Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,053
- 79,395
MAISHA HAYAHITAJI HARAKA. UKIONA MTU AU MFUMO UNAKUHITAJI UWE NA HARAKA UJUE UMEWEKEWA MTEGO WA KUKUANGAMIZA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Maisha ni mfumo wa kuishi bila pupa. Bila haraka.
2. Kila Jambo Lina wakati wake. Kufosi kuishi wakati wa mbele ni pupa. Ni kuyaharibu maisha yako.
3. Kufosi kuishi maisha ya nyuma ungali upo mbele ni kujichelewesha na kujimaliza.
4. Zipo njia nyingi niliwahi kuwaeleza za kuwatawala watu. Katika njia hizo kuna mbinu kadhaa.
5. Moja ya mbinu hizo ni kuhakikisha watu wajione wamechelewa hata kama hawajachelewa.
6. Kuwafanya watu wawe na haraka, wawe na speed ambayo kwa hakika lazima iwatumbukize mtaroni.
7. Mbuyu ulianza kama mchicha.
Meno yako yalichukua zaidi ya miaka 20 ili yakamilike katika kinywa chako.
8. Zipo sababu za mbuyu kuanza kama mchicha. Na zipo sababu za kisayansi na kimfumo kwa nini uchukue miaka yote hiyo ili uwe na meno 32 katika kinywa chako.
9. Mfumo wa maisha hautambui harakaharaka. Hiyo sio nature. Na ukiona harakaharaka ujue hiyo ni catastrophe. Kimbunga, tufani, radi, janga hilo.
10. Maisha ni fumbo. Maisha ni mkusanyiko wa taarifa nyingi za Siri na mafumbo ambayo inahitaji intelejensia(ujasusi) ili kuweza kuyaishi ipasavyo.
11. Intelejensia hahitaji uwe na pupa, haraka uhitaji kujiendea bila utulivu.
12. Nature inakawaida ya kujisahihisha, ukweli unakawaida ya kujitokeza wenyewe. Lakini sio kwa haraka.
13. Unapopitia nyakati ngumu usiwe na haraka kujinasua. Ni katika nyakati ngumu ndipo unapata fursa ya kuyajua na kujifunza maisha.
14. Kadiri unapofanya haraka kujinasua kwenye matatizo ndivyo unavyoongeza na kujifunga matatizo zaidi.
15. Vitu vinavyoonekana visikuendeshe kwani vitakutoa kwenye ramani.
Pesa, utajiri, magari, majumba, na others man-made materials.
16. Ukitulia utavipata kwa wakati na vitakupa furaha ya kudumu.
Ukiwa na pupa unaweza ukavipata lakini visikupe furaha.
17. Usifanye haraka kuoa kama akili yako haukuituliza. Haujui kwa mini unaoa.
Lakini pia usichelewe Sana kuoa.
18. Usiwe na haraka ya kuolewa lakini usichelewe pia Kuoa.
17. Wakati sahihi wa kuoa ni pale ambapo unajitafuta. Upo down, lakini unaweza angalau kupata milo walau mara mbili kwa Siku na hiyo isizidi miaka 30.
18. Halikadhalika na mwanamke. Olewa wakati wanaume wengi ndio wanakuhitaji. Ukiwa kwenye peak.
19. Ukiwa unahisi hauhitaji mwanaume ukiwa 17-25.
20. Hakunaga Mapenzi ya kweli baada ya miaka 30. Yaani ukianza kutafuta mwenza ukiwa kuanzia miaka 30 kamwe usitarajie kupata mwenza anayekupenda Ile kindaki ndaki.
21. Mapenzi ya kweli, true love ipo kuanzia kwenye Balehe 14- 24/25 hapo.
21. Kipindi cha utafutaji kinaanzia miaka 25. Na utajiri na flow ya pesa mara nyingi huanza kufunguka kuanzia miaka 30-44.
26. miaka 30-44 ndio kipindi cha accumulation ya pesa na utajiri. Huo sio umri wa mapenzi tena. Huo ni umri wa kusaka mapene.
27. Sio uanze kukimbizana na Wanawake kwenye umri usio wake.
Umri wa mapenzi unajulikana 15-25 kaa wanawake.
Wanaume 20 -30.
28. Ndio maana kijana haushauriwi kuoa single mother kwa umri huo yaani 15-44 kwa sababu ni umri unaohusu kuhangaikia maisha yako.
Umri kuhangaikia msalaba wako mwenyewe.
29. Kuoa single mother ukiwa 15-44 ni kuharakia maisha. Pupa. Kubeba msalaba ya wengine ukiacha msalaba wako.
30. Kusaidia jamii ukiwa na miaka 15-44 ni pupa. Huo sio umri wa kutoa. Ni umri WA kukusanya.
31. Sio umri wa kulea wazazi wako. Ukiwa na miaka 15-35 wengine mpaka 40 wazazi watakuwa bado hawajafika miaka 60. Watakuwa bado Wana nguvu ya kujitafutia na kujilisha.
32. Usiwalee kama wagonjwa au wazee wakati bado wananguvu na wanajiweza. Huko ni kuharakia mambo.
33. Watumie zawadi ndio lakini sio uwabebe mabegani kama wazee au wagonjwa au watoto.
34. Hutobarikiwa popote pale.
Mtu yeyote mwenye umri wa kufanya KAZI lazima afanye KAZI.
Labda awe mgonjwa.
35. Kumlisha mtu mwenye nguvu anayeweza kujilisha lakini kwa sababu zozote nje ya ugonjwa huko ni kujihujumu, kuhamasisha unyonyaji, utegemezi, na kujipa laana. Na lazima ikupate.
36. Kulea mtoto asiyewako ambaye wazazi wake wapo na wanauwezo huo sio Wema. Na kamwe hautalipwa Baraka isipokuwa laana na itajibu na utakuwa shahidi.
37. Kila mtu awajibike. Msaada uende panapostahili.
38. Ni muhimu kuzaa kwa wakati ili kuwalea watoto wako mapema vizuri ukiwa na nguvu. Ili wakishakua unapata nafasi nyingine ya kuwatunza Wazazi wako ambao tayari watakuwa ni wazee.
39. Utafutaji wa Pesa hautokani na akili ya utafutaji Bali akili ya mahusiano yako na watu pamoja na mazingira.
40. Ubahili ni kujua wakati na mahali sahihi pakuweka pesa yako. Kutokuwa na pupa. Haraka. Kutokukurupuka.
Nawatakia Siku njema.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam