Maisha Haya...!!Nimejfunza Kpya Hapa...Hebu 2shee!

Majigo

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
5,519
1,825
Mimi ninakaa na mwanaume ambaye kwa sasa nimeshazaa naye watoto wawili mapacha wanamiezi minne, kabla ya ujauzito mapenzi yetu yalikuwa motomoto lakini baada ya kubeba mimba mwanaume huyu akaanza vituko vya ajabu,
mara anachelewa kurudi, hela ya matumzi hatoi hapo nikiwa na mimba mpaka najifungua vituko tu haviishi.

kuna wakati siku moja akaniletea mwanamke ndani akaniambia ni dada yake mtoto wa baba yake mkubwa.
Yule dada nilimkaribisha vizuri nikijuwa ni wifi yangu kumbe alikuwa mwanamke wa huyo baba watoto wangu, nilikuja kujuwa baada ya siku moja nikamwambia baba watoto natoka kwenda kufanya mazoezi kunyoosha miguu nikawahi kurudi kabla ya saa yangu ya kawaida nikawakuta chumbani kwetu wakichuma tunda la ndoa!!!! sikuamini macho yangu nilijikuta nimenyanyua chupa ya pafyumu na kumpiga nayo baba watoto wangu kichwan ndipo waliposhtuka.
Nilipomuuliza akaniambia kwamba kwao wamakonde ni ruhusa kulala na dada ambaye sio wa tumbo moja, huku akiniomba msamaha nilipokataa kumsamehe akaniambia kama sitaki hawezi kunibembeleza niachane naye, akaondoka na huyo dada!!!!!

Wakarudi wamelewa nilikuwa nimelala kitandani akanishusha nilale chini wao walale kitandani kwakuwa nilikuwa na tumbo kubwa sikutaka kubishana naye maana angeishia kunipiga
basi nilishuka nikalala chini, na hata nilipojifungua akawa ananiambia utalala
na hivyo vipaka vyako chini usitubane kitandani!!!! (kweli leo mimba tuliyoitunga kwa furaha imezaa vipaka???)

Siku nikajifungua yule dada hapo hajaondoka bado, nikawa nalala sebleni sasa na watoto maana tulikuwa tumepanga kwenye chumba sebule jiko na choo, wazazi wangu wapo kijijini hata nikiwaambia
hawatakuwa na lakunisaidia zaidi tu ya kuniambia niondoke na nitaenda wapi na hawa watoto wachanga!!
Hata baada ya kujifungua baba watoto hakuwa ananiachia hela ya matumizi natapatapa kwa majirani kuomba kufanya kazi nikiwa nimebeba watoto wangu nipate japo hela ya kuweza kula watoto wanyonye,

kiukweli mimi sikusoma nilikutana naye kwenye mziki tukapendana maana nilijuwa anakazi nzuri kwamba atanisaidia mbeleni kumbe nilijitumbukiza kwenye mto. Madharau yake yakazidi nikashindwa vumilia nikaamua kuondoka kwenda kwa mama yangu mdogo sinza huko nilikaa kwakuwa hakuwa na mume akanisaidia kulea watoto (sikuwahi kusikia kutoka kwa baba yao mpaka sasa wanamiaka mitano), huku nikifanya kazi katika saluni ya kiume nikakusanya hela nikajiendeleza kusoma kompyuta nikasoma kwa bidii nikamaliza, nikasoma qt nikamaliza sasa nimepata kazi katika stationary moja ambayo ndio nilpo,
basi mwenyewe
nawahudumia watoto na mama yangu mdogo vizuri tu maana sijahama. Sasa juzi nikiwa natoka kazini nikautana na baba watoto wangu kituo cha basi yani nilivyomuona nilitaka kulia kwasababu alivyokonda na kuchakaa nikamsalimia wakati naondoka akaniomba namba ya simu ili apige aongee na watoto wake na mbaya zaidi kilichonisikitisha
akaniomba hela ya kula jioni!!!!!!!!!!!
akaniambia tokea nimeondoka maisha yamekuwa magumu sana kazi alifukuzwa nyumba akashindwa kulipa kodi akafukuzwa vitu ilibidi auze ili apate chakula zilipoisha ndio anabangaiza na maisha akitafuta kazi mpaka leo hajapata. Alivyowapigia akaomba kuja kuwaona alipofika akaanza kulia na kuwaomba msamaha mbele ya mama yangu mdogo akamuomba mama yangu mdogo amuombee msamaha kwangu turudiane tulee watoto!!!!
Hata aibu hana kasahau kabisa mateso yote aliyonifanyia hana hata aibu Rohoni sina hata hamu naye, ila watoto tokea wamuone baba yao na anavyojishauwa kuja kuwaona mara kwa mara wanamlilia kila akiondoka, mama yangu mdogo ananiambia nisiwe na roho ya chuma nimsamehe kwa ajili ya watoto kweli mtu unaweza kumsamehe vipi naanzaje???

