Maisha ni Watu

Maisha ni Watu

CONTROLA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2019
Posts
7,087
Reaction score
23,869
Katika maisha tunayoishi tunahangaika sana kutafuta pesa,furaha,mali,nk kila siku tunapoamka kila mtu kuna kitu anawaza kichwani mwake kuhusu kesho yake,tumetofautiana kimalengo na kimawazo kwasababu ninachokiwaza mimi kitokee kesho yangu n tofauti na chako na mwisho hayo ndio maisha.

Leo nataka tupige story kuhusu nionavyo mimi najua tunatofautiana wewe unaona vingine ila mimi nionavyo ktk haya maisha pambana sana,pigana sana,hangaika sana ila kama utakua peke yako unachokifanya ni sawa na Zero yani sifuri.

Tunatafuta pesa tunapozipata pesa ni lazima hizi pesa tuzitumie,hivi inawezekana ukatumia hayo mahela yote peke yako? hivi inawezekana ukawa na furaha peke yako tu bila mtu kuisababisha? kwa upande wangu nadhani ni haiwezekani.

ili uweze kuya enjoy maisha ni lazima watu wawepo na si bora watu ila wawepo wale watu ambao wamesababisha wewe kupata hela,wamesababisha wewe kuwa na furaha,wamesababisha wewe kuwa hapo ulipo,tunahitaji Watu ili kukamilisha circle yetu ya kuenjoy haya maisha.

December ni mwezi ninaosafiri kwenda kujumuika na ndugu,jamaa,wale wa damu damu huwa ni moment flani nzuri sana naipenda japo huwa inakuaga ya muda wa siku chache sana,ninapokua njiani kurudi kwangu kuanza mwaka nikiwa peke yangu huwa najionaga mpweke sana natamani sana kuwa na company ile ile hata ktk maisha yangu lakini si bora tu watu ila niwe na watu tutakao waza sawa,tembea sawa,fikiria sawa na kila tutakapokamilisha lengo letu flani tujipongeze pamoja.

Huu ni mwisho wa mwaka nimefungua hii thread JF nadhani itakua thread ya mwisho kwa huu mwaka thread zangu zingine zitaanza January kama Mungu atatupa uzima,mimi ni moja ya watu ninaopenda kutoa na kusaidia watu kwa kile kidogo sana ninachokipata ktk mahangaiko yangu.

Kila mtu anaweza kutoa asante na shukurani yake kwa mtu aliemfanyia jema ktk maisha yake,mimi kama controla nimepata mafunzo mengi,elimu,pesa,nk kupitia JF nitakua mchoyo wa fadhila nisiporudisha asante zangu kwa huu uongozi wa wavumbuzi wa huu mtandao uliobadilisha maisha ya wengi namimi nikiwa mmoja wao.

Sina pesa za kugawa kwa kila member hapa JF sina uwezo huo,kuna muda nawaza niwafanyie kitu member wote wa JF lakini najikuta nawaza nakupitiliiza sasa basi nimeamua kufanya kitu kidogo kwa member wawili walio ndani ya JF.

Member hawa wawili ninaotaka kufanya kitu ni kama shukurani yangu kwa JF na hii wengine wanasema tunarudisha kwa Jamiii,Huu ni mtandao lakini ni Jamiii yenye watu tofauti,wagonjwa,wazima,maskini,matajiri,nk

Hawa member ninaotaka kufanya kitu kwao hamuwezi amini eti (siwajui) kweli siwajui lakini nataka wao wenyewe waamue niwajue na wakikubali nikawajua basi sadaka yangu itakua zawadi ya kuwatoa hapo/huko walipo na kuwasogeza hadi nilipo mimi.

Kuna member wapo Humu JF wanapitia shida kubwa sana ktk maisha yao,hawana pakulala,hawana pakula,yani faraja yao ni kuingia JF simu zao ndio rafiki yao mkubwa hawana zaidi ya hapo.

kundi hili la watu si mlemavu,wala si mgonjwa ila amekata tamaa kutokana na kujaribu sana na kushindwa,kuomba sana Mungu mpk sasa amechoka anahisi Mungu hamsikilizi,yupo haelewi afanye nini aanzie wapi,anaranda randa na maisha ukikutana nae njiani ukimuuliza unaenda wapi atakosa la kukujibu maana ni hajui.

