Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,114
- 79,522
MAISHA NI VIPAOMBELE
Na, Robert Heriel
Maisha hayana bahati nasibu, maisha huja kwa makusudi maalumu. Hakuna jambo linalotokea kwa bahati, kila litokealo chini ya jua limepangwa kwa makusudi kabisa.
Watu wengi hasa wale tuishia katika ulimwengu wa tatu tunaamini kuwa maisha hayana Fomula, kumaanisha kuwa maisha ni jambo linalotokea tuu kwa bahati. Kukubali dhana hiyo ni kukiri na kuthibitisha kuwa uwezo wa kiakili kwa wafuasi wa dhana hiyo ni duni.
Usipopanga maisha yako basi kuna watu watakupangia maisha yako. Maisha ili yawe na maana lazima wawepo wapangaji na wapangiwaji. Wapangaji huyaona maisha kama jambo la kujiamulia, wakati wapangiwaji huona maisha kama jambo la kuamuliwa.
Wapangaji huyaona maisha kama jambo lenye fomula
Wapangiwaji huyaona maisha kama jambo lisilo na fomula.
Katika kubaini makundi hayo mawili, mtu ataweza kuwatoshafautisha watu waliomo katika makundi hayo kwa kuangalia jambo kuu moja, nalo ni SHERIA.
Wapangaji wa maisha huwa na tabia ya kujiwekea sheria nyingi mno ambazo kimsingi huzifuata.
SHERIA hizo huhusisha kanuni, taratibu, miiko na desturi ambazo tabaka hilo huifuata.
Hii ni tofauti na WAPANGIWAJI, hawa hawana tabia ya kujiwekea sheria, wao huishi kama mbuzi au kondoo. Hawana sheria kama kanuni, taratibu, miiko na desturi wanazozifuata.
Kwa vile hawana sheria basi ni lazima maisha wayachukulie kama jambo la nasibu tuu, na kila kinachotokea hukiona kama bahati jambo ambalo halina ukweli wowote.
WAPANGAJI wa maisha kimsingi huwa ndio watawala wa Koo, kabila fulani, taifa na Dunia kwa ujumla.
Mtu hawezi kuwa mtawala katika nyanja za kisiasa au kiuchumi kama hayupo kundi la WAPANGAJI wa maisha.
Mataifa makubwa yaliyoendelea, au jamii zilizoendelea ukizichunguza karibu zote zinasheria nyingi kuliko jamii zozote zile duniani licha ya kuwa zina uhuru mkubwa. Taifa kama la Marekani, Ujerumani, Urusi, Uchina, Japan, Israel, Iran miongoni mwaa mataifa mengine makubwa, mataifa haya yanasheria nyingi kuliko jamii zingine.
Wapangaji wa maisha huwa na miiko mingi ambayo hupelekea kuwafanya kuwa wabaguzi kwa mataifa mengine. Kwa mfano Taifa la Israel, ambao ni Wayahudi ni nadra sana kwa watu wa jamii nyingine kuoana na myahudi, Wayahudi waanamiiko mingi mno, jamii ya Warusi, Wahindi, Wahispania, na wafaransa bila kuwasahau Waitaliano wanamiiko mingi mno katika kuchangamana na watu walionje na jamii yao.
Wapangaji wa maisha huzipenda sheria na desturi zao, hulinda tamaduni zao ikiwemo chakula, mavazi, dini, majina na sanaa.
Wapangaji wa maisha hawanaga shobo au kujipendekeza kwa tamaduni za watu wengine, huwezi mkuta Myahudi akijionea fahari kuzungumza lugha ya kiswahili. Au Mhindi akiitwa jina la kisukuma au Kihaya, au jina la kiswahili.
Wapangiwaji wa maisha kwa vile hawana sheria, wao wanaishi kama ng'ombe hujikuta wakimezwa na mataifa makubwa kwa kuathiriwa vilivyo na tamaduni zao.
Mpangiwaji wa maisha hupelekwa kama bendera ipelekwavyo na upepo.
Wakija wachina atataka awe kama wachin, akija mzungu atataka awe mzungu, akija Muarabu atataka awe Kama Muarabu.
Wakija wenye dini ya Kikristo utashangaa linaacha dini yake ya kijadi linakuwa likristo, wakiwaja Waislam linabadili tena linakuwa liislam wakati yeye ni Mpare. Upare na Uislam au Ukristo wapi na wapi ndugu?
