Mkuu Zyansiku uko sahihi kabisa, nilikuwa naangalia ile jana na wife nikamwambia kabisa hizi fadhila anazofanyiwa Neema hizi si za kawaida. walijidai kumtoa feki, ili isionekane kama ni upendeleo wakamuunganisha na yule jamaa wa kiume, wakapelekwa saluni sijui kufanywa nini huko, nadhani ilikuwa opportunity ya kwenda kumtumia. sasa wamerudi tu kundini kapigwa na keki ya Birthday, na mwenzie aliyekwenda naye akawa evicted yeye amebaki. Mkuu AMA nadhani jaribu kufuatilia vizuri mtiririko wa matukio yanavyokwenda pale kijijini utaelewa. Lisemwalo lipo baba