutungwa sheria yenye kulinda uongo wenye manufaa'πŸ˜ƒ!

Kuhusu vitabu vya dini namna vinavyouongelea 'uongo', havina uhalali ama ukamilifu wa kuulani uongo kwa sababu wao pia wametumia uongo(hadithi) katika kujenga mantiki kwenye simulizi zao!

Kuna jambo muhimu umelieleza, lakini umemaliza mada bila kuliwekea angalizo, jambo hilo ni ule ukweli unaoshindwa kwa kutumia uongo na kuonekana kuwa ukweli huo ni uongo!

Nilitaka kusikia pia kuwa itungwe sheria ya kuulinda ukweli huo ulioshindwa kwa kutumia uongo.

Maana ilivyo sasa, uongo ukiushinda ukweli, mada ama kesi hufungwa na mambo hayo yameleta madhara makubwa kwa binadamu wengi wakweli, wasiokuwa na hatia na mambo huishia kuisha hivyo bila ya way foward.
 
Hii haihitaji sheria maana ukweli unatakiwa uthibitike tu so ukiweza kuuthibitisha basi kesi ushaimaliza!, shida inakuja muda mwengine ni ngumu sana kuuthibitisha ukweli japo anaefahamu hili jambo lilitokea ni ukweli dhahiri.
 
Ukiweza kuongea uongo kwa kujiamini na ukaaminika, Ipo siku utaongea ukweli huku unalia kwa hisia na Usiaminike.
Inategemea uongo mwengine huwa una muda wakuishi, kuna uongo hukaa muda mrefu sana huu unahutaji gharama kuulinda na kuna uongo hukaa muda mfupi ina maana hata ukija kuwaambia ukweli wahusika basi taarifa hiyo inakuwa haina nguvu tena watajua tu uliwadanganya basi!, hapa ndipo unapotakiwa ucheze na calculation...

nakubaliana na hoja yako pia.
 
Hehe! pole
 
Naskia wanaume wameumbwa na hulka ya uongo
Ukiwa mtu wakujihusisha na vitu vingi basi asilimia za kuongopa nazo zinaongezeka!. kwenye jamii wanaume ndio viumbe tunaojihusisha na vitu vingi na vyengine ili ku win hakuna kutia huruma ni kuupepeta uongo tu!..πŸ˜…
mwanaume huwezi kukaa tu unatia huruma unataka upewe vitu kwa kuhurumiwa muda mwengine hata kama huiwezi unasema unaiweza maana bila hivyo hulambi kitu!.. so mambo ni mengi mkuu
 
Hio ni mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…