Usukuma na Uislam au Ukristo wapi na wapi?
Wapangiwaji wa maisha ni kundi la wale waliojidharau na kujidunisha na kuona asili yao si kitu. Na ndio maana baadaye huja na dhana kuwa maisha ni nasibu jambo ambalo sio kweli.
Kwenye elimu na sayansi hakuna kitu cha nasibu, kila kitu hutokea kwa sababu na kwa makusudi maalumu. Mpangaji hupanga maisha, na mpangiwaji huona yaliyopangwa kama nasibu.
Maisha huwa na nasibu kama hakuna kitu Kiitwacho VIPAOMBELE.
Wapangaji wa maisha kwa vile hutumia sheria na kanuni basi lazima wawe na Vipaombele.
Hii ni Tofauti na Wapangiwa maisha, hawa hawanaga vipaombele.
Vipaombele ni mambo ya lazima ambayo unayapa nafasi ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne na kuendelee kwa mtiririko wa kutegemea umuhimu wake.
Mtiririko huo sharti uzingatie ulazima wa jambo katika mfumo wa maisha. Jambo la kwanza lazima litegemewe na jambo la pili, sio uweke jambo la pili liwe la kwanza.
Ngoja nikupe mfano;
Mpango: Kuwa Mfugaji mkubwa wa Ng'ombe.
1. Tengeneza Zizi au Ranchi au nunua eneo kubwa la kufugia ng'ombe kulingana na uwezo wako.
2. Gawanya maeneo kulingana na aina, sifa na umri wa ng'ombe. Mgawanyo huu uzingatie na malisho na uwepo wa maji, miinuko na mabonde, hali ya hewa kulingana na ng'ombe husika.
3. Nunua ng'ombe kisha watenge kulingana na sifa na matokeo unayoyataka.
4. Weka wachungaji, walinzi na wataalamu wa Afya wa mifugo
5. Andaa maeneo ya walinzi kupumzika
6. Tenga eneo la kuhifadhia chakula kitakachotumika wakati wa kiangazi wakati malisho yakiwa madogo
7. Mwisho, sio kwa mwisho kabisa, tengeneza eneo maalumu la Mnada, Bucha ambapo wateja wako watakuja kuchukulia mifugo yako
MFANO WA PILI
Kwa ambaye bado hana Familia
MPANGO; Kuwa na Familia Bora
Vipaombele
1. Jali Afya yako
Vipaombele kwenye Afya yako
1.1 Afya ya Akili
Jifunze ujuzi, maarifa, elimu, ufahamu na mambo yote yahusuyo akili wenye manufaa hii itakusaidia hatua inayofuata.
1.2 Afya ya Kiroho
Jifunze kuishi kwa imani kwa kufuata mafunzo ya akili ambayo ni elimu, ufahamu, maarifa, hekima, falsafa na ujuzi.
Imani ni uhakika wa mambo yatarajiwayo, bayana ya yasiyoonekanaa. Sasa huwezi kuwa na imani wakati huna akili, imani bila akili ni upumbavu. Akili ndio huleta imani, akili ni utambuzi, imani ni uhakika wa kile ulichokitambua.
Mtu asiye na elimu, maarifa, ujuzi, ufahamu, hekima wala falsafa hawezi kuwa na imani. Atajidanganya au kudanganywa. Na ndio maana watu kila siku wanaambiwa hawana imani kumbe indirect wameambiwa hawana akili. Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, sio imani. Na mwenye haki ataishi kwa imani sio akili. kumbuka, kipaombele cha kwanza kwenye maisha ni Afya, na katika afya cha kwanza ni afya ya akili, cha pili ni afya ya kiroho, kupitia roho tunakuwa na imani, tunakuwa na tumaini ya mambo yajayo ambayo tayari tumeyatambua kwa akii zetu baada ya kufanya tathmini
1.3. Afya ya kimwili
Jifunze kuishi kwa kuutunza mwili wako. Kula vizuri, kunywa vizuri, vita hewa safi, lala pazuri, na vaa vizuri.
Tunahangaika kwa sababu ya miili yetu, sio akili wala roho, miili yetu ndio inauhitaji.
Miili yetu ndio utambulisho wetu.
Tunza mwili uwe na haiba ya kike kama wewe ni mwanamke. Tunza mwili uwe na haiba ya kiume kama wewe ni mwanaume.
