Maisha ni kula na kunywa.

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,675
9,993
Mwenzangu wewe unakula na kunywa nini?
Kula na kunywa kwako ndio kielelezo cha maisha yako.
Urefu wa maisha yetu unategemea sana misosi tunayokula.
 
Athari za muda mrefu za pombe
hutapakaa baina ya uwezekano wa faida za
kiafya kwa watumiaji wa viwango vya chini
vya pombe hadi madhara makubwa katika
hali yamatumizi mabaya ya pombe kwa
muda mrefu. Viwango vya juu vya matumizi
ya pombe huhusiana na ongezeko la hatari
ya kuendeleza ulevi, ugonjwa wa moyo,
kutofyonza vyakula, ugonjwa sugu wa
kongosho , ugonjwa wa ini kutokana na
pombe, na kansa. Uharibifu kwa mfumo
mkuu wa neva na mfumo wa neva za
pembeni unaweza kusababishwa matumizi
kila mara ya pombe.[2][3] Matumizi ya
pombe kupita kiasi kwa muda mrefu
yanaweza kuharibu takribani kila kiungo na
mfumo katika mwili.[4] Ubongo unaokua
wa kijana aliyebaleghe huwa hasa katika
hatari kubwa ya kudhurika na sumu ya
pombe.[5]
Kihistoria, madaktari wametetea pombe
kwa faida zake za kiafya na hivi karibuni
kwa ajili ya uwezo wake wa kulinda
watumiaji dhidi ya ugonjwa wa moyo. Kuna
ushahidi wa faida kwa mishipa ya moyo
inayotokana na kutumia kinywaji 1- 2 kwa
siku, hata hivyo, faida za kiafya kutokana na
unywaji pombe kwa wastani ni swala lenye
utata. Shauku zimetolewa kuwa sawa na
ilivyo katika sekta ya dawa, wadau wa sekta
ya pombe piawamehusika katika kutilia
chumvi faida za kiafya za pombe. Pombe
inapaswa kuonekana kama dawa ya
burudani yenye uwezo mkubwa wa
kusababisha athari mbaya kwa afya na
hipependekezwi kwa-ulinzi wa moyo badala
ya mbinu nyinginezo za salama na
zilizothibitika za jadi kama vile lishe bora
mazoezi na tiba za dawa.[6][7]
Baadhi ya wataalamu wanadai kuwa faida
za matumizi ya pombe ya wastani zinaweza
kupitwa na ongezeko la hatari ikiwa ni
pamoja na majeraha, vurugu, uharibifu wa
mimba, aina fulani za saratani, ugonjwa wa
kongosho na presha.[8] Kwa vile faida
bainifu za kiafya za matumizi ya pombe ya
wastani ni ndogo kwa watu walio katika
hatari ndogo ya kupata maradhi ya moyo,
wataalamu wengine wanatahadharisha
itumike kwatahadhari kwa sababu ya
uwezekano kwamba kupendekeza matumizi
wastani ya pombe kunaweza kusababisha
ongezeko la hatari ya matumizi mabaya ya
pombe, hasa miongoni mwa vijana.[9]
Manufaa haya ya matumizi wastani ya
pombe yanapitwa na hatari za matumizi ya
pombe wastani.[8]
Tafiti za kisayansi
Historia
Madhara mabaya ya matumizi ya pombe
kwa muda mrefu kupita kiasi ni sawa na
yale yanaoonekana katika vitulizi-hipnoti
vingine (mbali na sumu kwa viungo ambayo
hutatiza zaidi katika pombe). Athari za
kujiondoakatika pombe na utegemezi
hukaribia sana kufanana.[10] Pombe cha
kiwango wastani ina athari chanya na hasi
kwa afya. Athari hasi ni pamoja na ongezeka
la hatari ya magonjwa ya ini, sarataniya
orofarinji, kansa ya umio na ugonjwa wa
kongosho. Kinyume na hayo, unywaji
wastani wa pombe unaweza kuwa na athiri
za faida kwa gastriti na kolelithiasi.[11]
Matumizi sugu na mabaya ya pombe huwa
na athari kubwa kwa afya ya mwili na akili.
Unywaji sugu wa pombe kupita kiasi au
utegemezi pombe, unaweza kusababisha
uharibifu mpana viungo mbalimbali vya
nevaza ubongo,mfumo wa neva ama
ugonjwa wa mishipa ya moyo, maradhi ya
ini, na neoplasmsi isiyopona. Matatizo ya
akili ambayo huhusishwa na ulevi ni pamoja
na mfadhaiko mkubwa, disthimia, mania,
hipomania, tatizo la hofu fobia , tatizo la
wasiwasi wa kijumla, tatizo la tabia za mtu,
skizofrenia, kujinyonga, upunufu wa mfumo
wa utendakazi mwilini (km kazi za
kumbukumbu, hisia, kazi za uamuzi, uwezo
wa kuona,mwendo na uwiano) na uharibifu
wa ubongo. utegemezi wa pombe ni
huhusishwa na shinikizo la damu, ugonjwa
wa moyo na kiharusi cha iskemi, kansa ya
mfumo wa upumuaji, mbali pia na saratani
ya mfumo wa mlo, ini, kifua na ovari.