HII STOR NI YA KWEL NA NILSMULWA NA NIKAOMBWA USHAUR NA HUYU DADA...
NIMEONA NISHEE NANY!
 
Hii stori imekaa kimtego...............
Mambo ya unyumba yana vibweka vyake, na kumpa ushauri mtu kama huyo inatakiwa uwe makini sana kwani unaweza kupata matokeo tofauti kabisa na ushauri wako. Kwa jinsi binti alivyojieleza mie naona kuna dalili zote za kurudiana na huyo bwana.
Wewe mwambie ausikilize moyo wake, usije akabeba lawama bure.

Wanawake wana huruma we acha tu..................................
 
Umeona Eeeh! yaan MTAMBUZ Hii Hoja Nzto Kweli!
 
Umeona Eeeh! yaan MTAMBUZ Hii Hoja Nzto Kweli!

Basi mwenyewe nawahudumia watoto na mama yangu mdogo vizuri tu maana sijahama. Sasa juzi nikiwa natoka kazini nikautana na baba watoto wangu kituo cha basi yani nilivyomuona nilitaka kulia kwasababu alivyokonda na kuchakaa nikamsalimia wakati naondoka akaniomba namba ya simu ili apige aongee na watoto wake na mbaya zaidi kilichonisikitisha
akaniomba hela ya kula jioni!!!!!!!!!!!
akaniambia tokea nimeondoka maisha yamekuwa magumu sana kazi alifukuzwa nyumba akashindwa kulipa kodi akafukuzwa vitu ilibidi auze ili apate chakula zilipoisha ndio anabangaiza na maisha akitafuta kazi mpaka leo hajapata. Alivyowapigia akaomba kuja kuwaona alipofika akaanza kulia na kuwaomba msamaha mbele ya mama yangu mdogo akamuomba mama yangu mdogo amuombee msamaha kwangu turudiane tulee watoto!!!!
kama ukisoma hayo maelezo kwa makini kabisa unaona dhahiri ni jinsi gani anajaribu kutaka kuhalalisha iwapo atarudiana naye.....
Hapo utasikia, "ameshajifunza hatarudia tena" au "hakuna binadamu mkamlifu, kila mtu hukosea"
Kwa ujumla kutatafutwa misamiati yote ya kuhalalisha kurudiana na huyo baba watoto wake, kisa eti amezaa naye..... Kuzaa nayo nongwa...! Mbona hata wendawazimu wanazaa na kamwe baba wa watoto hao hawajulikani na bado wanaishi seuze yeye pamoja na kutupwa jalalani alimudu kunyanyuka na kusonga mbele na akapata mafanikio, lakini leo anatujia hapa na stori za kututega......mh!
Huyu anatafuta tu kuhalalisha dhamira yake, lakini maamuzi tayari anayo moyoni mwake.
 
dada zangu kuweni makin na wanaume wa kuokota sijui kwenye mziki, disko, bar, barabaran, mbaya zaidi unatokea kumwamin na kuishi naye + kumzalia watoto, this is so stupid. sio kila mwanaume ni mwanaume wengine wanaume suruali, kwa mfano angalia huyu mpuuzi mchumba wake/mkewe ana ujauzito alafu yeye anamletea changudoa ndani tena ktk kitanda anacholala mkewe.
 
Ishu Ya Watoto Ni Tata Hackwambie M2
Hasa Wakjua Baba Yao Yupo
Ila Alichokosea Ni Kuruhusu Huyu Mwendawazmu(alyeruhusu Hawara Kitandan Mwa Mkewe Mwenye Uzto Wake)
Akawa Na Mawasiano Na Wanae!
 
dada zangu kuweni makin na wanaume wa kuokota sijui kwenye mziki, disko, bar, barabaran, mbaya zaidi unatokea kumwamin na kuishi naye + kumzalia watoto, this is so stupid. sio kila mwanaume ni mwanaume wengine wanaume suruali, kwa mfano angalia huyu mpuuzi mchumba wake/mkewe ana ujauzito alafu yeye anamletea changudoa ndani tena ktk kitanda anacholala mkewe.

Kwel Bab,Huu Ni Uchanganykeni!
 
Huo wembamba wake ni wamaisha magumu tu au na kamdudu tayari ameshapata maana najaribu kuunganisha matukio kwa jinsi alivyokuwa anakuletea changudoa ndani halafu na wewe umekutana naye disco!Hebu kabla ya maamuzi yeyote na afya yake uicheki kwanza. Kuhusu kurudiana nakushauri fuata nafsi yako inavyohisi maana mwisho wa siku ni wewe na yeye.
 
Mkuu Hapo Umeongeza Longo La Maana!
 
Aaah wapi! Hana mapya huyo, pandisha vioo!
Kilichobadilika hapo ni yeye kufulia, asingefulia wala asingekuwa na habari na wewe wala watoto.
Yakimnyookea tu mule mule. Uamuzi ni wako!
 
Back
Top Bottom