Maisha nchini Namibia

Maisha nchini Namibia

Bird Watcher

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2013
Posts
4,205
Reaction score
8,445
Najua ziara ya mkuu italeta chachu kubwa kwetu migrants wa mataifa mbalimbali wasaka tonge popote pale, risk takers, tourist and so far, Tunaomba mliopo Namibia mtujuze fursa zikoje huko kwa professionals and non professionals Vipi life huko japo ka nchi kako na roughly 2.5m population ila tunaomba muongozo tuone namna ya kujipanga.
 
Namibia ni nchi kubwa sana kwa eneo. Ila eneo kubwa la nchi hiyo ni jangwa... Eneo linalokaliwa na binadamu ni eneo dogo. Namibia imefanana sana na Libya ambayo nayo ina eneo kubwa sana lakini eneo linalokaliwa na watu ni dogo kwa kuwa eneo lililobaki ni jangwa.
 
Jamaa ni wagumu sana kutoa resident permit kwa waafrika .Hawataki nchi yao ichafuliwe.Hakuna Machinga kule au waendesha bodaboda kama huku kwetu.Mwisho pamoja na kuoa kule alijiamulia kurudi bongo maana permit haikuwa rahisi kuipata.Tafuta story ya Mwisho wampamba ilisambaa kwenye mitandao miaka ya nyuma akilalamikia hii issue ya resident permit.https://www.jamiiforums.com/threads/mwisho-mwampamba-kufukuzwa-namibia.530681/
 
Nchi safi....imepangika vizuri sana...ofisi za mipango miji huko kwao zimefanya kazi yake ipasavyo....
 
Tatizo la hiyo nchi ni ubaguzi pia maisha yako juu kwa kiasi flani japo utafitaji wake (amafaranga) siyo mgumu.

Ukienda kama mwajiliwa utaishi vizuri ila private utarudi mwenyewe tu...!
 
Namibia ni nchi ngumu kuishi kama wewe sio mfanyabiashara au mtaalam au "expatriate".

Mji mkuu wa Windhoek ni mji wa 150 wenye maisha ghali.

Fursa pekee iliyopo ni kuingiza bidhaa mbalimbali khasa vyakula na kama una fedha za kutosha basi unafungua duka lako mwenyewe la maana na sio genge la kupanga nyanya mbili tatu.

Ila mfumo wa kodi na taratibu za kulipa ushuru zinaweza kukupa shida kidogo.

Namibia ina miji mkiuu mitatu Windhoek, Walvis Bay na Swakopmund.

Wanamibia wana tabia za kijerumani kutokana na historia ya kutawaliwa na wajerumani na kizazi cha warerumani bado jipo Namibia.
 
Tanzania na Namibia tunahistoria moja ya kutawaliwa na wajerumani mpaka 1918, inakuwaje wao wawe na tabia za kijerumani na sisi tusiwe nazo.
Baada ya vita ya kwanza Namibia iliwekwa chini ya uangalizi wa SA ambayo ilikuwa chini ya makaburu. Kumbuka makaburu wana asili ya udachi na ujerumani hivyo ndugu moja. Sisi tuliwekwa chini ya uangalizi wa mwingereza na mazalia ya wajerumani bado tunayo Iringa, Bukoba na baadhi Moshi.
 
Baada ya vita ya kwanza Namibia iliwekwa chini ya uangalizi wa SA ambayo ilikuwa chini ya makaburu. Kumbuka makaburu wana asili ya udachi na ujerumani hivyo ndugu moja.
Hata hao waingereza sisi hatuwahusudu kiivyo, je watanzania ni toto tundu au imetokea tuu sisi kuwa waswahili?
Sisi tuliwekwa chini ya uangalizi wa mwingereza na mazalia ya wajerumani bado tunayo Iringa, Bukoba na baadhi Moshi.
Nafahamu mazalia ya wajerumani Lushoto, je uweupe uchangani unatokana na damu ya kijerumani?
 
Kila kitu Wakenya.. wakenya.
Katika dunia hii wakenya ndio unawaona watu wa maana sana kiliko nchi nyingine zote!?
Hakika ujinga mzigo.
Mtanzania akisafiri nje akirudi Ni kuonyesha tu album ya picha alizopiga akiwa nje kwani uongo?
Hicho ndicho anachoanza kusimulia.Uliza watanzania hata wakisafiri kwenda nchi jirani hapo Rwanda tu wakirudi uwasikie watakachosema.Atakuonyesha picha alizopiga na Cha pili atakwambia aisee Rwanda kusafi ,kumepangika.Full stop.Hawezi sema Kuna fursa gani.Hata ukimuuliza Hilo swali kuwa Rwanda Kuna fursa gani? jibu unakuta hana anajiuma Uma mdomo na anatoa tu mimacho Kama mjusi aliyefiwa na mkwewe.
 
Back
Top Bottom