Sasa basi nahitaji kusaidia watu wawili wanaopitia hali hiyo ambao wapo humu JF ambao wao machozi yameshakua jambo la kawaida haipiti siku hajalia,furaha kwake haelewi nini maana yake,anahisi dunia imefika mwisho haoni tena mbele anatamani atokee mtu amwambie Njooo ulale hata bandani kwa kuku wangu,anatamani vitu ambavyo hajui ni lini atapokea huo muujiza wa hivyo avitamanivyo vitokee kwake.

Nilisema mwanzo wakati naanza andika hii thread kuwa maisha ni watu na watu wenyewe ndio sisi lakini tunahitaji watu sahihi katka maisha yetu ili kukamilisha furaha tunayoitamani.

Mtu yeyote mwenye shida asie na pakulala,pakula,kazi yakufanya,nk mwenye huzuni na mambo ya namna hiyo kabla mwaka haujaisha namuhitaji atoke huko alipo aje aishi namimi tuishi kama familia atakula na kuvaa juu yangu,akilia mimi niwe sababu,akicheka mimi niwe sababu,akikonda mimi niwe sababu akinenepa mimi niwe sababu,awe sehemu ya maisha yangu.

Kupitia mimi nataka kuona watu wawili tokea humu JF wana tabasamu kama wanavyotabasamu wengine niliojitoa kwao,lakini wakati huu sitochukua tu ilimradi nitahitaji vigezo ambavyo vikitimizwa basi muhusika uwe huru kusema changamoto na maisha yako kwa ufupi unayopitia kwenye comment na wapi ulipo,nitakua kimya sitojibu comment yyte zaidi ya wahusika ninaowatafuta.

Kila mtu atasaidia yule atakaeguswa na simulizi na mapito yake kwa namna anayoona yeye lakini mimi wale wawili nilioamua kuwasaidia nitawasaidia endapo

1.Acc yake iwe Verified

ambae account yake haiko verified na akanigusa ktk simulizi yake na anahitaji awe sehemu ya maisha yangu itambiidi a verify Account yake,atakapotimiza hilo tu akapata Green Tick toka JF huyo ataandamana nami popote nitakapokua for the rest of his/her life.

Jinsia sijali ni wakiume au wakike au wakike wote au wakiume wote nimeamua saidia nitasaidia member wawili bila kujali watakua jinsia mbili tofaut au zitagongana jinsia 1 eneo hilo sina ubaguzi wala sharti aina lolote.

2.Asiwe Mtu Mwenye Familia

Nimeamua kusaidia mtu mmoja ambae hana watu nyuma yake,kwahiyo yawezekana kuna mtu ana watoto nyuma yake,ana ndugu yuko nao au vyvyte vile mtu wa aina hiii tupo wengi humu JF simulia storia yako kwa wingi wetu tukitoa kidogo kidogo hutokosa cha kukusogeza mbele.


3.Makundi maalumu (special Groups)

watu wanaotoka kundi hili pia msisite wala msiache simulia historia zenu kama mpo,maana kwa wingi wetu humu JF naamini tukijikusanya kidogo kidogo hatutoshndwa kukusaidia huko huko ulipo,naomba mimi niishie hapa maana huwa simalizagi nikianza andika kitu nilichokidhamiria toka ndani ya moyo wangu.Walionielewa wapo naamini wapo pia ambao risala hii hawajaielewa kabisa nitaomba walioelewa wasaidie kuwaelewesha waliolewa lakini zaidi wale wahitaji huu ni uwanja wao,narudia tena mimi nitakua kimya nikipitia kila ataetoa yake yamoyoni ila kama pia watakosekana watu nitashukuru kwasababu siombei wala sitamani uwepo wa wanaoteseka kwahyo kama hatoonekana mtu kabisa pia nitasema asante kwa Mungu maana anatutetea na kutoanekania sisi tulio wake.

Happy 2020 tukutane January Mungu akipenda.

Controla.
 
MUNGU akubariki sana Controla kwa nia yako hiyo.
Najua si vyema kumfanya mtu ajianike hadharani ili tu umsaidie LAKINI ni kipimo kizuri maana mwenye shida ya kweli hana cha kupoteza kwahivyo hatoona aibu wala soni kujiverify hapa.

All the best in the coming 2021.
 
Hongera Sana mwamba
Mungu azidi kukuinua kila iitwapo Leo na uzidi kuwa baraka kwa wengine.
 
mkuu nia yako ni njema bt bora ungewaita pm wakajieleza maana hapa wengi watahisi wanajidhalilisha.
 
Mbuzi ukimlisha vizuri unamnywa Mchuzi.
Watu ndugu watu, hakuna kitu.
Wahenga walishayafanyia conclusion.
-tenda wema
-ukimfadhiri binadamu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom