Maisha magumu sana jamani

Hali tight sana na kwatuliomaliza vyuo aisee cio powa.
Wewe uliomaliza Kusoma Au ushauri wangu kwa waliomaliza kusoma Jaribu kuwa creative kubuni kitu ambacho pengine kinaweza kukuongozea kipato At kidg kwa siku Usikae ndani toka zunguka maeneo yenye mchanganyiko wa watu pengine akili inaweza ikazalisha kitu kutokana na elimu uliokuwa nayo Na Allah akakusaidia kwa uwezo In shaa Allah
 
Hela inatosha kula mmoja tu.....nyie ndio mnapanga mnakula muda Gani........

Hakuna tena furaha kwenye familia na jamii kwa ujumla............

Chakula kimekuwa anasa, ukionekana unakula watu wanakushangaa........

Ukiandaa sherehe labda ufunge milango ndio ule na wageni maana watu watajaa wengine hata uwajui......

Watu wanaenda waongea peke Yao kama vichaa barabarani.........

Watu wamejaa hasira muda wote wapo siriaz kama wapo kwenye mafunzo ya kijeshi.......

Sura za watu zimekaa kishari Shari tu.......mtu ukimtazama mara mbili anakushushia tusi mpaka unashangaa...... kwenye dala dala mtu ukimwambia sogea kidogo tukae vizuri anaanza na tusi alafu ndio anakujibu...........

Sherehe za basdei zimepungua sana kama sio kuisha kabisa.....

Baba wa familia hata shikamoooo unaipata kwa mbinde......unawakuta wamenuna mpaka unakuwa mkali wewe Juma Hebu amkia........

Kwa kweli hii hali ikiendelea hivi tutamjua mwanaume maana imefikia hatua mtu ukifanikiwa kula Milo mitatu unajipongeza.........
 
Yaendelee tu kuwa magumu ilimkome kuchagua viongozi wasiojali maslahi ya wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…