Hakuna tabia za kijerumani bali nchi ina mifumo ya Afrika Kusini, kila kitu kinatoka SA, miji yao japo midogo sana kwa mfano mji una watu 40,000 tu lakini una malls nyingi na kubwa kuliko Dar es Salaam.Tanzania na Namibia tunahistoria moja ya kutawaliwa na wajerumani mpaka 1918, inakuwaje wao wawe na tabia za kijerumani na sisi tusiwe nazo.
Ukiwa expert utafurahi na kuishi kizungu vinginevyo hakuna biashara ndogo ndogo za kimachinga sana watu wengi hununua vitu super market.
Nchi ni ya kibepari kama SA kwani walitawaliwa na SA hadi 1990. Kuna wanabia wengi waliishi Tz kama wanafunzi wa Nyerere wakati wakipigania uhuru na wanamweshimu Nyerere na watanzania sana. Hawa huongea Kiswahili.
Pamoja na uchache wa watu (2.5m) yaani kama mkoa wa tanga tu nchi ya Namibia ina eneo kubwa kama Tz, ila ardhi nzuri imeshikwa na walowezi wachache wa kizungu ambao hata hawaishi Namibia. Ardhi ni ghali mno pamoja na kwamba ni jangwa jangwa.
Kuna fursa ila inabidi uwe capitalist mkubwa sio mmachinga. Wazungu wachache waliopo huku wana-enjoy kuliko Ulaya.
Wanamibia ni watu wazuri na friendly sio kama wasauzi au waBotswana na hufanya kazi kwa ushirikiano na wageni.
Ukija Namibia usiishi kwenye miji mikubwa hasa Windhoek au swakopmund miji hii ni ya kizungu na ghali sana.
Karibuni South West Africa.