Usilegeze ngozi ya mwili kama wewe ni mwanaume, usiweke laini sana, usinukie sana, usijilegeze. Kumbuka wewe ni mwanaume, ukaze mwili ukae kiume, ngozi ikaze, sauti ikaze, kila kitu kikaze.
Mwanamke jilegeze, legeza ngozi, legeza macho, legeza sauti, usijikaze, legeza kila kitu lakini usilegeze sehemu zako za siri isipokuwa kwa mwanaume mmoja.
1. 4. Afya ya kihisia
Jifunze kuzipa afya njema hisia zako. Tiisha mihemko yako, iwe ni hasira, furaha, ashki za ngono au pombe, huzuni au furaha, kilio au kicheko, jifunze kuzitiisha hisia zako. Tawala njaa yako, tawala kiu yako, tawala tamaa yako ya ngono. Sio kila mwili unachotaka uupe. Ukisikia njaa, jaribu kukaa lisaa limoja ndio ule ili mwili usikuendeshe, ukiwaka tamaa ya ngono zizuie hata wiki kwa waliooa.
Ukikasirika tawala hasira zako, jifanye kama umezisahau hasira zako muda huo huo, jitahidi kama mtu kakuudhi leo basi muadhibu siku saba au miezi saba ijayo. usitawaliwe na hasira zako au mihemuko yako. Hii itakusaidia kwenye suala la maamuzi bora ukissaidiwa na afya ya akili na kiroho.
2. JALI MAHUSIANO YAKO
Hiki ni kipaombele cha pili kwa wanaotaka Familia bora.
Katika kipaombele hiki kuna vipaombele ndani yake vitatu ambavyo vitazaa kipaombee cha nne.
2.1. Jali mahusiano yako na Mungu wako
Fuata amri, sheria na maagizo yake
2.2 Jali mahusiano yako na Wazazi wako
Fuata mafundisho mazuri uliyopewa na wazazi wako, usiogope kuwafundisha pale walipojikwaa
2.3. Jali Mahusiano yako na ndugu, jamaa na rafiki(jamii)
Ishi vizuri na watu, usiwadhulumu, usiibe, usizini na watoto wa watu, usiibe wake za watu, usiue, usishuhudie jirani yako uongo, acha fitina, usengenyaji,
Mambo hayo matatu yatakupa Kipaombele kikubwa cha nne ambacho ni Mke/mume bora. Na hivyo utamalizia kipaombele cha nne ambacho huja badaye sana baada ya vipaombele vya kazi, na makazi. Kipaombele cha nne kweye JALI MAHUSIANO YAKO ni;
2.4 Jali mahusiano yako na Mwenza wako wa maisha
3. PENDA KAZI YAKO
Hiki ni kipaombee cha tatu kwa mtu anayetaka kujenga familia bora
Penda kazi yako, tenda kwa ufanisi zaidi, tenda kwa uaminifu, usimdhulumu mtu, hakikisha asilimia tisini ya unaowahudumia wanaridhika na kazi yako.
Usizidishe malipo kwa tamaa ya kujiongezea kipato, bali unaowahudumia ndio waone haja ya kukuongezea kipato.
Kusanya pesa, weka akiba, wape wahitaji. Kula bata na starehe kwa kiasi, furahia pesa zako bila kumuumiza au kukwaza wengine
Ukiipenda kazi nayo itakupenda
Ukiitambua kazi na kuiheshimu, nayo itakutambulisha kwa watu na kukuheshimisha. Usifanye kinyume
4. JENGA MJI WAKO/ MAKAZI
Kipaombele cha nne ni makazi,
Ukishakuwa na uhakika wa kazi yako inakuingizia kipato cha uhakika kuendesha maisha yako, kwa maisha ya kawaida yaani kula, kuvaa, kulala, basi jenga mji wako au makazi yako.
Makazi yanaweza kuwa ya aina mbili;
1. Kujenga nyumba yako mwenyewe
2. Kukodisha./ kupanga
Makazi ni makazi tuu ilimradi unauhakika wa kuishi na kuka bil bughudha.
Nunua vitu vya ndani, Vitanda na godoro viwe vizuri, viti vya kukalia wageni, vyombo vya kulia chakula, kutawazia, na kuogea. Urembo wa ndani kama mapazia ya milangoni, dirishani, mazulia, Saa ya ukutani. Vyombo vya mawasiliano kama vile luninga, Redio, simu ya mezani, Laptop. Vyombo vya muziki kama vile ngoma, Kinanda, Sabufa miongoni mwa vingine.
Picha za ukutani kama vile picha yako, wazazi au mwenzi wako, au wewe na watoto, picha zenye maua au jumbe mzipendazo miongoni mwa picha zingine.
Vyombo vya kutunzia vyakula kama vile Jokofu.
Vyombo vy kuhifadhia nguo kama kabati la nguo, viatu n.k
Taa za kila aina kulingana na muktadha wa chumba au tukio ndani ya nyumba au makazi yenu.
Kazi ndio itaamua mambo yote haya na mengine ambayo sijayataja. Ni lazima ufanye kazi kwa bidii ili kazi iwe na bidii ya kukupa kipato kizuri
5. OA/OLEWA NA MTU UMPENDAYE.
Kipaombele cha tano ni mwenza wa maisha.
Lazima utafute mtu umpendaye, unayefanana naye. Kumpenda mtu msiyefanana ni dalili ya ugonjwa wa kisaikolojia. Kiasili mtu humpenda mtu anayefanana naye, ila tamaa huweza kukudanganya kuwa unampenda mtu ambaye hujafanana naye.
Ukweli ni kuwa kumpenda mtu msiyefanana ni kutafuta maumivu na wala hakuna atakayejali.
Mfanane kimaumbile, kiakili, kitazamo, kiimani, kiuchumi na kimalengo.
Sio mtu ni handunje unajitia kupenda watu warefu wamekuzidi zaidi ya futi moja, huko ni kutafuta kudharaulika au kujidharaulisha.
Mtu masikini Bwiiii! Unatafuta wanawake au wanaume matajiri, hakuna mapenzi ya namna hiyo zaidi ya mateso.
Oa au olewa na mtu anayejivunia wewe, anayejivunia kazi yako, anayejivunia kila kitu chako.
Sio unaolewa au unaoa mtu anayeona aibu kazi uifanyayo. Yaani hataki watu wajue mume/mke wake unafanya kazi gani.
Ukifanikiwa kuoa mke au kuolewa na mume mnayefanana basi utakuwa ume-win maisha.
Matokeo ya kuoa au kuolewa na mtu mnayefanana ni haya;
Mwenza unaweza mpata ukiwa umepanga nyumba au ukiwa na nyumba yako ilimmradi uwe na kazi inayokuingizia kipato. Muhimu zaidi ni suala la umri.
Usichelewe wala usiwahi kupata mwenza wa maisha.
Mwanamke na mwanaume wote hakikisha kabla ya miaka thelasini uwe umeshaoa au kuolewa.
Utamu wa ndoa upo ujanani, miaka 25 - 35 hapo kila mmoja ananguvu ya kuufurahia utamu wa ndoa.
Ukichelewa, labda ni miaka 40 kuna hatari ya kushindwa kumridhisha mwenza wako hasa kitandani.
Ndoa ni kazi, ukishapata kazi ya uhakika Oa, mengine huja baadaye, hakikisha kabla ya miaka thelasini uwe umeshajiwekea kazi yako ya kuifanya maishani mwako, itakayokutambulisha.
6. ZAA WATOTO WAKO WANAOFANANA NA WEWE
Sharti la kuzaaa watoto unaofanana nao ni kuoa mke unayefanana naye.
Hutosumbuka kwenye malezi
7. JIANDAE KUFA
Hiko kiwe kipaombele cha mwisho,
Lakini ajabu siku hizi hiko kimekuwa kipaombele kisichokuwa cha mwisho.
Nimechoka kuandika jamani
Mwisho niseme, Kila mtu anaamu aishi vipi.
Penda nchi yako, kuwa mzalendo.
Ulikuwa nami;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Kasulu, Kigoma

Usisahau kuweka maeneo ya mapumziko ya ng'ombe
Usisahau kuweka mahali pa kunywea maji
Usisahau kutengeneza barabara ya magari kuratibu shughuli zote za uchungaji, ulinzi na usalama n.k

Sio kuaa vitoto visivyoeleweka kuanzia kimaumbile mpaka kitabiaMtazaa watoto wanaofanana na ninyi
Lakini kama utaoa au kuolewa na mtu msiyefanana, yanayotokea katika maisha yenu hayafanani na yale mliopanga kwani hata ninyi wenyewe mbona hamfanani.Kila kinachotokea kwenye maisha yenu kitafanana na vile mlivyopanga.