Unywaji kupita kiasi huhusishwa na
ugonjwa wa ini, kama vile sairosi.[12] Utafiti
zimelenga wanaume na wanawake, vikundi
vya umri mbalimbali na watu wa makundi
mengi ya kijamii. Machapisho kwa sasa
yanafikia jumla ya mamia huku tafiti
zikiweza kuonyesha uwiano uliopo kati ya
matumizi wastani ya pombe na afya ambayo
labda yanaweza kuwa yalitokana na athari
za manufaa ya maingiliano ya kijamii
ambayo mara nyingi huambatana na
matumizi ya pombe. Baadhi ya njia
mahususi ambapo pombe huweza kuathiri
afya ya mishipa ya moyo zimetafitiwa.[13]
Mtazamo wa kisasa
Utafiti fulani katika baadhi ya nchi umedai
kuwa vifo vinavyosababishwa na sababu
zozote zile vinaweza kufikia viwango vya
baina ya 16 hadi 28% kwa uchache
miongoni mwa wanywaji wa wastani
(vinywaji 1-2 kwa siku) ikilinganishwa na ile
miongoni mwa wanaojiepusha na unywaji
kabisa.[14][15][16][17] Mmwandishi wa
habari Roni Caryn Rabin wa New York Times
anasema kwamba takwimu za utafiti huu
zina makosa.[18]
Upeo wa kiasi kinachopendekezwa
Habari zaidi: Recommended maximum
intake of alcoholic beverages
Nchi mbalimbali hupendekeza kiasi tofauti
cha upeo wa kunywewa . Kwa nchi nyingi
kiasi cha upeo kwa wanaume ni 210g-140g
kwa wiki. Kwa wanawake, kiasi ni 84g-140g
kwa wiki. Nchi nyingi hupendekeza
kutumiwa kwa pombe kabisa wakati
ujauzito ama kunyonyesha.
Vifo vinavyohusiana na Pombe
Matumizi ya pombe kupita kiasi ni
mojawapo ya sababu zinazoweza
kuzuilikaambayo husababisha vifo vingi
kote duniani.[19] Utafiti mmoja unahusisha
pombe na kila kifo 1 katika 25 kote duniani
na kwamba 5% ya miaka wanayoishi watu
na ulemavu hutokana na matumizi ya
pombe.[20][21]
Nchi hukusanya takwimu kuhusu
wanaofariki kwa ajili ya pombe. Huku
baadhi ya takwimu zikihusiana na athari za
muda mfupi kama vile ajali, nyingi
huhusiana na athari za muda mrefu wa
kutumia pombe.
Urusi
"Matumizi ya pombe kupita kiasi nchini
Urusi, hasa kmiongoni mwa wanaume,
katika miaka ya hivi karibuni imesababisha
zaidi ya nusu ya vifo katika umri wa miaka
15-54.[22]
Uingereza
Vifo vinavyohusiana na pombe nchini
Uingereza ni huainishwa kwa kutumia
Uainisho wa Kimataifa wa Magonjwa, Toleo
la Kumi (ICD-10).[23] ICD-10 hujumuisha:
Matatizo ya akili na tabia kutokana na
matumizi ya pombe - ICD-10 F10
Kuzorota kwa mfumo wa neva kutokana na
pombe - ICD-10 G31.2
Polineuropathi ya pombe - ICD-10 G62.1
Kadiomiopathi ya pombe - ICD-10 I42.6
Gastriti ya Pombe - ICD-10 K29.2
Ugonjwa wa ini wa pombe - ICD-10 K70
Hepatitis sugu , isiyoainishwa mahali
kwingine kokote - ICD-10 K73
Fibrosi na sairosi ya ini - ICD-10 K74 (bila
kujumuisha K74.5 K74.3-Sairosi ya biliari)
Ugonjwa sugu wa kongosho kutokana na
pombe - ICD-10 K86.0
Sumu itumikayo kiajali kutokana na
mkumbano na pombe - ICD-10 X45
Sumu itumikayo na mtu binafsi kimaksudi
kutokana na mkumbano na pombe - ICD-10
X65
Sumu kutokana matumizi na kukumbana na
pombe, bila kusudi wazi - Y15 ICD-10
Mashirika ya takwimu ya Uingereza
yanaripoti kwamba "Kulikuwa na vifo 8,724
vinavyouhusiana na pombe katika mwaka
2007, chini zaidi kuliko 2006, lakini zaidi ya
mara mbili ya 4,144 iliyorekodiwa katika
mwaka 1991. Kiwango cha vifo kuhusiana
na pombe kilikuwa 13.3 ya watu kwa kila
watu 100,000 mwaka 2007, ikilinganishwa
na idadi ya watu 100,000 6.9 kwa mwaka
1991."[24]
Nchini Skotlandi, NHS inakisio kwamba
katika mwaka 2003 kifi cha kia mtu mmoja
katika 20 waliofariki inaweza kuhusishwa
na pombe.[25]
Utafiti wa 2009 uligundua kuwa watu 9,000
hufa kutokana na magonjwa yanayohusiana
na pombe kila mwaka, mara tatu ya idadi ya
miaka 25 ya hapo awali.[26]
Marekani
Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji Magonjwa
kinaripoti kuwa, "Kutoka 2001-2005,
kulikuwa na takribani vifo 79,000 kila
mwaka zinazotokana na matumizi ya pombe
kupita kiasi. Kwa hakika, matumizi ya pombe
kupita kiasi ni ya 3 katika sababu
zinazoambatana na mitindo ya kimaisha
kwa kusababisha vifo kwa watu nchini
Marekani kila mwaka".[27] Utafiti mmoja wa
1993 ulikadiria vifo vya waliofariki Marekani
kupitia pombe kuwa 100,000. [28]
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom